Wababa kununua nguzo/taulo za ndani watoto wa kike dhambi

Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
50,947
22,098
Jamani nimesikia leo hili swala nkasema naweza pata mawazo hapa yenye maana
kuna topic walikuwa wakijadili clouds fm ,,lakini ikanigusa nina mtoto wa mama mdogo ana miaka 23 mpaka leo ananuliwa Taulo la ndani(PD),nguo za ndani,..

kwa mchango wa wengi wakawa wanakunusha na kusema inategemea mazingira gani na umri gani@!##

kwenu wana JF dhambi kumnunulia mwanao Nguo za ndani????
 
Wala si dhambi, kimfaacho mtu chake. Juzi juzi nilikuwa katika nchi fulani ya Afrika, nikashuhudia binti wa miaka 22 akimnunulia baba yake nguo ya ndani. Nikamwuliza mara mbili, akasema "ndio, ni ya baba hii"
 
Kwanini umununulie wewe baba wakati mama yupo,kwa mila na desturi za Kiafrika vitu kama taulo za ndani au chupi ni vitu nyeti na mtoto akisha vunja ungo tunachukulia ni mtu mzima na haifai kwa baba ukajua kuwa binti ana chupi aina fulani au siku zake zimefika,kwa kifupi kama baba mambo hayo ni ya binti na mama na pia unatakiwa kumpa binti wako angalau vijisenti kidogo kwani hawezi kuja kukuomba hela ya pedi,huo sio utamaduni wetu sisi waafrika na sababu ya mabadiliko vitu kama pedi vilikuwa havitangazwi hadharani kama ilivyo siku hizi,utakuta umekaa mezani unakula pamoja na familia yako mara tangazo la pedi linatokea kwetu sisi wengine hujisikia vibaya na ndio maana siangalii TV pamoja na vijana wangu sababu ya mambo ya hovyo kama hayo
 
Sasa jamni binti wa miaka 23 si bado anasoma hiviyo mzazi inabidi umnunulie au unataka FATAKI wakusaidie kulea:confused:
 
sasa jamni binti wa miaka 23 si bado anasoma hiviyo mzazi inabidi umnunulie au unataka fataki wakusaidie kulea:confused:

yalaaaaa na wewe !!!!yamekuwa hayo !!!!!
Acheni tuendelee kuwanunulia jamani!!!huyu kaniumiza kweli hilo neno""fataki""
 
Kwani ukimnunulia ndio unakuwa umemwona akiwa mtupu? ama ndo unakuwa umetembea naye? Hebu tuache imani potofu jamani, dunia imebadilika sasa kwenye mambo mengi, hizi tamaduni zinadumaza akili sasa, aah, mimi sioni ubaya, zawadi ni zawadi, ili mradi heshima ipo pale pale na haijavurugwa!
 
Inategemea mazingira unamoishi..kama ni kijijini..hii inaweza kuwa ishu.
Kama ni mjini....hizo ni supplies kama supplies nyingine ndani ya nyumba jamani!
Maisha yamebadilika siku hizi.... enzi zile za mababu wakivaa matambara... kweli baba asingehusika..

Siku hizi ulimwengu wa tofauti... unapoenda dukani kufanya shopping ya mwezi au wiki... akina baba msiogope kuchukua sanitary pads pamoja na pampers za watoto wenu!\Cha msingi wewe baba usiende kwa undani kuzigawa ..wewe ziweke stoo au popote kutegemeana na mpangilio wa nyumbani kwako... wenyewe wal;engwa watajua nini cha kufanya...
Ndivyo nionavyo mimi.
 
lovely advice...
 
Good! kila kitu kinategemea na mazingira unayoishi, si lazima majukumu yote ya malezi ya mtoto wa kike yawe kwa mama.
 
Kama waweza mnunulia mkeo why not binti yako? Wenye wake zenu mnajulishwa kila mara Mamaa awapo kwenye siku zake? Angalieni mtasaidiwa si mchezo!
 
