Waasi wa Syria maji ya shingo,Obama aahidi kuwasaidia silaha.

shekalage

Member
Apr 26, 2013
47
3
[h=2]Waasi wa Syria maji ya shingo,Obama aahidi kuwasaidia silaha.Licha ya kutangazwa kwa azma hiyo ya Marekani, Ikulu ya White House imeweka wazi kwamba, Rais Assad amevuka kile Obama alichowahi kukiita "mstari mwekundu", serikali hiyo inakusudia kuliendelea suala hilo kwa tahadhari.[/h]Uamuzi wa Rais Obama wa kuwapelekea silaha waasi unakuja wakati vikosi vya Assad, vikisaidiwa na Hizbullah, vikisonga mbele kuelekea ngome kuu ya waasi, mji wa kaskazini wa Aleppo.
Tayari kuna kila dalili za kushindwa kwa waasi nchini Syria, kufuatia msaada huo wa Hizbullah, kwani hivi karibuni wamepoteza mji muhimu wa Qusayr. Naibu mshauri wa usalama wa Marekani, Ben Rhodes, amesema kwamba Rais Obama ameamua tu kutoa msaada wa kijeshi, bila ya kuweka wazi ukubwa na upana wa msaada huo.
Hata hivyo, uamuzi huu unaashiria kuhama kwa msimamo wa Marekani kutoka ule wa kuangalia mambo na kuja wa kuingilia mambo, ambao imeuchukua kwa muda mrefu, ikihofia kujirejea kwa hali ya Libya na pia maslahi yake muhimu kwa taifa jirani la Syria, Israel.
Maafisa wa serikali ya Obama wamesema ikiwa waasi watapewa silaha hizo, basi zitakuwa ni zile ndogo ndogo na sio makombora ya kutungulia ndege, kama ambavyo wameomba, na ambayo yatakuwa na matokeo ya haraka kwenye vita vyao dhidi ya Assad.

[h=2]Gazeti la New York Times limeripoti kwamba utumwaji wa silaha hizo utaratibiwa na Shirika la Ujasusi la Marekani, CIA, na huenda ukajumuisha silaha za kukabiliana na vifaru vya kijeshi.
0,,16867488_403,00.jpg
[/h]
 
Mkuu jana Raisi wa Russia bwana Putin alikataa wazo hilo na imewekwa wazi kwamba halikubaliki na Obama amekubali kusalimu amri.

Ila viongozi hao wawili wamekubaliana kukomesha vurugu nchini humo na kuhakikisha kemikali za sumu zinadhibitiwa.

Assad al Bashar ni rafiki kamili wa Russia kisiasa na kijeshi huku Russia ikiipa Syria msaada mkubwa wa vifaa vya kijeshi.

David Cameroon nae alipokutana na Putin siku ya Jumapili pia aligonga mwamba juu ya wazo la kuwapatia silaha waasi wa Syria.

Halafu pia suala la waasi wa Syria ni kama suala la Libya ambapo waasi hawajulikani upande upi wana msimamo mkali na upande upi wametulia hasa wale ambao wanashirikina na kikundi cha Hizbullah.
 
assad must fall haijarish itachukua muda gani,inawezekana ikafanyika pre-emptive strike kwa russian deffence sytmes,pia tumeona misri ikisitisha urafiki na utawala wa assad
 
Back
Top Bottom