Waathirika wa bomu mkoani Kagera wakumbukwa kwa msaada

mtu watu

JF-Expert Member
Dec 10, 2017
2,123
1,615
Miezi mwili baada ya wanafunzi watano kuuawa na wengine 43 kujeruhiwa kwa bomu la kutupwa kwa mkono katika Shule ya Msingi Kihiga wilayani hapa mkoani Kagera, Kampuni ya Kabanga Nickel imewapa msaada wa vitu mbalimbali vyenye thamani ya Sh20 milioni.

Shule hiyo iliyoanzishwa mwaka 1956 ina wanafunzi 801; wavulana 432 na wasichana 369.
Misaada iliyokabidhiwa ni sare za shule kwa wanafunzi 192 waliokuwa darasa la kwanza mwaka jana, vyakula kwa ajili ya familia tano zilizopoteza watoto na vifaa vya kujifunza na kufundishia kwa shule hiyo.

Akikabidha misaada hiyo juzi kwa waathirika wa tukio hilo la Novemba 8 mwaka jana, ofisa uhusiano wa kampuni hiyo, Francis Widkez alitaja misaada nyingine ni dawa na vifaatiba kwa hospitali ya Rulenge vyenye thamani ya Sh11.34 milioni walikotibiwa majeruhi wa ajali hiyo.

“Pamoja na vifaa vya kujifunza na kufundishia, wanafunzi wote 192 ambao darasa lao lilihusika katika ajali hiyo wamepewa sare za shule, huku familia zilizopoteza watoto wakipewa kila moja vyakula ikiwamo mchele, mahindi, maharagwe, sukari na mafuta ya kupikia vyote vikiwa na thamani ya ShSh8.7 milioni,” alisema Widkez
Akizungumza kwa niaba ya wazazi, diwani wa Kibogora ilipo shule hiyo, Adronis Bulindoli alisema licha ya tukio la bomu kuibua hofu miongoni mwa wananchi, mahudhurio ya wanafunzi shuleni hapo yameendelea kuwa mazuri tangu muhula wa masomo ulipoanza Januari 8.

“Kutokana na tukio la bomu kuharibu darasa la kwanza, wazazi kwa hiari tumekubaliana kila kaya kuchangia Sh5,000 kwa ajili ya kujenga madarasa mapya kwa ajili ya wanafunzi 126 wa darasa la kwanza walioandikishwa na kuanza masomo mwaka huu,” alisema Bulindoli.

Naye mkuu wa wilaya ya Ngara, Michael Mtenjele aliwashukuru waliojitokeza kuwasaidia waathirika wa tukio hilo na kuongeza kuwa, tayari kuna wahisani kutoka nchini Marekani ambao hakuwataja wamejitolea kujenga na kukarabati miuncdombinu ya shule hiyo.
“Ili kuhakikisha usalama kwa wanafunzi, walimu na wananchi wa maeneo jirani na shule, Serikali imewatumia wataalamu wa mabomu kutoka Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) kukagua eneo lote kujiridhisha iwapo hakuna mabomu mengine,” alisema Mtenjele.

Nafasi ya shule
Kwa mujibu wa ukurasa wa tovuti ya Baraza la Mitihani la Taifa (Necta) katika matokeo ya darasala la saba mwaka jana, wanafunzi waliosajili shuleni hapo walikuwa 37 lakini waliofanya mtihani ni 34.

Katika kundi la shule zenye watahiniwa pungufu ya 40, shule hiyo ilishika nafasi ya 53 kati ya 63 kiwilaya na kimkoa ni ya 363 kati ya 435, huku kitaifa ikishika 3,928 kati ya 6,839
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom