Wabongo Vimeo Mnaendekeza nyie Wenyewe

Mtu wa Pwani

JF-Expert Member
Dec 26, 2006
4,178
2,000
Wabongo Vimeo Mnaendekeza nyie Wenyewe.
Watanzania ni watu wanaopenda bidhaa vimeo, kuliko bidhaa zilizo na ubora kwa kuwa wanapenda vitu vya bei ya kutupa ni kweli ama si kweli.

Kwa mujibu wa Waziri wa Mipango uwezeshaji na uchumi Juma Ngasongwa alipotakiwa kujibu swali kuwa kwa nini Serikali inapokea ujumbe wa wafanyabiashara kutoka China wakati wakifahamu kuwa kuna bidhaa zao nyingi vimeo ambazo hazina ubora.

Alisema jopo la wafanyabiashara kutoka Bongo pindi wanapotua China hutafuta viwanda vidogo ambavyo
hutengeneza bidhaa ambazo hazina kiwango badala ya kudili na viwanda vikubwa ambavyo vinatengeneza bidhaa bomba.

Alisema wachina hawatakiwi kulaumiwa kabisa wanaotakiwa kulaumiwa wabongo ambao wanaendekeza vitu vya bei poa bila kuangalia madhara yake.

Bidhaa nyingi ambazo ni feki kutoka China zimekuwa zikiteketezwa na kujikuta wafanyabiashara wanaoingiza bidhaa hizo kupata hasara.


source www.darhotwire.com
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom