Waarabu,Wahindi,Wapemba,Wachaga wana siri gani katika biashara?

454

Senior Member
Apr 23, 2017
136
193
Nimekuwa najiuliza Mara nyingi inakuwaje wafanya biashara wakubwa katika nchi yetu ni Waarabu na Wahindi Lakini pia Wachaga na Wapemba nao hawapo nyuma katika ujasiriamali.Ukiangalia sekta ya viwanda wanaomiliki ni Wahindi na Waarabu 99% na upande wa maduka makubwa Wachaga na Wapemba wanaongoza.Sisemi hakuna wengine ila hao niliowataja ni magwiji katika biashara.Sisi makabila mengine tuko nyuma sana.
 
usiwasahau wakinga
 
Wafanyabiashara wengi duniani ni wahamiaji wa nchi nyingine.
Wameleta biashara toka nchi zao miaka nenda rudi
Binadamu wanapohamia sehemu wengi huwa wanaanza na biashara ndogondogo katika community zao
Kutafuta kazi ya kulipwa kwa mwezi ni kama umejifunga kitanzi tu
From hand to mouth

Naona wengi wameanza kufanya biashara siku hizi kinyume na zamani ambapo watu walikuwa wanafikiri mswahili hawezi biashara wala hakuzaliwa nayo

Zama zinabadilika taratibu
Ila jamani hebu mvumbue hata mzani wa mbao maana karanga unapimiwa kwa makadirio tangu nipo primary school 1960's
 
Kuna makabila kibao tu siku hizi wanafanya biashara kama waha, wakinga, wahaya, wasukuma,wakurya, wanyakyusa, wanyaru n.k wee endelea kulalili tu
 
Wabahili
Hawapendi starehe

Mfano mhindi yeye na familia yake na huwa hakai mbali aidha kariakoo juu kapanga ghetto chini duka ,saa 12 kafungua yupo busy saa saba anaenda kula na kugonga kisha anarudi mpaka jioni anafunga hana shida ya kugombania daladala anaenda ndani saa mbili ,tatu anapumzika

Mwarabu anaenda kwenye biashara saa saba anaenda msikitini anarudi anapiga kazi anarudi home kwa familia .
Bar haendi ,kazi na kukaa na familia.

Mchaga mvumilivu na biashara kwenye time management hana tofauti na mhindi na muarabu

Wapo wabahili pia

Uvumilivu
Kushinda kwenye biashara
Kurudi nyumbani kukaa na familia na kupumzika

Ndio maana wanakaa kwenye biashara muda mrefu

Sasa wewe starehe
Pombe sana
Michepuko
Uvumilivu wa kukaa masaa mengi kwenye biashara kwa mwaka huwezi

Wahindi
Waarabu
Wachaga
Wasomalu

Wana heshimu biashara
Wanaheshimu muda

No starehe,michepuko ,bar with exception of wachaga

Pia ndugu hupigana tafu ,baba humsaidia kijana wake
 
Kuna makabila kibao tu siku hizi wanafanya biashara kama waha, wakinga, wahaya, wasukuma,wakurya, wanyakyusa, wanyaru n.k wee endelea kulalili tu
Mkuu sijasema kuwa hawafanyi ila ninaeleza hayo makabila yapo juu
 
Back
Top Bottom