Wabongo tunasubiri nini?

mnyikungu

JF-Expert Member
Jul 26, 2009
1,960
2,464
Nimesoma kwa kina sana makala ya mzee mwanakijiji imenigusa mno! Achilia mbali makala hiyo yaliyoongelewa pia nayajua sana, Hakika kuwa mkimbizi ndani ya nchi yako! inauma kwa kweli, Ni mengi ambayo watanzania tunafanyiwa angalia watu wa north mara wanavyoteswa na kemikali zenye sumu, je unakumbuka skendo ya mgodi wa byamhuru "kama sijakosea jina"ambayo mheshimiwa Mrema ndiye aliyeiibua enzi zake,watu walifukiwa wazima wazima na mwekezaji walifia kwenye mashimo yaopamoja na sululu zao kama vile hawana selikali unyama gani huu?

Kwa upande wangu hakika nimechoka na kwa tasmini yangu si mimi tu, waliochoka na mienendo ya selikali kama mimi ni wengi na ni hapa linapokuja swali je kwa nini hatuchukui hatua? ama wametupa libwata? wanatufanyia michezo michafu halafu tunamwachia Mungu tutamuachia mbaka lini?uvumilivu huu UVUMILIVU GANI? Ilhali tunaumia mimi ninamashaka nao,wakula hela ya uma,wanaingia mikataba mibovu,ona mishahara yao wawapo mjengoni,magari ya kifahari wanayotumia,rasilimali zetu zote wamegawa bure halafu bado tunawatazama?

Nakumbuka Ufaransa enzi hizo watu walichukua hatua kwa kile ambacho leo wengi tunakifahamu kama mapinduzi ya wakulima,NDIO walichoshwa na kodi za kijinga zinazowaneemesha wachache huku wao wakifa njaa.sasa kwa nini sisi hatuchukui hatua? ukiniambia kwamba muda bado itakuwa tiyari lini? na tukiendelea kusubiri basi kama ni migodi tutakuta mashimo na kama ni mbuga za wanyama tutakuta mapori matupu! ndiyo,kwa maana kasi ya wizi ni kubwa,ukiongeza na misamaha wanayopewa? je kwa hali hii ya viongozi wetu kujizawadia rasilimali kama mheshimiwa Ben alivyojizawadia Kiwira tutafika kweli?

MUDA UMEFIKA WATANZANIA TUACHE WOGA,TUCHUKUE HATUA KWANI HATA WAKITUKABILI KWA MITUTU HAWATUWEZI HAWA. RISASI ZA WANAJESHI WAO ZITAISHA ILA SISI WATU (UMMA) HATUTAISHA.
 
Nakusikitikia sana kuwa umedanganyika kisi hicho. Data zilikuhamasisha hivyo ni zile za kufa mbuzi wanne?

Nashangaa sana, watu wanamwaga sumu kwenye mito ya maji ambayo inauwa na inaleta maradhi yasiyitibika lakini hayajakuhamasiha? ajabu, kufa mbuzi wanne kukuhamasishe mpaka ufikie kutangaza vita! ama kweli wajinga ndio waliwao!
 
Bora wewe mwerevu ambaye yawezekana baba ako au kaka ako ni fisadi kwa hiyo hizi nyimbo za ukombozi daima zitakukera
 
Bora wewe mwerevu ambaye yawezekana baba ako au kaka ako ni fisadi kwa hiyo hizi nyimbo za ukombozi daima zitakukera

Kaanze kukombowa wanapokufa kwa sumu inayomwagwa makusudi, kwenye mto wa maji, unaoathiri kila kitu, kuanzia binadam mpaka wanyama mpaka mimea, ya leo na ya vizazi vijavyo, ntakuona wa maana sana tena ntakuunga mkono mia kwa mia.

Leo wewe kwa kudanganywa kidogo na kutiliwa chumvi ya vifo vya mbuzi wanne, wewe unataka kuanza ukombozi wanapokufa mbuzi wanne? yaani unanishangaza sana! badala ya kukombowa binadamu wanaothirika na maradhi ya ajabu na wanaokufa, wewe unata kwenda kukombowa nini? Mbuzi?
 
MUDA UMEFIKA WATANZANIA TUACHE WOGA,TUCHUKUE HATUA KWANI HATA WAKITUKABILI KWA MITUTU HAWATUWEZI HAWA.RISASI ZA WANAJESHI WAO ZITAISHA ILA SISI WATU(UMMA) HATUTAISHA.

