Elections 2010 Wabunge 22 of cuf vs 22 of chadema

Hapo nadhani kuna mkanganyiko,inawezekana bado wanajaza hizo data.kwa sababu mpaka sasa wapinzani wamefikia 53,ccm wenyewe walisema pamoja na vyombo vya habari,kwa maana hiyo(nccr-4,udp-1,tlp-1,chadema na cuf ni 47,hivyo mmoja wao ana 23 na mwingine ana 24)
 
CUF ana viti 24 na CHADEMA 23, lakini CHADEMA kitakuwa chama kikuu cha upinzani maana kitapata viti maalum vingi zaidi kwa sababu mgombea urais wake alipata kura nyingi zaidi ya yule wa CUF.
 
ISSUE YA CUF NI A BIT CONTRAVERSY...KWA SABABU TAYARI WABUNGE WENGI WANATOKA ZANZIBAR AMBAKO KUNA SERIKALI YA UMOJA[CCM/CUF kama zamani TANU/ASP].....NINA SHAKA KUBWA NA INTERGRITY YAO KUWA OFFICIAL OPPOSITION .........ILA HILI LIKISHAWEKWA SAWA NI VEMA SASA VYAMA VYOTE VYA UPINZANI VIUNGANE ILI KUUNDA UPINZANI RASMI BUNGENI WENYE NGUVU!!
 
......chadema na cuf ni 47,hivyo mmoja wao ana 23 na mwingine ana 24)
ili kupata 47 ni lazima 23 ijumlishwe na 24, haiwezekani mmoja akawa na 22 mwingine akawa na 25, au mmoja akawa na 21 mwingine 26?
 
CUF wataongeza viti vyao kwenye majimbo yaliyoahirisha uchaguzi kule Pemba hivy kuendelea kuwa kiongozi wa upinzani Bungeni.
 
ISSUE YA CUF NI A BIT CONTRAVERSY...KWA SABABU TAYARI WABUNGE WENGI WANATOKA ZANZIBAR AMBAKO KUNA SERIKALI YA UMOJA[CCM/CUF kama zamani TANU/ASP].....NINA SHAKA KUBWA NA INTERGRITY YAO KUWA OFFICIAL OPPOSITION .........ILA HILI LIKISHAWEKWA SAWA NI VEMA SASA VYAMA VYOTE VYA UPINZANI VIUNGANE ILI KUUNDA UPINZANI RASMI BUNGENI WENYE NGUVU!!

Umesema kitu cha msingi sana. Tusitegemee wabunge wote waliopo kambi ya upinzani watakuwa wapinzani. Naamini hata CCM, siyo wabunge wote walioko ndani ya chama tawala watakuwa yes man. Hii inatokana na ukweli kuwa wengi wamehangaika sana kuyapata hayo majimbo. Hivyo lazima wawathibitishie wapiga kura wao kwamba wanafanya yale wanayotakiwa kufanya.
 
tunachotaka ni kuona kila mbunge anatetea maslahi ya wananchi na kupambana vikali na mafisadi, lakini kama watajivunia uwingi pasipo kuchambua hoja kwa makini kama mfano wa dk.Slaa. Wingi wao utakuwa ni sawa na wingi wa inzi kwenye kinyesi.
 
Kwa kawaida, CUF hawapaswi kuongoza kambi ya Upinzani kwa ajili ya Umoja waliounda kule Zanzibar. Hii ina maana hata serikali ya huku Bara itakuwa kama wanaushirikiano fulani hivi. Hivi, kama wakiongoza kambi ya upinzani hawawezi kuwa wapinzani wa kweli. Lakini pia, itawachanganya na maslahi yao kule Zanzibar.

Ukweli ni kwamba, muundo wa bunge kipindi hiki una changamoto sana. Ningeshauri Chadema na NCCR Mageuzi wange kaa pamoja na kuunda kambi ya upinzani. Tatizo ni kwamba vyama hivi havina uhusiano wa karibu. Ikizingatiwa hivi sasa vina shutumiana hata kutishiana kupelekana mahakamani. Tusubiri tuone!
 
Haya ndiyo majimbo ya chadema.1.Ubungo2.Kawe3.Arusha mjini4.Moshi mjini5.Hai6.Karatu7.Rombo8.Mbulu9.Arumeru magharibi10.Iringa mjini11.Mbeya mjini12.Mbozi mashariki13.Bukombe14.Musoma mjini15.Kigoma kaskazini16.Ukerewe17.Maswa mashariki18.Maswa magharibi19.Singida mashariki20.Ilemela21.Nyamagana22.Meatu23.Biharamulo magharibi24.Mpanda kati.Hili la mwisho naomba kuwa asured.
 
CUF wataongeza viti vyao kwenye majimbo yaliyoahirisha uchaguzi kule Pemba hivy kuendelea kuwa kiongozi wa upinzani Bungeni.

Nafasi ya kuwa official opposition inatokana na idad ya kura za urais na si namba ya wabunge waliopatikana.
 
CUF ana viti 24 na CHADEMA 23, lakini CHADEMA kitakuwa chama kikuu cha upinzani maana kitapata viti maalum vingi zaidi kwa sababu mgombea urais wake alipata kura nyingi zaidi ya yule wa CUF.

You belong here at JF.Good analysis.
 
Majimbo kama ya kilombero,mbozi west,segerea etc CHADEMA wakikomaa mahakamani uchaguzi ukirudiwa wanaweza chukua ayo maeneo
 
mbunge mmoja wa CHADEMA ni sawa na wabunge 12 wa ccm, na mbenge mmoja wa CHADEMA ni sawa na wabunge 4 wa cuf KWENYE MCHANGO WA MAWAZO.....
 
Back
Top Bottom