Waasi wamiminika Mogadishu

kilimasera

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
3,068
268
Mamia ya wapiganaji wa Somalia wanaotii kundi la kiislamu la al-Shabab wamemiminika mjini Mogadishu, huku walioshuhudia wakisema kuna matarajio ya kuwepo mapigano mazito.
Walioshuhudia wameripoti kuwa wapiganaji, takriban magari 20 na makombora yaliwasili kwenye mji mkuu wa Somalia nyakati za usiku.

Wakazi wa mji huo wamekuwa wakihama maeneo yao kukiwa na imani ya kuwepo hatari ya waasi na majeshi ya serikali kuingia katika mapigano makubwa.

Al-Shabab na makundi mengine ya waasi yanadhibiti eneo kubwa la kusini mwa Somalia.

Hata hivyo, serikali hivi karibuni imeahidi kuhakikisha itafanya mashambulio ili kuweza kudhibiti nchi nzima.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom