Wabeba samaki Feri ni kero kubwa mabasi ya mwendokasi

kimarabucha

JF-Expert Member
Jul 29, 2017
791
621
Hakika uongozi wa mabasi ya mwendokasi wanatakiwa waangalie utaratibu mzuri wa kipakia abiria hasa wabeba samaki kituo cha Kivukoni.Wabeba samaki wamekuwa chanzo cha foleni ukataji tiketi kwani hawataki kufuata foleni iliopo.

Wabeba samaki wamekuwa wanatumia nguvu kubwa kuingia kwenye mabasi huku wakiwasukumua kina mama wagonjwa na watoto na pia mizigo inajaa kwenye mabasi hata kuleta usumbufu kwa abiria wengine.

Mwisho ni kelele na kusababisha usumbufu kwa abiria wengine kusikia matangazo yatolewayo ndani ya basi.

Ushauri kwa uongozi uangalie namna ya kuwahudumia wabeba samaki.
 
baadae mtawaomba hao mwendokasi wawawekee mamonita wa kuandika wapiga kelele kwenye basi.
 
UDART
wangefanya utaratibu wa kufanya marekebisho kwenye huu usafiri

kwanza hao wauza samaki wangepewa basi lao ambalo linakua linapatikana asubuhi mchana na jioni sio kwa shombo hiyo

pili wanafunzi pia wangepangiwa mabasi yao asubuhi na jioni unakuta katoto kamebanwa na mipaja ya watu wazima kanahemea juu juu tu mpaka huruma

ila UDART Ni usafiri wa hovyo kabisa sio kwa kubanana kule na kusongamana hakuna ustaarabu

unatoka nyumbani umenyoosha nguo zako saafi lakini ukifika posta inakua kama imetafunwa na mbuzi halafu unanukia harufu mbalimbali
 
Kiukweli UDART wanapaswa walitazame hilo, hawa Jamaa wanapaswa wawe na Magari yao kwakuwa Ustarabu kwao ni Changamoto, Pamoja na Mizigo yao kuwa kero hata wenyewe pia wamekuwa kero unakuta Mtu amelala bahaharin akitoka asubuh mbio anawah Mwendokasi hata kuoga hajaoga ikiwa pale Ferry kuna Mabafu kwa ajili yao, ss humo kwenye Gari ni full ni kulalia Wenzake kwa Usingizi hadi unajuta kupanda gari lenyewe!!!
 
Jamani msiwachukie hao wabeba samaki,Udart ndo wakulaumiwa kwa kuweka mabasi machache barabarani
 
umenena vema mtoa mada....... watengewe gari lao ili wawe wanatoleana mishombo wenyewe kwa wenyewe, mtu unakuta una mtoko wako wa nguvu afu unafika kwenye bus uapakwa shombo la samaki yaani kero tupu
 
Hakika uongozi Wa MABASI ya Mwendokasi wanatakiwa waangalie utaratibu mzuri Wa kipakia abiria hasa wabeba samaki kituo cha KIVUKONI.Wabeba samaki wamekuwa chanzo cha foleni ukataji tiketi kwani hawataki kufuata foleni iliopo. Wabeba samaki wamekuwa wanatumia nguvu kubwa kuingia kwenye MABASI huku wakiwasukumua kina mama wagonjwa na watoto na pia Mizigo inajaa kwenye MABASI hata kuleta usumbufu Kwa abiria wengine.Mwisho ni KELELE na kusababisha usumbufu Kwa abiria wengine kusikia matangazo yatolewayo ndani ya basi.Ushauri Kwa Uongozi uangalie namna ya kuwahudumia wabeba samaki.
kwani mabasi hayo si ya watanzania wote au ulutaka wapande kirikuu kurudi na kitoweo hicho pendwa huko kimara?


hao mabasi wangefanya utaratibu mwingine wangeweka hawa mabasi ya wauza samaki pekee kwa muda ule ambao hao wauza sakaki wanatoka huko feri vinginevyo wana haki kama wengine kutumia usafiri huo na
 
Hawa wauza samaki ni kero kwa mabasi yote afadhali waandaliwe utaratibu maalum.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom