chandarua, cherehani, chakula, choo ............kuna msemo umeenea sana siku hizi utasikia "chandarua chenye dawa" Je hii ni sahihi?mimi kwa ufahamu wangu finyu nilidhani neno sahihi ni "chandarua yenye dawa"naomba mchango kwa wataalam wa lugha adhimu ya kiswahili..
kama ni hivyo tukifika kwenye chumvi tuseme chumvi changu?chandarua, cherehani, chakula, choo ............
Kama chakula kina sumu, waweza sema chakula chenye sumu si chakula yenye sumu.
Kama choo kina ufa, waweza sema choo chenye ufa si choo yenye ufa.
Kama chandarua kina dawa, waweza sema...................sio..................
Hivyo ndivyo isemavyo sarufi ya kiswahili
asante kwa maelekezo nimeanza kukupataMara nyingi kama hicho kitu kinahesabika(countable noun) ukitumia cha lazime umalizie che. Chandarua chenye dawa. Ila vitu kama chumvi ambavyo havihesabiki(uncountable noun) lazima utumie ye.. Chumvi yenye rangi nyeupe...
Nashukuru kama nimeweza kukusaidiaasante kwa maelekezo nimeanza kukupata
Hongera sana mkuuNashukuru kama nimeweza kukusaidia