Inategemea mazingira unamoishi..kama ni kijijini..hii inaweza kuwa ishu.
Kama ni mjini....hizo ni supplies kama supplies nyingine ndani ya nyumba jamani!
Maisha yamebadilika siku hizi.... enzi zile za mababu wakivaa matambara... kweli baba asingehusika..

Siku hizi ulimwengu wa tofauti... unapoenda dukani kufanya shopping ya mwezi au wiki... akina baba msiogope kuchukua sanitary pads pamoja na pampers za watoto wenu!\Cha msingi wewe baba usiende kwa undani kuzigawa ..wewe ziweke stoo au popote kutegemeana na mpangilio wa nyumbani kwako... wenyewe wal;engwa watajua nini cha kufanya...
Ndivyo nionavyo mimi.

Asante dada, ni ushauri mzuri kweli.
 
asante mama umejibu vizuri
 
Kwanini umununulie wewe baba wakati mama yupo,kwa mila na desturi za Kiafrika vitu kama taulo za ndani au chupi ni vitu nyeti na mtoto akisha vunja ungo tunachukulia ni mtu mzima na haifai kwa baba ukajua kuwa binti ana chupi aina fulani au siku zake zimefika,kwa kifupi kama baba mambo hayo ni ya binti na mama na pia unatakiwa kumpa binti wako angalau vijisenti kidogo kwani hawezi kuja kukuomba hela ya pedi,huo sio utamaduni wetu sisi waafrika na sababu ya mabadiliko vitu kama pedi vilikuwa havitangazwi hadharani kama ilivyo siku hizi,utakuta umekaa mezani unakula pamoja na familia yako mara tangazo la pedi linatokea kwetu sisi wengine hujisikia vibaya na ndio maana siangalii TV pamoja na vijana wangu sababu ya mambo ya hovyo kama hayo

Inakuwaje iwapo mzazi wako(mama au baba) anaumwa, hajiwezi na huna ndugu yeyote wa kukusaidia.. na anhitaji kuogeshwa na kubadilishwa nguo... zikiwemo za ndani... utaacha sababu ya miiko ya Mila? nielimishe hapo!
 
inategemea mazingira unamoishi..kama ni kijijini..hii inaweza kuwa ishu.
Kama ni mjini....hizo ni supplies kama supplies nyingine ndani ya nyumba jamani!
Maisha yamebadilika siku hizi.... Enzi zile za mababu wakivaa matambara... Kweli baba asingehusika..

Siku hizi ulimwengu wa tofauti... Unapoenda dukani kufanya shopping ya mwezi au wiki... Akina baba msiogope kuchukua sanitary pads pamoja na pampers za watoto wenu!\cha msingi wewe baba usiende kwa undani kuzigawa ..wewe ziweke stoo au popote kutegemeana na mpangilio wa nyumbani kwako... Wenyewe wal;engwa watajua nini cha kufanya...
Ndivyo nionavyo mimi.

asante kwa mawazo hayo ni mahitaji muhimu kama mengine t/paper, sabuni, uwekaji na ugawaji ndio muhimu
 
Kama waweza mnunulia mkeo why not binti yako? Wenye wake zenu mnajulishwa kila mara Mamaa awapo kwenye siku zake? Angalieni mtasaidiwa si mchezo!

asante kwa kuwakumbusha akina baba maana nanii wanapenda huduma wanaona mhhhhhhhhh eti mila na desturi
 
sasa jamni binti wa miaka 23 si bado anasoma hiviyo mzazi inabidi umnunulie au unataka fataki wakusaidie kulea:confused:
waambie jirani, wanachokumbuka kwa watoto wao ni ada na nauli tu. Hawajui mahitaji mengine ya watoto wao, jiulize ni akina baba wangapi wamewanunulia vijana wao vitu kama "sendo" mikanda ya suruali, na hata pesa za dharula.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom