Wabeba mizigo ya samaki wagombania kuingia ndani ya mabasi ya mwendo kasi

mwembemdogo

JF-Expert Member
Feb 28, 2016
2,282
1,252
Tunauomba uongozi wa mabasi ya mwendo kasi kuwaelekeza wabeba mizigo ya samaki kivukoni namna ya uingiaji ndani ya mabasi kwani wamekuwa wakigombania na kusababisha usumbufu kwa abiria wengine.Vijana hao wamekuwa hawana ustarabu kwani hats lugha zao kwa abiria wenzao zinakera.

Ni vema uongozi ukasimamia.
 
Tunauomba uongozi wa Mabasi ya Mwendo kasi kuwaelekeza wabeba Mizigo ya Samaki kivukoni namna ya uingiaji ndani ya mabasi kwani wamekuwa wakigombania Na kusababisha usumbufu Kwa abiria wengine.Vijana hao wamekuwa hawana ustarabu kwani hats lugha zao Kwa abiria wenzao zinakera.Ni vema uongozi ukasimamia.

Sasa unataka hao wasimamizi waingie katika " makolomero " yao wawazuie kuongea au? Watanzania bhana! Yaani leo tunapanda haya mabasi yenye Viti vya Mtoto wa Chekechea huku yakiwa tu na mkwara wa madereva wake kupiga tai na kuna redio za Stereo ndani ndiyo tunajifanya nasi ni wastaarabu na kusahau kuwa hao hao wabeba hiyo mizigo ya Samaki walikuwa si tu wakitukana bali walikuwa hata wakitua mizigo yao ya Samaki katika mibichwa yetu wakati tumeminyana ndani ya daladala na tulikuwa hatulalamiki. Tuache unafiki na ubaguzi wa aina hii. Kama kweli Wewe " ngangari " mbona hukuwaambia pale pale na umekimbilia huku ili Wahusika wakusaidie? Na una bahati ungejifanya kuwakanya pale leo ungeelea majini Dar hadi Nungwi.
 
UuuhAhaha aa.... hiyo mijineno ya wachangiaji tu mie nimejikuta naachia cheko la ekotike..... mtoa mada pole sana na yaliyokukuta na wabeba samaki, hongera pia kukutumia basi za mwendo kasi
 
Aisee! Endeleeni kuisoma namba kwa style tofauti tofauti.

Nimesikia job mates wanaoishi TEGETA huko wakilia kulipa zaidi ya buku 2 kwa siku kama nauli.
 
Sasa unataka hao wasimamizi waingie katika " makolomero " yao wawazuie kuongea au? Watanzania bhana! Yaani leo tunapanda haya mabasi yenye Viti vya Mtoto wa Chekechea huku yakiwa tu na mkwara wa madereva wake kupiga tai na kuna redio za Stereo ndani ndiyo tunajifanya nasi ni wastaarabu na kusahau kuwa hao hao wabeba hiyo mizigo ya Samaki walikuwa si tu wakitukana bali walikuwa hata wakitua mizigo yao ya Samaki katika mibichwa yetu wakati tumeminyana ndani ya daladala na tulikuwa hatulalamiki. Tuache unafiki na ubaguzi wa aina hii. Kama kweli Wewe " ngangari " mbona hukuwaambia pale pale na umekimbilia huku ili Wahusika wakusaidie? Na una bahati ungejifanya kuwakanya pale leo ungeelea majini Dar hadi Nungwi.
Unajua kuandika lakini naona kwenye ustaarabu na kufuata utaratibu bado kidogo
 
UuuhAhaha aa.... hiyo mijineno ya wachangiaji tu mie nimejikuta naachia cheko la ekotike..... mtoa mada pole sana na yaliyokukuta na wabeba samaki, hongera pia kukutumia basi za mwendo kasi
humu ndani ni shida aisee, kuna yule dogo aliwekaga picha yake sijui kama alirudi tena
 
Tunauomba uongozi wa mabasi ya mwendo kasi kuwaelekeza wabeba mizigo ya samaki kivukoni namna ya uingiaji ndani ya mabasi kwani wamekuwa wakigombania na kusababisha usumbufu kwa abiria wengine.Vijana hao wamekuwa hawana ustarabu kwani hats lugha zao kwa abiria wenzao zinakera.

Ni vema uongozi ukasimamia.
kucheka bule?
 
UuuhAhaha aa.... hiyo mijineno ya wachangiaji tu mie nimejikuta naachia cheko la ekotike..... mtoa mada pole sana na yaliyokukuta na wabeba samaki, hongera pia kukutumia basi za mwendo kasi
Ngoja NA mm nikusaidie kuvunja mbavu
 
Unajua kuandika lakini naona kwenye ustaarabu na kufuata utaratibu bado kidogo

Siwezi kumfurahisha kila Mtu humu na ningeshangaa pia kusikia kama Watu wote mnapendezwa na uandishi wangu. Kama tu Yesu Kristo amekufa kwa ajili yetu Wakristo ili atukomboe kutoka dhambini lakini leo hii hii sisi Binadamu tunamdhihaki na kudharau maagizo yake itakuwa Mimi? Mungu tu anayetupa jeuri hii yote japo katuumba mwenyewe lakini kuna baadhi wasioridhika na Kazi yake. Halafu hata hivyo neno " ustaarabu " lina dhana pana mno hivyo kwakuwa Wewe umelitaja naomba unidadavulie vizuri kindaki ndaki ili nilielewe zaidi.
 
Mkuu niliona kama hujapendezwa na mleta mada ambaye hakupenda watu kutokufuata utaratibu wakati wa kuingia kwenye basi!

Mkuu wewe ni mkristo na ikitokea ukaalikwa msikitini utaingia na viatu?
 
Back
Top Bottom