CharmingLady
JF-Expert Member
- Apr 16, 2012
- 18,250
- 12,868
Morning pipoz!!!!!
Nilipoanza kazi kampuni A hakuna aliyeshangaa zaidi ya kunipa hongera... Kampuni nzuri yenye hadhi yake, ila siku nilipoacha na kuhamia Kampuni B kila mtu aliniona kama vile sikutumia akili ya ziada katika kufanya maamuzi..Wengine ooh "umeacha kazi kampuni ile, hutopata kampuni nzuri kama" uzuri na ubaya wa kampuni yangu umeujuaje wakati hujawahi kufanya kazi pale??
Wengine "yan umeacha kazi kampuni nzuri vile ukaenda kwenye kikampuni cha ajabu ajabu hata ofisi yao haieleweki kama ni ofisi ama store" Je uzuri wa ofisi ndiyo kulipwa mshahara mzuri????
Wengine "ingelikuwa mimi ndio wewe hakika nisingefikiria kuacha kazi pale, kwanza ofisi nzuri, full kiyoyozi bla blah nyiiingi" hakumbuki kwamba SIRI YA MTUNGI AIJUAE KATA na KITANDA USOCHOKILALIA HUJUI KUNGUNI WAKE