Wababa wanalalamika sana kutengwa na watoto wao kimawasliano hata kiuchumi. Je, shida ni nini? Wamama mnaliongeleaje hili? Watoto mnafanya haya kweli?

Hahaaa wamama wenyewe ndo hawa dada zangu kina cariha , Demi etc. utaanza vip kuwasimamia sijui

Si unaona mwenyewe misimamo yao, hadi kidume mwenyewe inasalimu amri, chezeyaaa
Mimi nimemuheshimu baba yangu hadi siku anafariki nimeshakuwa mtu mzima, sijawahi kumtenga au kumuona hana thamani. Baba na mama yangu wote wana thamani sawa.

Ukiona baba hathaminiwi basi tambua kuwa hakusimama vzr kwenye nafasi yake kimajukumu au ni mnyanyasaji kwa mke wake na watoto wameshuhudia.
 
Unajizungumzia wewe au jamii nzima?Hata kama watu wanafanya kazi 50-50 bado wanatakiwa kusaidiana majukumu wakiwa nyumbani ya malezi so haibadilishi fact ya kwamba wababa waliowengi wanakitoka kazini wanaishia bar au wanakojua wao na mama ndo anabeba mzigo wa ulezi!
Nazungumzia ujumla bwana, siku hizi hata wamama wakitoka kazini wanakaa kwenye sofa, kazi yao kutuma tu, hayo malezi walishawaachia wasaídizi wa nyumbani kwa asilimia kubwa tu. 50-50 inaapply sana tu kwa kizazi hiki.
 
Si nyie ndo mnawalisha sumu! Yani wanawake hamjuagi mnachotaka adamu alikuwa anaishi vizuri tu mpaka akina mende Simba na wanyama wote!.. alipokuja sasa mwanamke akafanya yake simba akaanza kumuona adamu Kama ugali tu..🤣
Duh!
 
Wanasababisha wenyewe bwana, nna rafik yang kaolewa lakini yupo close na babake balaa. hii ni sabb babake alkua hvyo alkua anamjulia hali sana kipindi tunasoma, wanaume badilikeni.
 
Mwanamke by nature ni mbinafsi na mwenye moyo uliojaa tamaa, jambo la msingi wanaume ili tusidharaurike uzeeni ni kuweka assets binafsi zitakazo kupa heshima hata mzeeni mwako pasipo tegemea watoto hata mkeo alikukuacha na kwenda kwa watoto wake anauwezo hata kusogeza mke mdogo akakupa furaha
Mke mdogo nae anakuja anazikula mali zako yeye na watoto wake, daah kweli wanaume wanachezewa sana nchi hii...
 
Nafikiri kuna thread yangu niliileta humu wababa wengi wanasababisha haya wao wenywewe,nina mifano iliyo hai kabisa baba anahudumia nyumba ndogo au michepuko zsidi kuliko familia mpaka watoto wapo vyuo, wanajitambua mzee haoni km ni shida ,anaehangaika zsidi na watoto ni mama, mzee akustaafu robo tatu ya hela anatumia na michepuko huku familia inaona na inapata shida then watoto wskipata kazi baba anakuwa na lawama kibao.

Watoto wanajua kuwa baba ahudumiwa na mama kwa kila kitu wanajua wakimpatia mama baba naye atafaidi, tofauti na baba wengi ndiyo hao wanahonga nyumba ndogo.
 
Kumekua na malalamiko mengi kwenye jamii za kitanzania na kiafrika kwa ujumla mara watoto wanapokua na kuanza kujitegemea na umri wa wazazi kusogea, wototo huwa wanakua karibu na mama zao zaidi ya baba zao.

Wababa wengi huumizwa na jambo hili na kujiona kutengwa na watoto wao baada ya watoto hao kupata mafanikio huku wakiamini kabiasa kwamba wake zao (wamama wa hao watoto) wanawafurahia hilo jambo na wana ushirika mkubwa na watoto wao katika kuwatenga

Wamama huwa tunakosea wapi hadi hawa wababa wafikie kulalamika kiasi hiki? Au umri ukienda mapenzi yanaisha na title ya mume inabadilika?

Nini kinawapelekea watoto kuwa na hii distance kubwa kwa baba zao? Je, wanajua kama na wao siku wakizeeka wakatengwa au kuhisi kutengwa itawaumiza?

Ikumbukwe hakuna mtoto wa mzazi mmoja, katika mazingira yoyote yale mtoto atabaki kuwa wa baba na mama unless huyo baba au mama amkatae mtoto

Kwenye imani zetu pia tumeamrishwa kuwaheshimu baba na mama. Hiyo ni amri bila maswali, kazi ni moja tuu kutekeleza. Yaani huwezi sema sababu mama yuko hivi au baba yuko vile sitamheshimu! Matakwa ya amri ni kutekeleza tuu

Familia ni upendo na familia ndio faraja na kimbilio la wakati raha na taabu. Tudumishe upendo

Cc Bushmamy mirisho pm Asprin Sky Eclat 50thebe wahenga wenzangu wote
This is a problem. Ila ninyi wamama ndiyo tatizo aisee.

