Wabara wanaoishi Zanzibar kupewa vitambulisho vya wageni Zanzibar

Bahati mbaya mfumo huu mbovu umekuwa mbovu zaidi baada ya kuacha makubaliano ya awali ya Muungano na matokeo yake kuongeza vitu vingine ambavyo vimekuwa ni sababu ya kuleta matatizo mengi.
Safi sana Nonda, sasa kama tumeacha mambo 11 ya awali na sasa tunayo 32, je, katika hayo 21 yapi yanaleta matatizo na kuikera Zanzibar?
 
mtaendelea kuona mazingaumbwe hadi hawa viongozi wa kiislam watoke madarakani
 
Kuwapa wabara vitambulisho vya wageni ni sawa na kuwapa wachaga na wasukuma waishio dsm vitambulisho vya wageni na sio wakazi.

Seriously, huko tunakoelekea siko. Bora tungeshughulikia kuachana na zbar. Kinachofuata hapa ni xenophobia.
 
Mbona hili halina shida; na hao Watanzania watakaoklubali kupewa vitambulisho vya uraia kama wageni Zanzibar watakuwa wapuuzi!!

Ni kweli kabisa unless wao pia wawe wanachukuliwa kama wageni Tanzania bara. Hiki wanachojaribu kufanya si halali kisheria na watakuwa wanavunja katiba ya muungano wakianza kubagua watanzania.
 
Mbona hili halina shida; na hao Watanzania watakaoklubali kupewa vitambulisho vya uraia kama wageni Zanzibar watakuwa wapuuzi!!
Huo ndo mwanzo wa Zanzibar kujitenga na Tanzania Bara:
kama wa-Zanzibari wanataka hivyo Muungano utakua hauna maana tena.
 
Jamani,twaache na nchi yao.Ila wabunge kutoka Zanzibar wajitathmini baada ya haya wanauwezo wakuingia kwenye bunge letu na kupewa posho na mshahara toka kwa walipa kodi kutoka Tanzania Bara?Wajitafakari halaf wachukue hatua.Hata wale Wazanzibar wanaoishi Tanzania Bara wajitafakari kama baada ya hili wanahaki ya kujiita waTanzania na kama wanahaki ya kuishi kama Mtanzania Bara.
 
Safi sana Nonda, sasa kama tumeacha mambo 11 ya awali na sasa tunayo 32, je, katika hayo 21 yapi yanaleta matatizo na kuikera Zanzibar?

Nguruvi3

Nafikiri mtu ambaye angejibu vizuri na kwa upana swali hili ni Ndugu Lula wa Ndali.

Mimi kwa upande wangu naona yote, hayo 11 na hayo 21 yanawaletea matatizo, wamejaribu kupiga kelele sana na bado wanasema waachiwe wapumue lakini serikali za CCM zimeweka pamba masikioni.

Au hujawasikia wakisema wanataka sovereignty ya Zanzibar irudi kama zamani na kiti chao UN?

Mkuu Nguruvi3 hili nafikiri unalijua, kuna nchi ndogo ndogo nyingi duniani, tena za visiwa na zinaheshimika kama nchi huru. Sychelles, Cape Verde, Mauritius, Sao Tome hapa Afrika.

Kama kuna kiongozi makini katika serikali inampasa kufanya maamuzi magumu, kuiacha Zanzibar ijitawale yenyewe.
Kuendelea kuikumbatia ni kuchelewesha tatizo tu.

Kama ni ukaribu, basi Lesotho na Swaziland zingekuwa sehemu ya Afrika Kusini. Hizo nchi mbili zimezingirwa kimipaka na South Afrika. Lakini hakuna cha muungano wala nini, ujirani mwema tu.

Kwa nini Tanganyika na watanganyika tunapenda kukumbatia matatizo na kufanya usanii?

Lula wa Ndali alisema hivi:
Kwa yeyote anayefuatilia historia ya nchi yetu ni rahisi kuona kuwa zile zinazoitwa "kero za Muungano" kimsingi ni matokeo ya mfumo mbovu ambao tuliubuni.

Bahati mbaya mfumo huu mbovu umekuwa mbovu zaidi baada ya kuacha makubaliano ya awali ya Muungano na matokeo yake kuongeza vitu vingine ambavyo vimekuwa ni sababu ya kuleta matatizo mengi.

Kero hizi za Muungano zimetokana na mfumo wenyewe ulivyo sasa hivi.
Raia Mwema - Ni serikali moja, taifa moja au utengano
 
Akufukuzaye hakuambii toka. Mara tunataka muungano wa mkataba, mara serikali tatu, na sasa vitambulisho vya ukaazi. Watanganyika tutaendelea kuitwa Wadanganyika hadi lini? Tumezidi kuwa kama makondoo yaliyonyeshewa na mvua. Tuamke, tuzinduke, tuikomboe Tanganyika yetu. Ndoa makanisani na misikitini zinavunjwa, sembuse muunganiko wan Tanganyika na Zanzibar? (maana huu si muungano)
Ila na sisi wabara ni wajinga kabisa.
:nono:
Yaani tunaruhusu watu wachache hivyo watupelekeshe hivi?

