Wabara wanaoishi Zanzibar kupewa vitambulisho vya wageni Zanzibar | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wabara wanaoishi Zanzibar kupewa vitambulisho vya wageni Zanzibar

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Sep 13, 2012.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Sep 13, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145

  Watanzania bara wanaoishi Zanzibar wataanza kusajiliwa na kupewa vitambulisho maalum sawa na raia wa nje ya Tanzania wanaoishi Zanzibar.

  Kwa Mujibu wa muswada wa marekebisho ya sheria ya Usajili ya Mzanzibari mkaazi namba 7 ya mwaka 2005 kazi ya kuwasajili itaanza kufanyika miezi mitatu baada ya kupitishwa kwa sheria hiyo.

  Muswada huo unatarajiwa kuwasilishwa katika Baraza la Wawakilishi Zanzibar (BLW) na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Ikulu) Dk. Mwinyihaji Makame Mwadini(pichani), Oktoba 10 mwaka huu.

  Kifungu cha 6A (1) cha muswada kimeleza kwamba kila mkazi asiyekuwa Mzanzibari atatakiwa kujisajili katika Ofisi ya usajili wa vitambilisho vya Mzanzibari mkazi.

  Muswada huo umeleza kwamba zoezi hilo pia litawagusa raia wa kigeni ambao wanaishi Zanzibar na kufanya kazi au biashara.

  Kifungu cha 6A (3) kimeleza aina ya wageni wanaotakiwa kusajili kwa mujibu wa sheria hiyo wanaofanyakzi Zanzibar ama kwenye taasisi ya umma au binafsi pamoja na wanaofanyabiashara visiwani humo.

  "Muajiri wa mkazi asiyekuwa Mzanzibari atatakiwa kutoa taarifa za mtu huyo kwa mkurugenzi au afisa msajili ndani ya siku 60 kuanzia ajira yake au ikiwa ameajiriwa kabla ya kuanza kutumika kwa sheria hii," umesisitiza muswada huo.

  Aidha, muswada huo umefuta kifungu cha 7 na watu wote watakaosajiliwa watatakiwa kuchukuliwa alama za vidole badala ya kidole gumba kimoja kwa mujibu wa sheria hiyo.

  Akizungumza na NIPASHE Mkurugenzi wa usajili wa Vitambulisho vya Uzanzibari mkazi Mohamed Juma Ame, alisema serikali imeamua kuwasajili watu hao baada ya kubainika kuwepo watu wanaopewa vitambulisho hivyo kinyemela.

  Alisema kwamba hali hiyo imekuwa ikifanyika baada ya vitambulisho hivyo kuonekana kuwa ni nyenzo muhimu katika maisha ya kila siku hasa katika upatikanaji wa huduma za jamii.

  Mohamed alisema sheria hiyo pia itasadia kuwatambua watu wanaoingia na kutoka Zanzibar maeneo wanayoushi na kazi wanazofanya Zanzibar.

  Hivi karibuni Baadhi ya Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wamekuwa wakilalamika kuwa vijana wengi Zanzibar wameshindwa kunufaika na ajira katika sekta ya Utalii kutokana na kazi hizo kuvamiwa na wageni kutoka nje ya Zanzibar ikiwemo Tanzania bara.

  HABARI NA MWINYI SADALLAH

  CHANZO: NIPASHE
   
 2. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #2
  Sep 13, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,361
  Likes Received: 6,380
  Trophy Points: 280
  Mbona hili halina shida; na hao Watanzania watakaoklubali kupewa vitambulisho vya uraia kama wageni Zanzibar watakuwa wapuuzi!!
   
 3. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #3
  Sep 13, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Na Wazanzibari Wanaoishi BARA watapewa VITAMBULISHO Vya WAGENI wanaoishi Tanganyika?
   
 4. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #4
  Sep 13, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Kwanini Watakuwa Wajinga na Zanzibar sio KWAO?
   
 5. N

  Nonda JF-Expert Member

  #5
  Sep 13, 2012
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 13,223
  Likes Received: 1,958
  Trophy Points: 280
  Mzee Mwanakijiji

  Tanzania ni Muungano wa nchi mbili. Bado hatutaki kuipigania Tanganyika irudi?
  Unajua China na Hong Kong ni nchi moja na sio kama Tanzania. Tanzania ni Muungano wa baadhi ya mambo baina ya Tanganyika na Zanzibar. China na Hong Kong wana taratibu tofauti za uhamiaji.

  La msingi, Tanganyika(jina la utani Tz bara/bara) iweke taratibu zake pia za uhamiaji.

  Muungano una kero? au Muungano ni kero?

  Link. The Government of the Hong Kong Special Administrative Region - Immigration Department
   
 6. O

  Ogah JF-Expert Member

  #6
  Sep 13, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 6,229
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Bara bado hatujifunzi tu, tumebakia na eti na sisi tuwape vitambulisho.............vitambulisho vipi hivyo?
   
