Waasi wa Uganda ADF wameshambulia mji wa Beni usiku wakuamkia leo

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,491
54,884
Waasi wa Uganda ADF wameshambulia kata moja ya mji wa beni usiku wakuamkia leo na kuuwa watu wasiopungua 27 na kuwajeruhi wengine tisa. Idadi ya waliofariki dunia,kufuatia shambulizi hilo huenda ikaongezeka kwakuwa hadi sasa jeshi la serikali linaendelea kuwasaka waasi hao, kwenye maeneo zilikopatikana maiti hizo 27 katika msitu wa viunga vya kata ya Ngadi.

Waasi hao walitumia mapanga na risasi kuwaua raia katika kata hiyo. Shambulio la mji wa Beni ni la la tano kwa kipindi cha wiki moja. Raia wa kata ya Boikene katika mji wa Beni waliwazuia wanajeshi wa Umoja wa mataifa Monusco kupita katika barabara ya eneo hilo, wakiwashutumu askari hao wa Umoja wa mataifa kuwa wazembe katika utendaji kazi wao, na kuwaomba kuondoka Congo.Meya wa Beni Nyinyi Bwanakawa ametangaza siku ya leo kuwa ya maombolezi. Mia
10458344_861381567240505_3296638312645357537_n.jpg

Chanzo:DW
 
Askari jeshi wa Congo wajipanga kuwasaka waasi wa ADF huko Beni baada ya kushutumiwa na mauaji ya watu 26 swala ambalo ni vigumu kuhakikisha kwani kupata ADF ni vugumu na kuwauliza ikiwa ni kweli ni wao wahusika.
1545952_777206269007647_6424504803206705071_n.jpg

10626583_777206422340965_4940399299575002620_n.jpg

Chanzo:Austere Malivika. Mia
 
Hii ADF niya Congo au Uganda!!?? Mnanichanganya
 
Vifo vimeongezeka mapaka hii leo... na tumetakiwa kupunguza movements
 
Back
Top Bottom