Waasisi wa JKK na kongamano kubwa kihistoria la jukwaa la kumhubiri Kristo

BAOBAO

JF-Expert Member
Oct 12, 2012
1,874
547
Waasisi wa Jukwaa la Kumhubiri Kristo ni askofu mkuu Sylvester Gamanywa, Mtume dk. Veron Fernandes, na askofu mkuu Zachary Kakobe ambao wameandaa na kugharimia kongamano kubwa la kihistoria la kwanza Tanzania kufanyika; IWE MVUA AU IWE JUA; watanguruma Jumamosi hii ! Hizi ni habari njema kwa ulimwengu kupitia Jukwaa la Kumhubiri Kristo(JKK) kwa Radio,Televisheni na mitandao ya jamii mbalimbali nitaweka hapo juu kama updates ! Baraza la makanisa ya pentekoste Tanzania limetoa baraka kwa kongamano hili, na maaskofu, mitume, manabii, wachungaji, waalimu, wainjilisti na kila mtu anayemtumikia Mungu amealikwa maalum. Simu ya mawasiliano ni +255754569100 kwa maelezo ya ziada kuhusu tukio hili la kihistoria kwa WATU WOTE WENYE MWILI !

Tumbuke ni tarehe 12-Oktoba-2019, linafanyika Kongamano Kubwa la Kwanza la JUKWAA LA KUMHUBIRI KRISTO (JKK); KUANZIA SAA NNE ASUBUHI HADI SAA KUMI JIONI. Hakikisha unawahi Ukumbi wa BCIC, Mbezi Beach Jogoo, Dar-Es-Salaam; bila kukosa, maana maandalizi yamekamilika kwa utukufu mkubwa wa Mungu anayelipenda kanisa lake. Ni siku ambayo hutaweza kuisahau wala kujuta ukihudhuria na ndugu na rafiki, kwa baraka nyingi za kiroho na kimwili. MARANATHA !!!

1570776364385.png
1570773489766.png
1570773336934.png
1570773443676.png


Ukishindwa kuhudhuria Kongamano kwa sababu zilizo nje ya uwezo wako, unaweza kutazama au kusikiliza mubashara moja kwa moja kupitia na mitandao ya jamii kama Youtube Online kupitia Shalom Tv;Ayo Tv; Global Tv; MTZ Digital; Chomoza tv. Pia chaneli ya AGAPE TV, inapatikana katika ving'amuzi cha Ting HD, Antena STARTIMES, na ungo wa CONTINENTAL. Bandiko hili litakuwa litakuletea habari zote karibu na wewe; lakini kuwa wa kwanza kupata habari za Jukwaa Kumhubiri Kristo kwa kubofya http://bit.ly/ShalomTvTz_Bishop_Gamanywa
 
Shalom Shalom

Samahani ndugu, kilichokuwa kinahitajika ni jukwa la pamoja au ujumbe wenye upako unaoweza kufanya watu wamrudie kristo?

Hivi jumbe kama zile za akina Moses Kolola zilizokuwa zinawafanya walioenda uwanjani kwa nia ya kufanya vurugu kurudi nyumbani wakilia kama watoto wadogo zimepotelea wapi? Nini chanzo cha Mungu kuziacha huduma nyingi (Nguvu zake kutokuwepo?)? JIBU: Pesa imepewa kipaumbele kuliko Mungu mwenyewe, "Kingdom business"imekuwa Business kweli kweli.

Hivi idadi ya makanisa ya kiroho inapokuwa inaongezeka kila uchwao inawiana na ongezeko katika nchi la waamuni wanaompenda Mungu kwa moyo wao wote? Hivi Impact ya ongezeko la makanisa inawiana na Ongezeko la wanaomcha Mungu katika jamii wanapinga kwa vitendo Rushwa, wizi, utapeli, Uzinzi & Uasherati, nk ? Hivi idadi ya watu inapongezeka katika nchini yetu Ratio ya wakristo (Waliokoka) Vs Wasiokoka (Wasio Wakristo) inaongezeka?

Sahamani kwa ujumbe ambao dhamira yake sio kupinga hilo jukwa la JKK bali kuwafanya hao watumishi na mwili wa Kristo kwa ujumla kuliangalia hili suala la kumhubiri Kristo kwa picha pana zaidi bila kusahau kuangalia wapi tulipoanguka.

Ahsante
 
Shalom Shalom
Samahani ndugu, kilichokuwa kinahitajika ni jukwa la pamoja au ujumbe wenye upako unaoweza kufanya watu wamrudie kristo? Hivi jumbe kama zile za akina Moses Kolola zilizokuwa zinawafanya walioenda uwanjani kwa nia ya kufanya vurugu kurudi nyumbani wakilia kama watoto wadogo zimepotelea wapi? Nini chanzo cha Mungu kuziacha huduma nyingi (Nguvu zake kutokuwepo?)? JIBU: Pesa imepewa kipaumbele kuliko Mungu mwenyewe, "Kingdom business"imekuwa Business kweli kweli. Hivi idadi ya makanisa ya kiroho inapokuwa inaongezeka kila uchwao inawiana na ongezeko katika nchi la waamuni wanaompenda Mungu kwa moyo wao wote? Hivi Impact ya ongezeko la makanisa inawiana na Ongezeko la wanaomcha Mungu katika jamii wanapinga kwa vitendo Rushwa, wizi, utapeli, Uzinzi & Uasherati, nk ? Hivi idadi ya watu inapongezeka katika nchini yetu Ratio ya wakristo (Waliokoka) Vs Wasiokoka (Wasio Wakristo) inaongezeka?

Sahamani kwa ujumbe ambao dhamira yake sio kupinga hilo jukwa la JKK bali kuwafanya hao watumishi na mwili wa Kristo kwa ujumla kuliangalia hili suala la kumhubiri Kristo kwa picha pana zaidi bila kusahau kuangalia wapi tulipoanguka.

Ahsante
Naomba kiongozi, fatilia link hii http://bit.ly/ShalomTvTz_Bishop_Gamanywa kufahamu makusudi ya Jukwaa la Kumhubiri Kristo; ambayo kesho pia, wataelezea kwa watu wote kupitia Kongamano hili. ASANTE NA MARANATHA !
 
Back
Top Bottom