Wababe Italy wameshindwa kufuzu kombe la dunia 2018

donniebrasco

JF-Expert Member
Aug 8, 2013
887
770
Timu ya mpira wa miguu ya ITALY ambao wamewahi kuchukua kombe la dunia mara nne (wakilingana na GERMANY na wakiwa nyuma ya BRAZIL ambao walichukua mara tano) wameshindwa kufuzu kushiriki kombe la dunia la mpira wa miguu litakalofanyika mwakani nchini URUSI,

Wametoka sare ya bila bila na SWEDEN na mechi ya kwanza SWEDEN alishinda moja bila.

Kwa hivyo SWEDEN kapita ITALY kabaki

======

Mabingwa mara nne wa kombe la dunia Italia, wameshindwa kufuzu fainali za mwa 2018 nchini Urusi ikiwa ni mara ya kwanza tokea mwaka 1958 baada ya kutoka suluhu ya bila kufungana na Sweden.

Hii ina maana kwamba Azzurri watayakosa mashindano hayo kwa mara ya pili tokea kuanzishwa, mara ya kwanza ilikua mwaka 1930.


Kiungo Jakob Johansson wa Sweden aliyefunga goli katika mzunguko wa kwanza alikuwa katika kiwango bora na kuwadhibiti vyema Italia katika uwanja wa San Siro.

Wengi walitaraji Italia kushinda mchezo huu kwa sababu lukuki ikiwemo historia sambamba na kucheza nyumbani.

Italia walitawala mchezo kwa asilimia 75 na kupiga mashuti 27 lakini bahati haikuwa upande wao.

Nusura mshambuliaji Stephan El Shaarawy aandike bao lakini juhudi za mlinda mlango wa Sweden Robin Olsen zilizima ndoto yake.

Matokeo haya yanaifanya Sweden kushiriki mashindano haya tokea mwaka 2006 waliposhiriki kwa mara ya mwisho.

- BBC
 
Cha ajbu kipi, atleast wao wameshachukua mara 4, sisi kushiriki tu hatujawahi, em' acha kunitia machungu aisee.., wawaachie nafasi wengine watoe nuksi kidogo. Any haitadhuru, nadhanii hii itapendeza sasa
 
BUFFON ameamua na kuachia Ngazi kabisa kwenye Timu yao ya TAIFA.

Kweli sio Mavumba
 
Dah ilkua habari mbaya sana, ila sasa tumejipoza na EURO2020 na sasa QATAR tunaenda kukiwasha mpaka fainali na

kubeba ndoo.
 
Back
Top Bottom