You lead the charge, dude! Sisi tutafuata nyuma umbali kadiri ya kilomita 2 hivi...:D
 
Kaanze kukombowa wanapokufa kwa sumu inayomwagwa makusudi, kwenye mto wa maji, unaoathiri kila kitu, kuanzia binadam mpaka wanyama mpaka mimea, ya leo na ya vizazi vijavyo, ntakuona wa maana sana tena ntakuunga mkono mia kwa mia.

Leo wewe kwa kudanganywa kidogo na kutiliwa chumvi ya vifo vya mbuzi wanne, wewe unataka kuanza ukombozi wanapokufa mbuzi wanne? yaani unanishangaza sana! badala ya kukombowa binadamu wanaothirika na maradhi ya ajabu na wanaokufa, wewe unata kwenda kukombowa nini? Mbuzi?
iwe mbuzi au watu vyote vinahaki ya kukombolewa.
 
Nimesoma kwa kina sana nakala ya mzee mwanakijiji imenigusa mno! achilia mbali nakala hiyo yaliyoongelewa pia nayajua sana,Hakika kuwa mkimbizi ndani ya nchi yako! inauma kwa kweli,Ni mengi ambayo watanzania tunafanyiwa angalia watu wa north mara wanavyoteswa na kemikali zenye sumu, je unakumbuka skendo ya mgodi wa byamhuru "kama sijakosea jina"ambayo mheshimiwa Mrema ndiye aliyeiibua enzi zake,watu walifukiwa wazima wazima na mwekezaji walifia kwenye mashimo yaopamoja na sululu zao kama vile hawana selikali unyama gani huu?
Kwa upande wangu hakika nimechoka na kwa tasmini yangu si mimi tu, waliochoka na mienendo ya selikali kama mimi ni wengi na ni hapa linapokuja swali je kwa nini hatuchukui hatua? ama wametupa libwata? wanatufanyia michezo michafu halafu tunamwachia Mungu tutamuachia mbaka lini?uvumilivu huu UVUMILIVU GANI?ilhali tunaumia mimi ninamashaka nao,wakula hela ya uma,wanaingia mikataba mibovu,ona mishahara yao wawapo mjengoni,magari ya kifahari wanayotumia,rasilimali zetu zote wamegawa bure halafu bado tunawatazama?
Nakumbuka Ufaransa enzi hizo watu walichukua hatua kwa kile ambacho leo wengi tunakifahamu kama mapinduzi ya wakulima,NDIO walichoshwa na kodi za kijinga zinazowaneemesha wachache huku wao wakifa njaa.sasa kwa nini sisi hatuchukui hatua? ukiniambia kwamba muda bado itakuwa tiyari lini? na tukiendelea kusubiri basi kama ni migodi tutakuta mashimo na kama ni mbuga za wanyama tutakuta mapori matupu! ndiyo,kwa maana kasi ya wizi ni kubwa,ukiongeza na misamaha wanayopewa? je kwa hali hii ya viongozi wetu kujizawadia rasilimali kama mheshimiwa beni alivyojizawadia kiwira tutafika kweli?
MUDA UMEFIKA WATANZANIA TUACHE WOGA,TUCHUKUE HATUA KWANI HATA WAKITUKABILI KWA MITUTU HAWATUWEZI HAWA.RISASI ZA WANAJESHI WAO ZITAISHA ILA SISI WATU(UMMA) HATUTAISHA.

point nzuri mheshimiwa Mnyikungu, ila hatua zipo za aina nyingi, hebu weka bayana basi kama una wazo au suggestion ya hatua yoyote ile halafu tuone tutajipanga vipi kuangalia na saizi ya miguu yetu..
 
Wengi humu ndani tupo lakini hatutaki active politics tunabaki tukiwa na dominant politics

Hapa sio mambo ya active politics or dominant.....kinachotakiwa hapa mtu unaleta habari unaichambua then wewe kama wewe unatoa angalau suggestion nini kifanyike na kwa njia zipi au kama huna suggestion omba watu wachangie nn kifanyike sio kulalama tuu ndo maana watu wanabaki kukoment hiki au kile.. haitoshi mtu kusema kua sasa twende vitani wakati hata strategies za vita huna so tutaishia kufa wote....
 
Back
Top Bottom