Wabunge 19 waliovuliwa Uanachama na CHADEMA washiriki kikao cha Bunge leo

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
3,141
2,000
Wale wabunge 19 wa Viti Maalumu wanaotokana na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), asubuhi hii wamefika na kuendelea na kikao cha Bunge kilichoanza leo Jumanne, Februari 2, 2021 Jijini Dodoma.

Itakumbukwa Wabunge hao tayari walishavuliwa uanachama na chama chao mwishoni mwa mwaka jana kwa madai ya kukiuka utaratibu wa chama chao.

Wabunge hao ambao ni pamoja na Halima Mdee na Ester Bulaya, wametinga mjengoni wakiwa wamevalia mavazi meusi huku Mdee akiwa amevaa barakoa kwa lengo la kujikinga na maambukizo ya virusi vya corona.

Hata hivyo kabla ya kuanza kikao cha Bunge, Waziri wa nchi ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi na Wenye ulemavu, Jeniste Mhagama aliwaomba watoke nje kwanza.

Spika Job Ndugai ameomba wabaki nje kwanza na baada ya dua ameanza kuwaita akianza na wabunge watano wa kuteuliwa, kisha wakaingia wabunge watano wa ACT.

Mwisho waliitwa wabunge 19 wa Chadema wakiongozwa na Ester Matiko na Cesilia Pareso.

Wabunge Halima Mdee na Ester Bulaya hawakuwa miongoni mwa walioingia mapema leo.


1612248999791.png
 

USSR

JF-Expert Member
Jul 15, 2015
5,253
2,000
Hapa swali la Ester bulaya linajibiwa wanawatetea watanzania shida iko wapi?
 

FUSO

JF-Expert Member
Nov 19, 2010
22,246
2,000
Esta bulaya kazi aliyotumwa kaimaliza - Balaza Kuu halina hata haja ya kuwasikiliza hawa COVID-19 maana lengo lao halikuwa kuulilia uanachama lah hasha, lengo lao ni uanachama wao kuendelea kuwepo ili ku justify ubunge wao feki.

Endapo Balaza kuu litakaa na kubariki kuwafuta uanachama basi watakimbilia mahakamani kesho yake kulalamika kwamba hawajatendewa haki, Mahakama itasema waendelee na uanachama wao hadi shauri lao litakapoisha - kichekesho shauri litakwisha siku moja kuamkia uchaguzi mkuu wa 2025 - kwa akili nani mshindi hapo!

Kuweni makini sana na wanawake - hata vitabu vya dini vinasema kabisa kwamba ishi na mwanamke kwa AKILI.

1 Petro 3:7

Kadhalika ninyi waume, kaeni na wake zenu kwa akili;
 

binbaraghash

JF-Expert Member
Apr 6, 2014
3,244
2,000
Ivi mbona kuna Clip nimesikiliza Juzi juzi hawa Wabunge 19 baraza lao kuu wameshawarudishia uwanachama wao?? Ivi Baraza wamekubaliana waendelee na ubunge wao ama inakuwaje naona sielewi hapa imekaaje hili sakata? naomba ufafanuzi
 

gachacha

JF-Expert Member
Jul 12, 2015
1,827
2,000
Ruzuku imechukuliwa mbona kwenye uchaguzi wanaoita fake, ila tuache kuwasakama hawa mademu acha wapige kazi mjengoni ajira hii tamu sana.

Hilda Newton anatamani kupasuka maana angekuwemo saivi mjengoni
 

Ngongo

JF-Expert Member
Sep 20, 2008
14,396
2,000
Kama CHADEMA wangekuwa makini wangeomba tafsiri ya Mahakama kuhusiaana na uhalali wao kuwakilisha chama wakati si wanachama.
 

radika

JF-Expert Member
Jul 15, 2014
19,855
2,000
Si tuliambiwa wapinzani wanachelewesha maendeleo wanatakiwa bungeni ccm
 

Chakaza

JF-Expert Member
Mar 10, 2007
36,520
2,000
Kama CDM wangekuwa makini wangeomba tafsiri ya Mahakama kuhusiaana na uhalali wao kuwakilisha chama wakati si wanachama.
Mkuu haita saidia katika kipindi hiki. Ni kukubali yaishe kwa sasa, lakini kwa vile jinai haina expired date kuna siku Ndugai atakuja kubebwa kutokea kijijini kwake huko Kongwa kuja kujibu mashtaka ya kukanyaga katiba aliyo APA.

Kwa taarifa kuvunja katiba ni kosa kubwa sana Ila tunaliona dogo kwa sasa kwa vile hajawahi shtakiwa mtu
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom