Mawembasa1979
JF-Expert Member
- Feb 26, 2015
- 2,152
- 2,500
Wababe wa Simba kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho leo tarehe 24/10/2018 wamechapwa magoli manne bila majibu. Hadi mapumziko wenyeji AS Vita walikuwa wanaongoza kwa mabao 2-0, mabao yaliyofungwa na E. Ngoyi dakika 6 na 39. Kipindi cha pili Al Masry walijitahidi kuweza kusawazisha mabao hayo. Hata hivyo walijikuta wakifungwa bao la tatu na mshambuliaji hatari aitwaye J. Makusu. Kuingia kwa bao hilo kulisababisha Al Masry kutaka kugomea mchezo kwa kuweka mpira kwapani kama ambavyo Simba wamewahi kugomea mechi na Yanga baada ya mapumziko. Wachezaji wa Al Masry walidai mfungaji alikuwa ameotea kabla ya kufunga bao hilo.
Hata hivyo, Al Masry walikubali kuendelea na mchezo na kufungwa bao la nne dakika za nyongeza na mfungaji akiwa ni M. Batezadio.
Katika mchezo huo Al Masry walionesha kiwango kibovu cha uchezaji. Kiasi kwamba haieleweki kwa nini waliweza kuwatoa Simba kwenye michuano hiyo.