Wabara wanaoishi Zanzibar kupewa vitambulisho vya wageni Zanzibar

" kama kudai mamlaka yetu kamili yaliyoporwa ni ubinafsi, haya tuiteni mutakavyo. who cares?! al muradi yetu yanatuendea kama tulivyopanga. hao waZanzibari waliopo huko mnaweza kuwataka nao wachukue vitambulisho pale tu mtakapokuwa na Tanganyika yenu. nyinyi kazi kusema tu. rejesheni Tanganyika yenu kwanza ndio muwe na midomo ya kusema ala! otherwise ....ZANZIBAR ni yetu waZanzibari na hiyo Tanzania ni yetu sote. Kila mZanzibari ni mTanzania lakini si kila mTanzania ni mZanzibari... (samahanini waZenji wenzangu najua wengine mnachefukwa mkiitwa waTanzania, ila hadi sasa hiyo ndio reality!"

Kwa taarifa yako,

Navyowafahamu wazanzibar ni zaidi ya unavyojua. Shida yenu kubwa ni mnavyodanganywa na wapemba na pesa kuwa mkiwa na independent zanzibar basi ndio mtafanikiwa kumbe wenzenu wanataka kufanya wanayoyataka but hilo sio la muhimu. Cha muhimu hapa bora muungano uvunjikie mbali mwende zenu. Hamna lolote zaidi ya kukosa shukrani na bataani zisizo na maana. Ni vema mkajitenga mkaenda huko mtakaporudi mtajua kuwa heshima. Nadhani katiba ijayo iwe na serikali ya Tanganyika na tuvunjilie mbali muungano tuone jeuri yenu mtaitoa wapi. Wenyewe kwa wenyewe mnabaguana. Mara huyo mdonge, yule wa dole, mara huyo wa kaskazini yule wa kusini, mara wewe mwarabu yule mnyamwezi. Mnabaguana kisawa sawa ni vema ukavunjwa muungano halafu tuyaone hayo mliokuwa mnatishia nyau. You are racists wazanzibar hasa wapemba.
 
Ila na sisi wabara ni wajinga kabisa.

Yaani tunaruhusu watu wachache hivyo watupelekeshe hivi?

Kwa kweli tunastahili....

afadhali wewe umeliona hilo kuna wenzio vipofu kabisa tena wameweka pamba za masikia jambo hili ndilo linalo nikumbusha watanganyika na CCM wamekuwa wakilazimishwa kuamini kuwa CCM ndio inayowapa uhai wa kiroho na pia ndio inayowapeleka makaburini leo Mmungu amewafunguwa macho maelfu kwa mamilioni ya watanganyika na kuliona hilo kumbe si la ukweli na wameanza kungana na ndugu zao wa chadema kuleta mabadiliko katika Nchi yao kinacho au naweza kusema chakusikitisha wamechukuwa miaka mingi kuelimika na hilo ,lakini basi pia najikumbusha “Don't cry because it's over, smile because it happened.”
 
Na Wazanzibari Wanaoishi BARA watapewa VITAMBULISHO Vya WAGENI wanaoishi Tanganyika?

Mimi siwalaumu Wazanzibari, maana wanayafanya haya kwa mujibu wa sheria ya serikali ya Mapinduzi Zanzibar. Sasa wewe hiyo serikali ya Tanganyika ipo wapi? Kuna sheria yoyote inayoelezea kuhusu hili? Naona sasa Watanganyika ndiyo wataamka kutoka usingizini.
 
" nakusahihisha kidogo sijui umekosea ama kwa makusudi .... ni kwamba "kila mZanzibari ni mTanzania ila si kila mTanania ni mZanzibari, hiyo ndio reality, japo kuna waZanzibari wengi tu hawautaki uTanzania na waTanzania wengi tu wanajiita waZanzibari ....solution pigania Tanganyika yako urudishe utaifa wako"
Niwie radhi ndugu yangu ni typing error tu
Namimi nakusahihisha kidogo sijui umekosea ama makusudi kulipa kisasi?...... ni kwamba "kila mZanzibari ni mTanzania ila si kila mTanzania ni mZanzibari"
Unaweza kunifafanulia vizuri hapo kwenye green? kwasababu waZanzibari wote ni wa Tanzania
 
Kwani ule uandikishaji wa vitambulisho vya taifa upo hadi znz ? Je Na waznz watakuwa wanatembea na IDs Mbili kwa wakati mmoja hebu niambieni hapa.....

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Nguruvi3

Nafikiri mtu ambaye angejibu vizuri na kwa upana swali hili ni Ndugu Lula wa Ndali.

Mimi kwa upande wangu naona yote, hayo 11 na hayo 21 yanawaletea matatizo, wamejaribu kupiga kelele sana na bado wanasema waachiwe wapumue lakini serikali za CCM zimeweka pamba masikioni.

Au hujawasikia wakisema wanataka sovereignty ya Zanzibar irudi kama zamani na kiti chao UN?

Mkuu Nguruvi3 hili nafikiri unalijua, kuna nchi ndogo ndogo nyingi duniani, tena za visiwa na zinaheshimika kama nchi huru. Sychelles, Cape Verde, Mauritius, Sao Tome hapa Afrika.

Kama kuna kiongozi makini katika serikali inampasa kufanya maamuzi magumu, kuiacha Zanzibar ijitawale yenyewe.
Kuendelea kuikumbatia ni kuchelewesha tatizo tu.

Kama ni ukaribu, basi Lesotho na Swaziland zingekuwa sehemu ya Afrika Kusini. Hizo nchi mbili zimezingirwa kimipaka na South Afrika. Lakini hakuna cha muungano wala nini, ujirani mwema tu.

Kwa nini Tanganyika na watanganyika tunapenda kukumbatia matatizo na kufanya usanii?

Lula wa Ndali alisema hivi:
Kwa yeyote anayefuatilia historia ya nchi yetu ni rahisi kuona kuwa zile zinazoitwa "kero za Muungano" kimsingi ni matokeo ya mfumo mbovu ambao tuliubuni.

Bahati mbaya mfumo huu mbovu umekuwa mbovu zaidi baada ya kuacha makubaliano ya awali ya Muungano na matokeo yake kuongeza vitu vingine ambavyo vimekuwa ni sababu ya kuleta matatizo mengi.
Kero hizi za Muungano zimetokana na mfumo wenyewe ulivyo sasa hivi.
Raia Mwema - Ni serikali moja, taifa moja au utengano
Nonda, huoni unajichanganya mufti. Hapo awali umesema yote 21 na 11 ni kero (nimepigia mstari) halafu unasema tumeacha mambo ya makubaliano.(nyekundu) wakati huo huo unasema mfumo mbovu.

Sasa kama ni mfumo mbovu, je ulikuwaje mzuri wa makubaliano ya awali? kama hukubali yote 32 kwanini udhani kuongeza 21 ni tatizo. Lakini hujajibu hoja ya msingi, je, katika hayo 21 yaliyoongezeka ni yapi ambayo ni kero?
Mimi nitakutajia moja, elimu ya juu haimo katika 11 ya awali. Leo kuna nafasi za upendeleo kuingia vyuo vya elimu ya juu na wakati huo huo upendeleo wa Wazanzibar kupewa mikopo 100%

Hivi huoni kuwa mtoto wa Tanganyika ananyng'anywa haki yake na kupewa raia wa kigeni?
Kama ZNZ inataka ijitawale ni vipi ikubali hilo ikiwa ni pamoja na mabilioni ya bajeti yasiyo na sababu(makamu wa rais bilioni 32), umeme wa bure n.k. Utawezaje kujitawala wakati huwezi 'kujitawala'?

Kuhusu Tanganyika kuwashilikilia, ah hili si kweli. Si znz wana bendera, mahakama kuu, wimbo wa taifa, BLW, Baraza la mapinduzi, Rais na makamu wawili. Unataka kusema vyote hivyo ni sanamu?
Ili ZNZ iwe huru wanapaswa kuomba passport zao! hili hawataki sasa uhuru utatoka wapi wakati umejibanza chumbani kwa mtu?