Kwa kweli tunastahili....
 
Huo ndo mwanzo wa Zanzibar kujitenga na Tanzania Bara:
kama wa-Zanzibari wanataka hivyo Muungano utakua hauna maana tena.

Ama kweli wanadam tuna matatizo,hilo la wao kutoa vitambulisho vya uzanzibar mnaliona kero ama la wanaotoka zanzibar kuja bara na mizigo kulipishwa hamlioni kama ni tatizo. Leo ukinunua TV ukaenda morogoro kuna chochote unacholipishwa pale mikese? Ile ni nchi nyingine acheni ajipangie taratibu zake. Hapa tatizo lipo kwetu sisi wabara kuwa Tanganyika imepotezwa. Tuirejeshe kwa kuukataa muungano kwenye maoni ya katiba mpya
 
Pamoja na mijadala mingi sana kuhusu huu muungano, ukweli bado unabaki pale pale, TATIZO LA MUUNGANO NI MFUMO WA MUUNGANO ULIOPO SASA!
 
[h=2]Wabara kupewa vitambulisho vya wageni Z’bar[/h]

























Mwinyihaji Makame(1)(1).jpg

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Ikulu) Dk. Mwinyihaji Makame Mwadini


Watanzania bara wanaoishi Zanzibar wataanza kusajiliwa na kupewa vitambulisho maalum sawa na raia wa nje ya Tanzania wanaoishi Zanzibar.

Kwa Mujibu wa muswada wa marekebisho ya sheria ya Usajili ya Mzanzibari mkaazi namba 7 ya mwaka 2005 kazi ya kuwasajili itaanza kufanyika miezi mitatu baada ya kupitishwa kwa sheria hiyo.

Muswada huo unatarajiwa kuwasilishwa katika Baraza la Wawakilishi Zanzibar (BLW) na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Ikulu) Dk. Mwinyihaji Makame Mwadini, Oktoba 10 mwaka huu.

Kifungu cha 6A (1) cha muswada kimeleza kwamba kila mkazi asiyekuwa Mzanzibari atatakiwa kujisajili katika Ofisi ya usajili wa vitambilisho vya Mzanzibari mkazi.

Muswada huo umeleza kwamba zoezi hilo pia litawagusa raia wa kigeni ambao wanaishi Zanzibar na kufanya kazi au biashara.

Kifungu cha 6A (3) kimeleza aina ya wageni wanaotakiwa kusajili kwa mujibu wa sheria hiyo wanaofanyakzi Zanzibar ama kwenye taasisi ya umma au binafsi pamoja na wanaofanyabiashara visiwani humo.

“Muajiri wa mkazi asiyekuwa Mzanzibari atatakiwa kutoa taarifa za mtu huyo kwa mkurugenzi au afisa msajili ndani ya siku 60 kuanzia ajira yake au ikiwa ameajiriwa kabla ya kuanza kutumika kwa sheria hii,” umesisitiza muswada huo.

Aidha, muswada huo umefuta kifungu cha 7 na watu wote watakaosajiliwa watatakiwa kuchukuliwa alama za vidole badala ya kidole gumba kimoja kwa mujibu wa sheria hiyo.

Akizungumza na NIPASHE Mkurugenzi wa usajili wa Vitambulisho vya Uzanzibari mkazi Mohamed Juma Ame, alisema serikali imeamua kuwasajili watu hao baada ya kubainika kuwepo watu wanaopewa vitambulisho hivyo kinyemela.

Alisema kwamba hali hiyo imekuwa ikifanyika baada ya vitambulisho hivyo kuonekana kuwa ni nyenzo muhimu katika maisha ya kila siku hasa katika upatikanaji wa huduma za jamii.

Mohamed alisema sheria hiyo pia itasadia kuwatambua watu wanaoingia na kutoka Zanzibar maeneo wanayoushi na kazi wanazofanya Zanzibar.

Hivi karibuni Baadhi ya Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wamekuwa wakilalamika kuwa vijana wengi Zanzibar wameshindwa kunufaika na ajira katika sekta ya Utalii kutokana na kazi hizo kuvamiwa na wageni kutoka nje ya Zanzibar ikiwemo Tanzania bara.




CHANZO: NIPASHE


Maoni yangu.

Huu muungano una maana gani sasa.Tanzania bara nayo ikichukua hatua ya kuwasajili wapemba waliojazana huku bara kama wagei muungano utabaki kweli ?.Ifike mahali huu muungano ufutwe kabisa tukutane na waZanzibar EAC.
 
za shein, changanya na za kikwete! ni vapour tu, mwisho wa siku!
 
Back
Top Bottom