Wababe wa kivita Urusi inapanga kujenga kambi ya Jeshi lake Afrika

MakinikiA

JF-Expert Member
Jun 7, 2017
5,011
6,542
Urusi kuanzisha kambi ya jeshi Sudan katika pwani ya Bahari Nyekundi.

Rais wa Urusi Vladimir Putin ameidhinisha kuendelezwa kwa makubaliano na Sudan ya kuanzishwa kwa kambi ya jeshi katika pwani ya Bahari Nyekundi.

Urusi inapanga kujenga kituo cha usafirishaji na ukarabati kwa jeshi lake la majini ambacho kitakuwa na wafanyakazi wasiozidi 300.
Rasimu ya makubaliano ya kambi hiyo itakuwa viungani mwa kaskazini mwa Bandari ya Sudan.

Wachambuzi wanasema, Urusi imeongeza shughuli zake Afrika katika miaka ya hivi karibuni hatua inayochukuliwa kama njia moja ya kupunguza ushawishi wa China na Marekani barani humo.​

1605604699568.png
 
Wanaona wachina na wamarekani wamekuja sana Afrika, sasa wanataka kujileta pia. Hii Afrika yaani ikioneshwa pesa tu, mshajisahau. Watakuja pigana huku Afrika wale jamaa, wapaharibu, warudi kwao.
 
Wanaona wachina na wamarekani wamekuja sana Afrika, sasa wanataka kujileta pia. Hii Afrika yaani ikioneshwa pesa tu, mshajisahau. Watakuja pigana huku Afrika wale jamaa, wapaharibu, warudi kwao.
Ndio kitu nawaza,wagombanie kwao waje wapiganie africa.
 
Back
Top Bottom