Wabara kupewa vitambulisho vya wageni Zanzibar

Kakke

JF-Expert Member
Dec 4, 2010
1,883
1,482
Mwinyihaji%20Makame(1)(1).jpg

Watanzania bara wanaoishi Zanzibar wataanza kusajiliwa na kupewa vitambulisho maalum sawa na raia wa nje ya Tanzania wanaoishi Zanzibar.


Kwa Mujibu wa muswada wa marekebisho ya sheria ya Usajili ya Mzanzibari mkaazi namba 7 ya mwaka 2005 kazi ya kuwasajili itaanza kufanyika miezi mitatu baada ya kupitishwa kwa sheria hiyo.


Muswada huo unatarajiwa kuwasilishwa katika Baraza la Wawakilishi Zanzibar (BLW) na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Ikulu) Dk. Mwinyihaji Makame Mwadini(pichani).

Kifungu cha 6A (1) cha muswada kimeleza kwamba kila mkazi asiyekuwa Mzanzibari atatakiwa kujisajili katika Ofisi ya usajili wa vitambilisho vya Mzanzibari mkazi.

Muswada huo umeleza kwamba zoezi hilo pia litawagusa raia wa kigeni ambao wanaishi Zanzibar na kufanya kazi au biashara.

Kifungu cha 6A (3) kimeleza aina ya wageni wanaotakiwa kusajili kwa mujibu wa sheria hiyo wanaofanyakzi Zanzibar ama kwenye taasisi ya umma au binafsi pamoja na wanaofanyabiashara visiwani humo.

"Muajiri wa mkazi asiyekuwa Mzanzibari atatakiwa kutoa taarifa za mtu huyo kwa mkurugenzi au afisa msajili ndani ya siku 60 kuanzia ajira yake au ikiwa ameajiriwa kabla ya kuanza kutumika kwa sheria hii," umesisitiza muswada huo.

Aidha, muswada huo umefuta kifungu cha 7 na watu wote watakaosajiliwa watatakiwa kuchukuliwa alama za vidole badala ya kidole gumba kimoja kwa mujibu wa sheria hiyo.

Akizungumza na NIPASHE Mkurugenzi wa usajili wa Vitambulisho vya Uzanzibari mkazi Mohamed Juma Ame, alisema serikali imeamua kuwasajili watu hao baada ya kubainika kuwepo watu wanaopewa vitambulisho hivyo kinyemela.

Alisema kwamba hali hiyo imekuwa ikifanyika baada ya vitambulisho hivyo kuonekana kuwa ni nyenzo muhimu katika maisha ya kila siku hasa katika upatikanaji wa huduma za jamii.

Mohamed alisema sheria hiyo pia itasadia kuwatambua watu wanaoingia na kutoka Zanzibar maeneo wanayoushi na kazi wanazofanya Zanzibar.

Hivi karibuni Baadhi ya Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wamekuwa wakilalamika kuwa vijana wengi Zanzibar wameshindwa kunufaika na ajira katika sekta ya Utalii kutokana na kazi hizo kuvamiwa na wageni kutoka nje ya Zanzibar ikiwemo Tanzania bara.

 
Kakke

Na huku bara tuanze mpango mapema wa kuhakikisha kila mzanzibari anapewa karatasi ya kuishi huku...
 
Last edited by a moderator:
Ni kweli CCM inatuvuruga sana .Na kama kweli Watanzania watapewa vitambulisho vya aina hiyo ndani ya Zanzibar nina hakika kutazuka mgogoro mkubwa mno na hata wabunge wao kuja Bara tutaka kujua zaidi .Zanzibar wana choko choko sana sijui kwa nini .
 
Majinga hayo, wacha yaanze ubaguzi kwa watanganyika yaone matokeo yake. Si wanamuona Ba Mwanaisha dhaifu!!, haya ngoja tuone kama ataongeza kipindi.
 
Operesheni kimbunga si imeendeshwa juzijuzi tu hapa, mbona tunakuwa wasahaulifu kiasi hiki.
 




Mwinyihaji%20Makame(1)(1).jpg
Watanzania bara wanaoishi Zanzibar wataanza kusajiliwa na kupewa vitambulisho maalum sawa na raia wa nje ya Tanzania wanaoishi Zanzibar.






Kwa Mujibu wa muswada wa marekebisho ya sheria ya Usajili ya Mzanzibari mkaazi namba 7 ya mwaka 2005 kazi ya kuwasajili itaanza kufanyika miezi mitatu baada ya kupitishwa kwa sheria hiyo.



Muswada huo unatarajiwa kuwasilishwa katika Baraza la Wawakilishi Zanzibar (BLW) na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Ikulu) Dk. Mwinyihaji Makame Mwadini(pichani).​



Kifungu cha 6A (1) cha muswada kimeleza kwamba kila mkazi asiyekuwa Mzanzibari atatakiwa kujisajili katika Ofisi ya usajili wa vitambilisho vya Mzanzibari mkazi.​



Muswada huo umeleza kwamba zoezi hilo pia litawagusa raia wa kigeni ambao wanaishi Zanzibar na kufanya kazi au biashara.​



Kifungu cha 6A (3) kimeleza aina ya wageni wanaotakiwa kusajili kwa mujibu wa sheria hiyo wanaofanyakzi Zanzibar ama kwenye taasisi ya umma au binafsi pamoja na wanaofanyabiashara visiwani humo.​



“Muajiri wa mkazi asiyekuwa Mzanzibari atatakiwa kutoa taarifa za mtu huyo kwa mkurugenzi au afisa msajili ndani ya siku 60 kuanzia ajira yake au ikiwa ameajiriwa kabla ya kuanza kutumika kwa sheria hii,” umesisitiza muswada huo.​



Aidha, muswada huo umefuta kifungu cha 7 na watu wote watakaosajiliwa watatakiwa kuchukuliwa alama za vidole badala ya kidole gumba kimoja kwa mujibu wa sheria hiyo.​



Akizungumza na NIPASHE Mkurugenzi wa usajili wa Vitambulisho vya Uzanzibari mkazi Mohamed Juma Ame, alisema serikali imeamua kuwasajili watu hao baada ya kubainika kuwepo watu wanaopewa vitambulisho hivyo kinyemela.​



Alisema kwamba hali hiyo imekuwa ikifanyika baada ya vitambulisho hivyo kuonekana kuwa ni nyenzo muhimu katika maisha ya kila siku hasa katika upatikanaji wa huduma za jamii.​



Mohamed alisema sheria hiyo pia itasadia kuwatambua watu wanaoingia na kutoka Zanzibar maeneo wanayoushi na kazi wanazofanya Zanzibar.​



Hivi karibuni Baadhi ya Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wamekuwa wakilalamika kuwa vijana wengi Zanzibar wameshindwa kunufaika na ajira katika sekta ya Utalii kutokana na kazi hizo kuvamiwa na wageni kutoka nje ya Zanzibar ikiwemo Tanzania bara.​






Suala la uraia ni miongoni mwa mambo ya Muungano kwa vile hakuna mzanzibar wala Mtanganyika bali kuna Mtanzania. Jambo hili linapojitokeza litaleta shida sana hasa kama mamlaka zinazohusika zikiendelea kukaa kimya juu ya suala hili. Kitendo cha kuruhusu Zanzibar kuwa na katiba yake lilikuwa ni kosa kubwa sana ambalo Mkapa anapaswa kujutia kwani ameongeza mgogoro kuwa mkubwa. Lakini pia Kikwete anapokaa kimya juu ya masuala kama haya anaendeleza msuguano wa jambo hili.

Mungu ibariki Tanzania
 
Kama kuna mtu wa bara atachukua kitambulisho kama vile yeye ni raia wa kigeni itabidi anyang'anywe uraia wa Tanzania.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom