Waathirika wa mabomu wakabidhiwa Sh 1.5 milioni

Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
50,956
22,138
Waathirika wa mabomu wakabidhiwa Sh 1.5 milioniNa Geofrey Nyang’oro

WAKATI Chama cha Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa Tanzania (Talugwu) kikitoa msaada wa Sh3milioni kwa ajili ya kusadia waathirika wa mlipuko wa bomu, kamati ya mazishi imekabidhi ubani wa Sh1.5 milioni kwa ndugu wa marehemu waliofariki dunia baada ya mlipuko huo, kutokea.

Akizungumza wakati wa kukabidhi msaada huo, uliofanyika katika ofisi ya mwenyekiti wa kamati ya mazishi, Jarome Bwanausi, Kaimu Mwenyekiti wa Talgwu Taifa, Edina Mwaigomole alisema tukio la mlipuko wa mabamu ni kubwa na kwamba lilisababisha madhara makubwa kwa watu mbalimbali.

Alisema ni wajibu wao kutoa msaada huo kutokana na waathirika wa tukio hilo kuwa sehemu ya jamii.

“Waliothirika na mlipuko ni Watanzania wenzetu, ni wanajamii, na ni dada zetu, mama zetu na wafanyakazi wenzetu, kwa kuwa chama kinawajibika kwa jamii,”alisema Mwaigomela.

Mwaigomole aliwaasa waathirika kuwa wavumilivu na kuendelea kuwa na subira wakati serikali ikiendelea na taratibu za kuwasaidia hadi hapo maisha yao yatakapotengemaa.

Naye Mwenyekiti wa Kamti ya mazishi, Mstaahiki Meya wa Manispaa ya Temeke, Bwanausi alisema msaada huo, unaonyesha ubinadamu wa kweli kwa watu walioathirika.

Alisema kutokana na uharibifu kuwa mkubwa katika eneo hilo, msaada zaidi bado inahitajika ili kuhakikisha watu ambao ni zaidi ya 3,975 wanapata mahitaji ya msingi. Alisema misaada iliyopo hadi sasa haitoshi na aliwaomba wananchi, taasisi na kampuni nyingine za hapa nchini kuendelea kutoa msaada kwa waathirika hao ili kunusuru maisha ya watu walioathirika.
 
Back
Top Bottom