Shida inaanza tangu watoto wakiwa wadogo, inafika siku ya sikukuu baba unamuachia mama pesa ya nguo za watoto mkiwa chumbani, mama akitoka anaanza, "wanangu nawapendaaa, twendeni nikawanunulie nguo nzuriii, mpendeze", watoto wanajua mama ndiyo katoa pesa. Watoto wanaanza kumhusudu mama.

Pili, mtoto anakosea, mama ananisubiri baba nikirudi ndiyo anamshtaki mtoto kwangu tena tukiwa faragha, mimi nikitoka chumbani ni bakora kwa kwenda mbele, halafu mama huyohuyo anaenda kumbembeleza, utasikia, "mwanangu mzuri, tema mate tukamchape baba!".

Yani nina mifano mingi sana ila sema tu nipo kwenye mazingira ambayo siyo rafiki.
 
Kumekua na malalamiko mengi kwenye jamii za kitanzania na kiafrika kwa ujumla mara watoto wanapokua na kuanza kujitegemea na umri wa wazazi kusogea, wototo huwa wanakua karibu na mama zao zaidi ya baba zao.

Wababa wengi huumizwa na jambo hili na kujiona kutengwa na watoto wao baada ya watoto hao kupata mafanikio huku wakiamini kabiasa kwamba wake zao (wamama wa hao watoto) wanawafurahia hilo jambo na wana ushirika mkubwa na watoto wao katika kuwatenga

Wamama huwa tunakosea wapi hadi hawa wababa wafikie kulalamika kiasi hiki? Au umri ukienda mapenzi yanaisha na title ya mume inabadilika?

Nini kinawapelekea watoto kuwa na hii distance kubwa kwa baba zao? Je, wanajua kama na wao siku wakizeeka wakatengwa au kuhisi kutengwa itawaumiza?

Ikumbukwe hakuna mtoto wa mzazi mmoja, katika mazingira yoyote yale mtoto atabaki kuwa wa baba na mama unless huyo baba au mama amkatae mtoto

Kwenye imani zetu pia tumeamrishwa kuwaheshimu baba na mama. Hiyo ni amri bila maswali, kazi ni moja tuu kutekeleza. Yaani huwezi sema sababu mama yuko hivi au baba yuko vile sitamheshimu! Matakwa ya amri ni kutekeleza tuu

Familia ni upendo na familia ndio faraja na kimbilio la wakati raha na taabu. Tudumishe upendo

Cc Bushmamy mirisho pm Asprin Sky Eclat 50thebe wahenga wenzangu wote
Wewe ni mtoto kwa baba yako. Vipi unaliongeleaje hili?
 
Unaousema n ukwel mkuu

Ila wababa tuache kulea watoto kikauzu badala yake tubadirike hasa wakat huu ambao ulimwengu unaenda kasi unalea mtoto kwa mifumo ya miaka 1980 wakat dunia inehama huko

Mtoto anakupigia simu anataka kujua nyumban mnaendeleaje wewe unajibu kifupi na hauoneshi kufurah kuwa mtoto kakupigia

Ila ukimpigia mama anaonesha furaha anakueleza mambo muhimu kuhusu nyumban

Unategemea mtoto atampenda au atampigia Nani simu kila wakat pale anapohtaj kujua Jambo fulani

.....wazazi hasa wakiume tubadilike....

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Katika hili wababa tubadilike kimalezi na kimahusiano na watoto wetu;

• Usipende kupewa makosa ya watoto na kuyafanyia kazi wakati hukuwepo makosa yakitendeka. Mama awajibike kuwafundisha watoto kama baba hayupo.

• Baba ukirudi nyumbani jaribu kuwa karibu na watoto wako, waonyeshe upendo na wafundishe, usipende kuwa kauzu kila wakati.

• Toa adhabu kulingana na kosa la mtoto, toa adhabu kwa upendo na ukimaliza kumpa adhabu endelea kuonyesha upendo.

• Usikubali hata kidogo mke aonekane yeye ndio kila kitu ndani, wamama wanapenda sana hii kitu, provider wa kila kitu hata kama baba ndio katoa.

• Watoe watoto for evening walks na hata weekends, let them feel dad's presence yani, wapeleke shopping pia ili wajue kuwa baba is providing for them.

Otherwise utatoa pesa, utatunza nyumba, utajenga mijumba but mama ataonekana kila kitu, wewe kituko tu.
Word ☝☝☝☝
 
Back
Top Bottom