Iceberg9
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 24,508
- 46,900
Kuna ndugu yangu mmoja yeye kwake akirudi nyumbani watoto wake hukimbilia chumbani hawakai nae sitting room hujificha huko, nikamuuliza kulikoni akanimbia wanapenda kujifungia chumbani ila nilipokaa nae nikaona anaongea nao l kwa hasira watoto wake yani ni mtu fulani hivi mkali akiwa na watoto, nikamuelezea hali hiyo sio nzuri sana kwa usatawi wa familia yake, baada ya muda akajirekebisha naona imemsaidia sana, na kushukuru, sisi wazazi kuwa wakali sana haijengi wala haimsaidii mtoto zaidi ya kuwatengenezea watoto uwoga usio na faida.