 7. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #7
  Sep 13, 2012
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Huu sasa ni usen.ge wa hali ya juu.

  Na yeyote anayeendelea kung'ang'ania uwepo huu muungano haeleweki!
   
 8. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #8
  Sep 13, 2012
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Eti wanataka muungano wa mkataba. Sielewi ni muungano wa aina gani huo. Na yeyote atakayekubali kukaa kitako kujadilia huo mkataba haniwakilishi kabisa.
   
 9. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #9
  Sep 13, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,361
  Likes Received: 6,380
  Trophy Points: 280
  Hapana; binafsi nataka wabara walioko Zanzibar wagome kupokea vitambulisho hivyo wala kuvitumia tuone Zanzibar watafanya nini
   
 10. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #10
  Sep 13, 2012
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,548
  Likes Received: 81,990
  Trophy Points: 280
  Magamba wananufaika na Muungano hivyo watafanya lolote lile ili kuuendeleza huu usanii walioupa jina la Muungano

   
 11. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #11
  Sep 13, 2012
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Ila na sisi wabara ni wajinga kabisa.

  Yaani tunaruhusu watu wachache hivyo watupelekeshe hivi?

  Kwa kweli tunastahili....
   
 12. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #12
  Sep 13, 2012
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,548
  Likes Received: 81,990
  Trophy Points: 280
  Population yao ni 25% ya ile ya Dar lakini bado wana kibri utadhani wao ndio wako 45 million na bara tuko millioni moja na upuuzi. Wakati umefika wa kuachana na huu ujinga. Hata yule msanii wa Ikulu eti alitamka katika kukusanya maoni ya katiba mpya, maswala ya muungano yasiguswe kabisa!!!!

   
 13. Job K

  Job K JF-Expert Member

  #13
  Sep 13, 2012
  Joined: Oct 4, 2010
  Messages: 6,850
  Likes Received: 2,776
  Trophy Points: 280
  Yaani hiki kiji-nchi kinakera sana! Hivi kuna mpumb.avu gani huko anayeking'ang'ania hiki? Hebu tuwatimue na Wabunge wao wasiendelee to fart on our Bunge's chairs! Tumb...f kabisa!! Tunawaomba na sisi wenyeviti wa mitaa waanze kuwatambua wa-Zanzibar mara moja!
   
 14. Tango73

  Tango73 JF-Expert Member

  #14
  Sep 13, 2012
  Joined: Dec 14, 2008
  Messages: 1,678
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 135
  nani alileta muungano huu wa kipuuzi namna hii hapa duniani ? Yaani ni muungano wa kipuuzi sana kuwahi kutokea duniani.
   
 15. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #15
  Sep 13, 2012
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 12,221
  Likes Received: 7,342
  Trophy Points: 280
  Nonda, unajua siri ya muungano wa mkataba inaanza kujidhihiri. Wanachotaka ni wawe na vitambulisho vyao na wakati huo huo wawe na vya Tanzania ili waje huku bila wasi wasi.

  Nimesema mara nyingi Tanganyika ikirudi hakuna muungano wa mkataba au serikali 3 na hapo muungano utakuwa umekoma. Hili litatokea muda si mrefu.

  Tunaomba Zanzibar waanzishe passport zao pia. Hili la vitambulisho si kubwa kihivyo, wanachotakiwa ni kuwa na passport kama nchi huru.

  Ila timimg yao ni mbaya kwasababu usione Watanganyika wamekaa kimya, taratibu tutahoji viwango vya watahiniwa kwasababu hatujui standard ya mitihani ya Zanzibar, tutahoji ajiri na hata uwekezaji. 'ukila na kipofu usimkamate mkono'
   
 16. N

  Nonda JF-Expert Member

  #16
  Sep 13, 2012
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 13,223
  Likes Received: 1,958
  Trophy Points: 280
  Nguruvi3

  Unataka niamini kuwa CCM wameshaiacha ndoto yao ya kutoka serikali mbili kuelekea moja?
  Naona tunafanya utani na ile kampeni ya "Let Zanzibar go!"

  Kampeni sasa iwe "Restore Tanganyika", "Re-install Tanganyika!" au "Tanganyika iokoke!(born again)".

  Haya mauza uza yanayoendelea yatazalisha majanga!

  Nakumbushia hii Singapore in Malaysia - Wikipedia, the free encyclopedia

  Tanganyika na Zanzibar zinaweza kuibuka kidedea bila muungano, kama nchi jirani zenye neema.
   
 17. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #17
  Sep 13, 2012
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 12,221
  Likes Received: 7,342
  Trophy Points: 280
  LET ZNZ GO!
  Hakuna sababu ya kudai Tanganyika, suala ni kuwa hakuna mktaba wala serikali 3. Kama muungano ni serikali moja.
  Vinginevyo anayeona hapafai aondoke na hapa ni ZNZ.

  Nonda, hivi umesikia watu wangapi wa bara wakidai mkataba au serikali 3?
  Si unaona Wazanzibar wanavyo haha! Sasa Mtanganyika anahitaji kitambulisho cha nini, si wangesema wageni tu.
  Swali, passport vipi?
   
 18. ITEGAMATWI

  ITEGAMATWI JF-Expert Member

  #18
  Sep 13, 2012
  Joined: Jan 26, 2012
  Messages: 4,222
  Likes Received: 1,065
  Trophy Points: 280

  Answer:Nyerere na Karume walipokuwa kijiweni wanakunywa kahawa.
   
 19. N

  Nonda JF-Expert Member

  #19
  Sep 13, 2012
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 13,223
  Likes Received: 1,958
  Trophy Points: 280
  Katika makala moja ya Mjj au Lula wa Ndali kati ya hawa mmoja wapo alisema mfumo huu wa muungano umetuletea balaa, unatuletea balaa na utatuletea balaa.

  Kuondoka si "option", wafukuzwe. Walikaribishwa kwenye Muungano.
  Na mwalimu kwa mahesabu yake akasema hataki kuimeza Zanzibar kwa maneno, kivitendo akawa anahamisha mamlaka ya Zanzibar kinyemela au kwa mkakati wa kisiasa. Baada ya miaka 24-26 ya utawala wake kazi ya kuimeza Zanzibar ikawa haijatimia.

  Sioni kwa nini tuwalaumu wazanzibari kudai kile ambacho wanaona ni haki yao.

  Ugumu unaongezeka pale mkulu anaposema Zanzibar ni nchi ndani ya Tanzania lakini nje ipo Tanzania tu. Hapa sioni wanaharakati, wabunge au sisi wa mtandaoni tunaoitaja au kupigania haki ya Tanganyika. Sijui huu ni udhaifu au ndio ujasiri?

  Au watanganyika sote tunakubaliana na CCM na sera yao? Kutoka serikali mbili kwenda moja?
  Vipi utaifuta serikali ya Zanzibar baada ya wazanzibari kupata Mwafaka?(serikali ya umoja wa kitaifa).

  Serikali ya umoja wa kitaifa, ...Taifa ndani ya taifa!!!

  Tumelikoroga big time!!

  Nukuu "Nikitambua ukweli wa sauti tunazozisikia kutoka Zanzibar na hasa kukosekana kwa sauti thabiti zenye kutetea Mapinduzi ya Zanzibar ambayo yalizaa Muungano sina shaka yoyote kuwa hakuna namna nyingine yoyote ya kuuokoa Muungano,. isipokuwa kuuvunja kwanza ili kila mtu aende na zake...."

  Tatizo ni kuwa Tanganyika kwa kweli haikufa kabisa; ilikubali kulazwa nusu kaputi ili kuokoa uhai wa Zanzibar. Sasa Tanganyika inaamka!
  Raia Mwema - Kila la kheri Zanzibar, bye bye Muungano!

  Ni lazima tuseme ukweli na ukweli ujulikane. Yanayotokea sasa hayakupaswa kutokea kama viongozi wetu wangeonyesha uwezo wa kuyamaliza matatizo ya ‘kero’ za Muungano.

  Ndugu zangu kushindwa kutatuliwa kwa haya kumegeuza kero hizi kuwa ‘matatizo sugu’ ya Muungano. Yaani, ni matatizo yaliyoshindikana. Kwa vile yameshindikana kutatuliwa kwa muda wa miaka hii 50 wakati umefika sasa wa kukubali kushindwa na kusalimu amri kuuachilia Muungano.
  Raia Mwema - Zanzibar iachwe iende  Kwa karibu miaka 50 tumekuwa tukijaribu kutengeneza taifa lenye serikali mbili na nchi mbili. Hata hivyo, mfumo huu wa sasa umeleta matatizo makubwa (si kero) ambayo yanatokana hasa na mfumo wenyewe zaidi kuliko siasa za nchi.

  Kwa yeyote anayefuatilia historia ya nchi yetu ni rahisi kuona kuwa zile zinazoitwa “kero za Muungano” kimsingi ni matokeo ya mfumo mbovu ambao tuliubuni.

  Bahati mbaya mfumo huu mbovu umekuwa mbovu zaidi baada ya kuacha makubaliano ya awali ya Muungano na matokeo yake kuongeza vitu vingine ambavyo vimekuwa ni sababu ya kuleta matatizo mengi.

  Kero hizi za Muungano zimetokana na mfumo wenyewe ulivyo sasa hivi.
  Raia Mwema - Ni serikali moja, taifa moja au utengano
   
 20. Boflo

  Boflo JF-Expert Member

  #20
  Sep 13, 2012
  Joined: Jan 20, 2010
  Messages: 4,394
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Wa znz wanatutia vidole wabara....kisha wanatuambia nusa! nusa!, na Wabara wametulia tuli...kwa kupenda Muungano

  na kudumisha fikra za Baba wa Taifa
   
Loading...