Wabunge 30 wa Zanzibar watetea Muungano; Wataka wasioutaka wang'atuke! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wabunge 30 wa Zanzibar watetea Muungano; Wataka wasioutaka wang'atuke!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by abdulahsaf, Aug 11, 2012.

 1. a

  abdulahsaf JF-Expert Member

  #1
  Aug 11, 2012
  Joined: Aug 31, 2010
  Messages: 859
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  • Moto mkali dhidi yao wawashwa
  • Wadaiwa kuvunja sera ya chama

  NI KAMA tayari kuna makubaliano ya kuwajibishana ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) juu ya utoaji wa maoni ya Katiba mpya, kutokana na kauli za kukinzana juu ya aina ya Muungano wanaoutaka.

  Wakati vitisho vya kuwafukuza uanachama viongozi na wanachama wake wanaopinga mfumo wa Muungano wa serikali mbili vikiibuka Zanzibar, mjini Dodoma nako wabunge wa CCM waliitisha mkutano na waandishi wa habari jana na ajenda ikawa ni hiyo hiyo, kufukuza uanachama wanaoupinga sera ya Muungano wa serikali mbili.

  Katika matukio yote mawili, viongozi waandamizi wa Chama, wakiwamo walioko katika Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) kwa sasa wamewaambia viongozi na wanachama hao kuwa ni afadhali wakarejesha kadi za uanachama badala ya kusubiri kufukuzwa na chama.

  Akifungua mkutano Mkuu wa Jimbo la Kitope katika Mkoa wa Kaskazini Unguja jana Kisiwani Zanzibar, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi, aliwataka wanaoupinga mfumo wa Muungano wa sasa wajiondoe CCM kabla ya kufukuzwa.

  Balozi Seif alisema wanachama na viongozi ambao wameamua kwenda tofauti na sera ya chama hicho kuhusu mfumo wa Muungano na kwamba wamekuwa pia wakienda kinyume na Ibara ya 221 ya Ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010.

  Balozi Seif ambaye pia Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) na Kamati Kuu (CC), alisema CCM ni chama tawala na kimepata ridhaa ya kuongoza nchi baada ya kuchaguliwa na wananchi, hivyo haiwezekani kutokea mwanachama au kiongozi akaenda kinyume cha sera yake.

  Aliwataka wanachama wa chama hicho kuhakikisha kwamba Zanzibar inaendelea kudumisha amani na umoja wa kitaifa chini ya Muungano wa Tanzania.

  "Wale wanaotaka kutuvurugia chama chetu na Muungano wetu waturejeshee kadi zetu, kwa nini wanachama hao wanasubiri mpaka wajadiliwe kwenye vikao vya chama au vile vikao vya maadili. Ya nini kutuvurugia chama chetu wakati nafasi za kung'atuka zipo wazi?" alihoji Balozi Seif huku akishangiliwa wajumbe wa mkutano huo.

  Alisema Taifa hivi sasa linapita katika kipindi kigumu kutokana na kuibuka kwa vikundi vinavyofanya kazi ya kushawishi wananchi na hasa vijana kujiingiza katika vitendo vya uvunjifu wa amani kitendo ambacho alisema ni kinyume cha misingi ya utawala wa sheria.

  Aidha, alisema kwamba wanachama wa CCM lazima wawe makini kupitia uchaguzi mkuu wa chama kwa kuhakikisha wanachagua viongozi makini na waadilifu ambao watasadia kuimarisha umoja, amani na mshikamano.

  Balozi Seif alitahadharisha kwamba hivi sasa jamii inashuhudia matusi ya nguoni yanayoendelezwa na baadhi ya makundi ya watu dhidi ya viongozi wa serikali na chama, hali ambayo alisema kama jamii hiyo haitakuwa makini, Taifa linaweza kutumbukia katika fujo na hatimaye maangamizi.

  "Tunakotoka kubaya, sote ni mashahidi kwa sababu familia na hata ndugu wa karibu walikuwa hawaulizani hali na hata maziko hawaendeani. Kwa kweli tusifikie tabia hii kuiruhusu irejee tena," alisema Balozi Seif.

  Alisema CCM Zanzibar kitaendelea kuunga mkono mfumo wa Muungano wa serikali mbili na kuwataka wanachama na viongozi wa CCM kuheshimu sera na katiba ya chama hicho.

  WABUNGE NAO WACHARUKA

  Hayo yakitokea Zanzibar, wabunge wa CCM kutoka Zanzibar wamewajia juu na kuutaka uongozi wa chama hicho kuwachukulia hatua ya kinidhamu baadhi ya viongozi wa serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wanaotaka kuuvunja Muungano.

  Akizungumza na waandishi wa habari mjini Dodoma jana, Mwenyekiti wa wabunge kutoka Zanzibar, Dk. Mohammed Seif Khatib akiwa amefuatana na wabunge wapato 30 kutoka visiwani, alisema wao kama wabunge wanashangaa kusikia viongozi hao wakitamka maneno makali ya kuvunjwa Muungano huku wakitazamwa.

  Alisema wao kama wabunge waliopata ushindi kutokana na Ilani ya CCM inayotamka wazi kuunga mkono wa serikali mbili, wataendelea kutetea msimamo huo kwa sababu wanachoamini kama yatafanyika mabadiliko mbalimbali kwenye Katiba, hatimaye kila upande utapata haki yake ya msingi.

  "Kuna baadhi ya viongozi wanashabikia kuvunjwa kwa Muungano, hilo sisi wabunge tunawaachia viongozi wa ngazi za juu kuhakikisha wanachukua hatua za kinidhamu ili kukomesha tabia hiyo," alisema Dk. Khatib.

  Dk. Khatib alisema wanaamini mfumo wa serikali mbili una faida kubwa kwa Zanzibar na watu wake ikiwa utawekewa mfumo wa kikatiba wa utekelezaji katika kuondoa kabisa kero hizo zilizoko katika Muungano.

  Alisema kuwa ilani ya uchaguzi ya CCM waliotumia kuombea ridhaa kwenye majimbo yao, inaweka wazi kuhusiana na mfumo wa serikali mbili, hivyo kulingana na ilani hiyo wote kwa pamoja wanaunga mkono msimamo huo.

  Hata hivyo, aliwataka wananchi wa Zanzibar kuaacha kujikita katika suala moja la Muungano wakati wanapotoa maoni yao juu ya Katiba mpya, kwani kuna maeneo mengine muhimu ambayo wanayaacha bila kuchangia.

  Tamko hilo limekuja kufuatia baadhi ya wanasiasa, wakiwemo makada wakongwe wa CCM Zanzibar kutoa maoni yanayokwenda tofauti na msimamni wa chama hicho kuhusiana na mfumo wa Muungano.

  Wiki iliyopita, mmoja wa waasisi wa Mapinduzi ya Zanzibae, Ali Nassoro Moyo na Waziri Asiye na Wizara Maalum, Mansour Yusuf Himid, walisema kuwa Muungano wa sasa unakabiliwa na kasoro nyingi na kupendekeza uanzishwe Muungano wa mkataba.

  Mbali na Moyo na Mansour, viongozi wengi wa Chama cha Wananchi (CUF) wamekuwa wakitetea Muungano wa mkataba ambao wanasema utasadia Zanzibar kuwa na bendera na kiti chake katika Umoja wa Mataifa (UN).

  Kadhalika, Jumiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kislamu (Jumiki) imeanzisha kampeni misikitini za kutaka Zanzibar kujitenga na Muungano.

  Hata hivyo, tamko la Balozi Seif linakwenda kinyume cha maelekezo yaliyotolewa na Tume Warioba ambayo inakusanya maoni ya Katiba mpya, ambayo iliwatoa wasiwasi Watanzania wote na kuwataka watoe maoni yao kuhusu katiba bila woga.

  Jaji warioba alisema kuwa tume yake itawasikiliza watu wote, wakiwemo wanaoupinga Muungano.