Maamuzi magumu wanatakiwa wafanye wznz, Muha, Mhaya , Mchaga, mngoni na mfipa wanatatizo gani znz wakiondoka leo. Nani atajua kuwa wameondoka. Wenye kutakiwa kufanya maamuzi magumu ni raia 350,000 wa znz wanaotakiwa waondoke bara.
 
Nonda, huoni unajichanganya mufti. Hapo awali umesema yote 21 na 11 ni kero (nimepigia mstari) halafu unasema tumeacha mambo ya makubaliano.(nyekundu) wakati huo huo unasema mfumo mbovu.

Sasa kama ni mfumo mbovu, je ulikuwaje mzuri wa makubaliano ya awali? kama hukubali yote 32 kwanini udhani kuongeza 21 ni tatizo. Lakini hujajibu hoja ya msingi, je, katika hayo 21 yaliyoongezeka ni yapi ambayo ni kero?
Mimi nitakutajia moja, elimu ya juu haimo katika 11 ya awali. Leo kuna nafasi za upendeleo kuingia vyuo vya elimu ya juu na wakati huo huo upendeleo wa Wazanzibar kupewa mikopo 100%

Hivi huoni kuwa mtoto wa Tanganyika ananyng'anywa haki yake na kupewa raia wa kigeni?
Kama ZNZ inataka ijitawale ni vipi ikubali hilo ikiwa ni pamoja na mabilioni ya bajeti yasiyo na sababu(makamu wa rais bilioni 32), umeme wa bure n.k. Utawezaje kujitawala wakati huwezi 'kujitawala'?

Kuhusu Tanganyika kuwashilikilia, ah hili si kweli. Si znz wana bendera, mahakama kuu, wimbo wa taifa, BLW, Baraza la mapinduzi, Rais na makamu wawili. Unataka kusema vyote hivyo ni sanamu?
Ili ZNZ iwe huru wanapaswa kuomba passport zao! hili hawataki sasa uhuru utatoka wapi wakati umejibanza chumbani kwa mtu?

Maamuzi magumu wanatakiwa wafanye wznz, Muha, Mhaya , Mchaga, mngoni na mfipa wanatatizo gani znz wakiondoka leo. Nani atajua kuwa wameondoka. Wenye kutakiwa kufanya maamuzi magumu ni raia 350,000 wa znz wanaotakiwa waondoke bara.

Nguruvi3

Pitia ule mchango ambao umechukua maneno ya Lula na kuonesha ni ya kwangu. Mchanganyo na mchanganyiko unaanzia hapo.
Umeuliza mambo 21 tu.
Mimi kwa maoni yangu Tanganyika haikupasa kuungana na Zanzibar katika Muungano wa kisanii.
Sio siri tena kuwa Muungano ulilazimishwa na mataifa ya US na UK. Hapo ndipo nnaposema mimi kuwa si mambo 11 au 21. Yote hayakupasa kuwepo. Ni kuwa Hakukuwa na haja ya Muungano wa kisanii.
Kumbuka Tanganyika, Uganda, Kenya na Zanzibar walitaka kuunda shirikisho la Afrika Mashariki.


Umejaribu kunilisha maneno ya Lula. Mimi nakubaliana na Lula kuwa Mfumo alioubuni Mwalimu ndio unaoleta tabu yote hii ya Muungano. Lakini ugumu uliongezeka kwa kuongeza na mambo mengine baada ya yale ya awali.

Ni kusema kuwa kama yangebaki 11 basi hili lalamiko kuwa Tanganyika inabeba/inamwaga hela kwa elimu ya juu ya wazanzibari lisingekuwepo. Pia madaraka ya mambo 21amabyo yaliyoengezwa katika muungano yangebaki kwa Zanzibar kwa hiyo, hizi kelele zinazopigwa kuwa wanabanwa zisingekuwepo katika ukubwa na upeo wa sasa.

Pia nitarudia kuuliza nchi hizo za visiwa ndogo ndogo, Mauritius, Sychelles,Cape Verde zinalipiwa na nani kuendesha mambo yao?
Tofauti ya hizo na Zanzibar ni kuwa hizo tatu ni sovereign nations, wakati Zanzibar inasemwa ni nchi ndani ya Tanzania lakini si sovereign entity, hata kwa yale ambayo si mambo ya muungano!
Mfumo mbovu wa muungano hautoi nafasi kwa Zanzibar kujiwakilisha yenyewe hata kwa mambo ambayo si ya Muungano.
Hapa unaona ni jinsi gani mfumo mbovu unavyozalisha malalamiko. Serikali ya Muungano inayatoa wapi mamlaka ya kuiwakilisha Zanzibar kwa mambo ambayo si ya muungano?

