lukindo
JF-Expert Member
- Mar 20, 2010
- 8,466
- 9,028
Matumaini ya Watanzanuia kuwa na umeme wa uhakika, yameanza kuonesha nuru baada ya Ijumaa, kampuni ya Odebreicht ya hapa kukubali kuwekeza katika umeme wa maji kwenye maporoomoko ya maji ya Stiglers Gorge yaliyopo ndani ya Bonde la mto Rufiji, umbali wa kilomita 374 kutoka jijini Dar es Salaam.
Hatua hiyo ilifikiwa Ijumaa katika mazungumzo kati ya wawakilishi wa kampuni hiyo kubwa ya uwekezaji katika sekta hiyo duniani kufanya mazungumzo na ujumbe wa Tanzania ukiongozwa na Waziri mkuuu, Mizengo Pinda.
.....
....
"Hawa watu wana uwezo mkubwa, kwani huu hautakuwa mradi wao wa kwanza, walishakuwa na mradi na mradi kama huo nchini mwao hapa ambao unazalisha megawati 3,150 …tunaamini watafanya vizuri," alisema Ngeleja.
Source: Habari leo 9/10/2011
My take:
Je, huu ni ushahidi kuwa Watanzania wamefikia kiwango chao cha mwisho cha kufikiri (kutatua matatizo yao)!????
Je, huo mkataba unaweza kuwa tofauti na mingine tuliyoizoea?
Naomba kujuzwa, hizo Mtera, Kadatu, Kihansi, Nyumba ya Mungu nk ni zinamilikiwa na nani (wawekezaji au Serikali)?
(Kama zinamilikiwa na serikali(?) iliwezekanaje wakati huo na ishindikane sasa kulijenga hili bwawa jipya wenyewe? ...ni kutokana na bajeti iliyopita amabpoa Tanesco ilitengewa fedha kidogo zaidi ya zile za "Stimuli package". Na niliwahi kuona hapa jamvini mchangiajia alisema kama serikali ingelitenga kiasi fulani kwa miaka mitano mfululizo lingekamilika)
Nawasilisha