  CHANZO: NIPASHE
   
 2. a

  abdulahsaf JF-Expert Member

  #2
  Aug 11, 2012
  Joined: Aug 31, 2010
  Messages: 859
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Hili ndio tatizo la ccm kutokujuwa democrasio na freedom speech, ukiwa eti kada wa ccm nilazima uwe na mawazo ya ccm hii ni mawazo mgando tunayaita.
   
 3. Nyakageni

  Nyakageni JF-Expert Member

  #3
  Aug 11, 2012
  Joined: Feb 1, 2011
  Messages: 13,962
  Likes Received: 1,284
  Trophy Points: 280
  Shauri yao! Adui wa Muungano ni CCM, ikifa Zenj itapata nchi yao
   
 4. M

  Mnyonge Namba1 JF-Expert Member

  #4
  Aug 11, 2012
  Joined: Jan 27, 2012
  Messages: 402
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Mimi nataka TANGANYIKA YETU IREJESHWE halafu tuunde SERIKALI TATU. 1.S/ZANZIBAR. 2.S/TANGANYIKA na 3.S/SHIRIKISHO YA JMTZ.
   
 5. t

  timbilimu JF-Expert Member

  #5
  Aug 11, 2012
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 4,785
  Likes Received: 155
  Trophy Points: 160
  Naona vibaraka wa Tanganyika wanaoitawala Zanzibar wameanza mikwara. Hapo hakuna ilani wa sera ya chama,hawa jamaa wamekua wanafaidi vya dezo toka Tanganyika ndiyo sababu wanalilia muungano wa serikali mbili.
   
 6. kibogo

  kibogo JF-Expert Member

  #6
  Aug 11, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 9,481
  Likes Received: 790
  Trophy Points: 280
  Thubutu! hilo la kufukuzana ndani ya CCM halipo na halitokuwepo na haliwezi kutokea, wote sio waadilifu kila mmoja anajua makosa ya mwenzake yaliyopelekea nchi yetu kuwa hapa tulipo hivyo wanaogopana.
   
 7. BONGE BONGE

  BONGE BONGE JF-Expert Member

  #7
  Aug 11, 2012
  Joined: Oct 19, 2011
  Messages: 3,401
  Likes Received: 1,525
  Trophy Points: 280
  .........sijawahi kuona watu waoga kama wa chama changu CCM kupokea changamoto, hatuwezi kuwa na akili moja, tukijiaminisha hivyo tutakuwa tunaajiaminisha ujinga.....
   
 8. S.Liondo

  S.Liondo JF-Expert Member

  #8
  Aug 11, 2012
  Joined: Apr 20, 2011
  Messages: 2,160
  Likes Received: 675
  Trophy Points: 280
  Muungano feki kabisa, tena sioni faida yeyote tunayoipata kwa kuwa nao. Wakitaka muungano wa kweli ni lazima uwe wa serikali moja.
   
 9. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #9
  Aug 11, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,364
  Likes Received: 6,394
  Trophy Points: 280
  Nani atamfunga paka kengele? Kama Rais wa Zanzibar anavumilia waasi ndani ya serikali yake na Rais wa Muungano (mwenyekiti wa CCM Taifa) naye yuko kimya hawa wabunge wana nguvu gani za kupiga mkwara? Itakuwaje kama rais atakuja na kusema "ni haki yao kutoa maoni"...
   
 10. m

  matambo JF-Expert Member

  #10
  Aug 11, 2012
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 728
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  namuonea huruma Dk. Mohammed Seif Khatib maana huyu baadhi ya wazanzibari humtukana kuwa ni m-bara na hivyo hasimamii matakwa ya wazanzibari, na siku si nyingi twaweza sikia vikaratasi vimesambazwa soko la darajani wakimtukana
  lakini ijapokuwa muungano wa serikali mbili ni itikadi y aCCM, si vibaya kuwa na mawazo mbadala na ndio maana twataka maoni ya wananchi juu ya katiba, sasa haa wabunge wakishaamua wao wanataka serikali 2 tu, then wazanzibari wakitaka serikali 3, je kwenye constitutional assembly watafuata yepi? matakwa yao au yale ya wananchi?
   
 11. jamesbond007

  jamesbond007 Member

  #11
  Aug 11, 2012
  Joined: Jun 27, 2012
  Messages: 36
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mmmmmmmmmmm! hao cc tunawajua kuwa wanachojali ni matumbo yao tu kwa kusheheni miposho wanayolipwa bungeni sasa wengi wao taaluma na fani zao hazieleweki yaani kuna wengine kati yao hata form 2 wakufika wamekuwa wabunge kwa ujinga wa ccm-zanzibar tu!

  sasa tunachosikia hivyo cc wazanzibar hatushangai hata kidogo kwani tunajuwa kuna mamluki na wanafiki ndani ya kundi la wazanzibar ambao wanajali maslahi yao binafsi tu! ila wajue mwisho wao unakaribia!
   
 12. Falcon

  Falcon JF-Expert Member

  #12
  Aug 11, 2012
  Joined: Aug 16, 2010
  Messages: 250
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mwanakijiji kila siku zikizidi kusonga mbele umekuwa na mawazo kama vile unatumia (Bob Marley)kwanza ndio uingiwe na mawazo ya kuandika nakunuku hapa unaposema Rais wa zanzibar anavumilia wasi ndani ya serekali yake huoni hata fedheha mtu mzima kama wewe kufedheheka unashindwa hata kufikiri matukio yanayotoke katika nchi unyoaita ni nchi yako ?wacha ni kukumbushe hivi Rasi wa Tanzania anaposhindwa kuwajibisha viongozi anaowaongoza ambao Dunia inawatambuwa kuwa ni Wizi susu hilo unalitafsiri vipi hilo? usigeuke muwamba ngoma nothing last forever tumeona hapa nini kilitokea katika nchi za east Europe .for your information, its not the size of the ship,its the motion of the ocean
  [h=3][/h]
   
 13. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #13
  Aug 11, 2012
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,188
  Trophy Points: 280
  Nje ya Muungano Zanzibar itakuwa sawa na Somalia...ni muungano ndio unawapa wengine wao jeuri ya kupayuka ovyo kama wanavyofanya wakabaki salama. Peke yao? Loo, mbona itakuwa mshike mshike!
   
 14. Ndoa

  Ndoa JF-Expert Member

  #14
  Aug 12, 2012
  Joined: Dec 2, 2011
  Messages: 985
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Wabunge toka zanzibar wana haki ya kutetea muungano kwani wao wamepata huo ubunge kupitia huo huo muungano.
   
 15. Head teacher

  Head teacher JF-Expert Member

  #15
  Aug 12, 2012
  Joined: Mar 10, 2012
  Messages: 1,811
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Wabunge wa Zanzibar wanaangalia fedha wanayopata katuka vikao, mishahara, na ajira za SMT
   
 16. M

  Mzee wa Usafi JF-Expert Member

  #16
  Aug 12, 2012
  Joined: Apr 16, 2008
  Messages: 634
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 45
  Nadhani kindumbwe dumbwe kitakuwa kwenye hilo bunge la katiba kwani nina imani kubwa kabisa wajumbe wa bunge hilo kutoka au walio karibu na magamba wataingia na msimamo wa chama...sisi nasi tutataka tofauti na msimamo wa chama....hakuna katiba mpya tanzania..."let us wait and see....time will reveal"
   
 17. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #17
  Aug 12, 2012
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,601
  Likes Received: 18,619
  Trophy Points: 280
  Huko Zanzibar kuna Wazanzibari, na Wanzanzibara, Wazanzibari ndio waliochoshwa na kero za muungano na ndio walio nyuma ya kikundi cha Uamsho na Wanzanzibara ndio hawa akina Balozi Seif Iddi na Mohamed Seif Khatibu wanaoutetea muungano wa serikali mbili kwa sababu wao ni benefisharies wa mfumo huu wa muungano, na utetezi wao wa muungano wa serikali mbili, sio utetezi chochote, sio utetezi lolote, zaidi ya kujikomba komba kwa CCM kwa nia ya kutetea tuu matumbo yao ili kimoyo moyo ukweli wanaujua kuwa Muungano wa serikali mbili doesn't work right!. Muungano wa ukweli ni wa ama serikali moja (unitary union), au serikali tatu (federal) kinyume cha hapo ni kutwanga maji kwenye kinu!.

  Namuomba sana Jaji Warioba, ayarudi ipasavyo haya majitu majinga yanayotaka kuharibu mchakato wa maoni ya katika kwa kuwatisha wenzao wasitoe maoni fulani ati watafukuzwa CCM!, who is CCM kwenye maoni ya katiba impya?. Kama Wazanzibari wamechoshwa na kero za muungano zisokwisha kwa miaka 48 sasa, hii ndio mara ya kwanza wamepata fursa ya kutoa maoni yao kuhusu huu muungano wenye mushkeli, waachwe watoe maoni yao kwa uhuru, bila kutishwa eti watafukuzwa CCM, kwenye mchakato wa katiba mpya, CCM is nothing, but a party kama ilivyo CUF, japo ni chama tawala, ni chama tawala nchi na sio tawala tume!.

  Wazanzibari wa kweli wenye uchungu na nchi yenu, endeleeni kutoa maoni yenu kwa uhuru, sisi Watanzania wenye mapenzi ya dhati na nchi yetu, tunakusikilizeni kwa makini, na hatimaye tutakupeni kile mnichokitaka ili nazi tuweze kusonga mbele kwa amani na usalama.

  Tena tunawahikikishieni msiwe na hofu kabisa, tutaendelea kuwaleteeni maendeleo makubwa zaidi ya hayo tuliyoshawapatiya. Baada ya kupitisha under sea cablles za umeme, maadamu sasa bara tuna gesi asilia kutoka Mtwara, na bomba linajengwa kutoka Mtwara kuja Dar, likishafika, tutawajengea na under sea bomba la gesi kuja Zanzibar na pemba, wale wanaopikia makumbi, wote watapikia gesi!.

  Toeni maoni kwa uhuru, hayo ni maoni ya watu na sio maoni ya vyama, japo vyama navyo vina uhuru wa kupeleka maoni yake kama vyama!.

  Pasco.
   
 18. M

  Mzenji73 JF-Expert Member

  #18
  Aug 12, 2012
  Joined: Jan 10, 2009
  Messages: 341
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  "astaghfirullah, nimo kwenye saumu, hao wabunge wanapaparika na kupapatika. Huyo mwenyekiti Mohammed Khatib mmh! (nimo kwenye saumu) ... Rais wetu Dr. Shein tayari ameshatueleza wazi kuhusu kutoa mawazo yetu bila woga, sijui walikuwa wapi!? Hata M/kiti wao wa CCM amesema kauli kama hiyo, ni juzi tu M/kiti wa tume, jaji Warioba kaelezea kuhusu vyama vinavyowalazimisha wanachama wake kuwasemea sera zao .... almuradi kipindi hiki viroja vitakuwa vingi ... (dua zetu zinaanza kuonesha miujiza yake) ... hapa sijui paka gani afungwe kengele tena!"

   
 19. D

  Deofm JF-Expert Member

  #19
  Aug 12, 2012
  Joined: Feb 27, 2012
  Messages: 383
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Na muungano ukifa hawana mshahara kwani kwao kuna serikali inayojitosheleza. wao hawatahitajika popote pale.
   
 20. M

  Mzenji73 JF-Expert Member

  #20
  Aug 13, 2012
  Joined: Jan 10, 2009
  Messages: 341
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  "umeona eenh?! leo hii wafukuzwe huo ubunge utaona jinsi watakavyokuwa watetezi wa JWZ, ulafi na kujali kwa watu matumbo yao ndio imekuwa tatizo kubwa sana huku kwetu"
   
Loading...