Kama tunapendelea kulea tatizo na kulikuza basi matokeo yake ni haya ya kuwakosesha watoto watanganyika elimu ya juu ili kufidia sehemu ya sovereignty ambayo inaifanya Zanzibar iwe nchi inayolelewa ndani ya "usanii" aka mfumo mbovu wa muungano.

Tanganyika itapata hasara ipi kwa kuiachia Zanzibar irudi kuwa nchi huru(sovereign nation)?

Mimi naona Tanganyika itaweza kutumia zile bilioni 32 za wizara ya Bilal na hizo za elimu ya juu kwa wazanzibari na hivyo kuimarisha miondombinu ya mikoa ya Kusini na kuwa na fedha za kutosha za kutoa mikopo ya masomo ya juu kwa watoto wa Tanganyika. Lakini faida zaidi ni kupata muda mzuri zaidi kushughulikia matatizo ya watu 40 milioni badala ya "kero za muungano" aka mfumo mbovu wa muungano.
 
Nonda, naona umegoma kukubali kuwa ZNZ ndiyo inauwezo wa kuondoka na kwambahaishikiliwi.
1. Kama ZNZ imechoshwa na muungano, kwanini watake mkataba uwe wa mambo 11, pungufu au zaidi?
2. Kwanini itake serikali 3 na ili hali inataka soverenity.Huwezi kuwa na mkataba, serikali 3 na bado ukawa na total soverenity. Kwakweli huko ni kukosa busara kwa viongozi akina Maalim Seif na washirazi.

3. Zanzibar inakosa nini hadi idai inashikiliwa? Kama mnakubali kulipiwa jeshi, mambo ya ndani n.k na hakuna anayelalamika hata siku moja kwanini muone mnashikiliwa? Huwezi kukubali kupokea kwa mkono mmoja na kukataa kwa mkono mwingine.

4. Kwavile Maalim amekwenda kudai kiti UN, kwanini wznz msimuunge mkono kwa kudai Passport?
Nani ameshikilia Passport ninyi au Tanganyika.

5. Kwa vile mliweza kufanya mabadiliko ya katiba, nini kinawashinda kufanya kura ya maoni isiyohitaji Tanganyika na kuamua hatima ya nchi yenu?

6. Katika zoezi linaloendelea la katiba mpya kwanini wznz hawajitokezi kusema muungano basi, na badala yake wanataka serikali 3 au mkataba?

7. Anayewashikilia wzn 350,000 bara ni nani? Lini walikatazwa kupanda meli na kurejea nchi ya ahadi?

8. Kuhusu visiwa vingine hili naona umesahau baadhi kama Comoro, Haiti, Vanuata, Fiji, st Lucia na Madagascar

Kwanini msiunge mkono LET ZNZ GO! mumebaki mkizunguka katika mkataba na serikali 3.
 
Ni mpaka hapo tutakapoitoa CCM ndipo mazingaumbwe haya yatakoma... Cha Ajabu waznz ndio wapigakura wakubwa wa CCM .
Mwisho huu umekaribia...
 
Kwa kweli muungano wa Tanganyika na Zanzibar umejaa Kero. Nyerere na karume wangemaliza kuungana kwa kila kitu yasingekuwepo haya malumbano ya leo.

Pia Serikali ya Zanzibar pamoja na Baraza la wawakilishi hawataki muungano kupitia matendo yao.

Thanks
 
Huo ndo mwanzo wa Zanzibar kujitenga na Tanzania Bara:
kama wa-Zanzibari wanataka hivyo Muungano utakua hauna maana tena.

Sasa kili siku si mnasema let znz go, ndo hivi sasa inakwenda na wala musilete habar ya katiba ya muungano Zanzibar haitambuliki
 
Back
Top Bottom