Money Stunna
JF-Expert Member
- Aug 9, 2011
- 13,054
- 6,281
tehe tehe maisha magumu. Uchoyo mwingine hauna maana
mkuu we mdogo kiasi,.cartoon za ctn na itv mi nishamaliza la saba(niko form one),kwa hiyo nilivyokuwa mdogo hakukuwa na tvenzi zetu.....TV inakaa chumbani kwa baba mpaka arudi ndo muombe itolewe,tena mnaangalia kipindi cha katuni kimoja alafu basi inarudishwa na stendi yake ya matairi,glassi zingine marufuku kugusa mpaka mgeni aje,album za picha kedekede kwenye kabati,ila bonge la ufunguo,watoto wanazionaga tu,ila ni marufuku kugusa....vitambaa vya sebuleni sasa wakati wa kuangalia Tiivii,ole wako upangarue,utakiona cha moto,kuondoa ugomvi bora tu ukae chini,kula kwenye kochi ni marufuku,ila baba anaruhusiwa.....baada ya kuangalia VIDEO mnaifunika VIDEO vizuuurrii,isiingie vumbi na vile vitambaa vya kufuma....na baba ndo anakaa na remote control,imefunikwa na ma-nylon kibao ili isizeeke.....akija mgeni nyumbani anafundishwa jinsi ya kuwasha na kuzima Tivii na namna ya kuweka mkanda asije akaugeuza.......kipindi hicho kuwa fundi TV ni bonge la ishu,unakuta fundi ana magari,,,,ni enzi hizzooo,katika utoto wangu,nilishuhudia hayo
mkuu we mdogo kiasi,.cartoon za ctn na itv mi nishamaliza la saba(niko form one),kwa hiyo nilivyokuwa mdogo hakukuwa na tv
usinikumbushe machungu,niliwahi kupata kichapo siku moja !kwa ajili ya mambo haya haya!ila ilikuwa poa!wach tu walivokuwa wanaficha funguo za kabati la TV rum!Hii zamani ilikuwa ni kila nyumba kwa kweli ....lol
Lakini wakuu tukubali kuwa yapo mazingira mtu unaweza kulazimika kufanya kitu kinachofanana na hiki (say kwa kuweka password etc).
TV zinaweza kukuharibia watoto (kutwa ni kutizama katuni au movies/programmes zisizofaa kwa watoto) na hata wadada wa nyumbani (baadhi) wanaweza kushindwa kutimiza majukumu yao ipasavyo na badala yake kutwa wapo kwa TV/movies. Wengine ni waaribifu - deck, remote etc! Yamenitokea haya na kwa kweli yanakera mno. I have stopped paying for DSTv, nikiona haijawa effective nitaondoa TV sebuleni kwangu na kuifungia chumbani kabisa!
Mambo gani ni ya kawaida?...mambo ya kawaida sana ayo
Mambo gani ni ya kawaida?