Waarabu walivyomponza Boss OBC Loliondo

jembejembe

JF-Expert Member
Jun 9, 2016
581
1,000
Hatimaye Mkurugenzi wa kampuni ya Uwindaji ya Oterlo Businness Coperation (OBC) Isack Lesian Mollel (59) aliyekuwa akisakwa kwa muda mrefu na jeshi la polisi mkoani hapa akiwa amejificha mafichoni kukwepa mkono wa dola ametiwa mbaroni na kupandishwa kizimbani kwa makosa 10 akituhumiwa kuajiri wafanyakazi raia wa kigeni kinyume cha sheria za kazi.

Akisomewa mashtaka hayo mapema leo katika kesi ya jinai namba 1 ya mwaka 2019 mbele ya Hakimu mfawidhi ,Niku Mwakatobe,wa mahakama ya hakimu mkazi Arusha,mwendesha mashtaka wa idara ya kazi mkoani hapa, Emmanuel Mweta alisema kuwa Mnamo Novemba 2018 hadi januari 2019 akiwa mkurugenzi wa kampuni hiyo ya uwindaji aliajiri raia 10 wa kigeni wenye asili ya Kiasia kinyume na sheria za ajira kwa wageni.

Mshtakiwa huyo alinusurika kwenda mahabusu gerezani mara baada upande wa mashtaka kuweka pingamizi akidaiwa kutokuwa mwaminifu baada ya kusakwa kwa muda mrefu bila kupatikana .

Mollel alikuwa akitetewa na mawakili watatu ambao ni Daud Haraka akisaidiana na Goodluck Peter pamoja na Method Kimomogoro alikana mashataka yote 10 na kesi hiyo kuahirishwa kwa ajili ya kutajwa tena Februari 22 mwaka huu.

Mshtakiwa huyo alifanikiwa kupata dhamana mara baada ya mabishano mazito ya mawakili na kufanikiwa kutimiza masharti ya dhamana ikiwa ni pamoja na kuwa na wadhamini wawili wenye barua za utambulisho na kusaini dhamani ya million 40 kila mmoja.

Awali mwendesha mashtaka aliiomba mahakama hiyo kupitia upya dhamana ya mshtakiwa kwani hapo awali alionyesha usumbufu wakati akitafutwa jambo ambalo lilionyesha jinsi gani mshtakiwa si mwaminifu.

Hata hivyo mawakili wa mshtakiwa walipinga hoja hiyo kwa madai kwamba mshtakiwa hakuwa na hati ya wito mahakamani na aliyekuwa akimtafuta ni polisi na si mahakama wala idara ya kazi.

Siku mbili Kabla ya kupatikana kwa mtuhumiwa huyo waziri wa mambo ya ndani ya nchi,Kangi Lugola akiwa mkoani hapa ,alimwagiza kaimu kamanda wa jeshi la polisi mkoani hapa,Longinus Tibushumbwamu kuhakikisha anamsaka popote alipo baada ya kutopatikana kwa muda mrefu ili amfikishe kwenye vyombo vya sheria na kujibu makosa yanayomkabili.

Hata hivyo mshitakiwa huyo kabla ya kutiwa mbaroni juzi aliamua kutoka mafishoni na kujisalimisha kwa jeshi hilo na hatimaye kupandishwa kizimbani.
IMG-20190215-WA0008.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 

DrLove69

JF-Expert Member
Jan 20, 2018
3,123
2,000
Wapelelezi wa kesi hii msisahau kumuuliza Isack Mollel kuhusu uhusiano wake na Godbless Lema katika biashara yao ya maduka haramu ya kubadilishia pesa za kigeni.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom