Waarabu,Wahindi,Wapemba,Wachaga wana siri gani katika biashara?

Mwenye Hill water, Hill animal feed...mwenye kiwanda cha banana, viwanda vya matrela etc etc ...wapo wengine wengi tuu wasiojitanganza kwenye tv/media
hata masawe wa akiba comercial....sikatai wakinga wapo on fire ila wao wameanza juzi ila wachaga kitambo icho iwe wapi utamkuta mchaga waulize hata wakenya na wa zambia watakwambia afuwakinga kwenye biashara mostly ila wachaga kuna wasomi na wajasiriamali tujifunzeni
 
Kuna mchaga mmoja pembeni yangu duka anafunga saw 6 usiku hivyo kila akifunga Lazima achome makopo na vifungashio vya majipoa mbele ya duka lake pembezoni wa duka langu
 
Siri ya biashara ni ujanja ujanja ukitaka kuwa straight foward hutoboi n kama utatoboa ni kwa mbinde sana huo ndo ukweli japo hawawezi kukuambia.
 
Nadhani hao wato wana vitu hivi
1. Wana malengo. Yaani yupo radhi alale humo humo dukani ilimladi a save hela kupanua biashara.

2. Ubahili - ukicheki kama wahindi, wakati wewe mfanyakazi wa chini lunch unaenda kula msosi wa maana, bosi wako muhindi amefungasha chakula nyumbani.
Mchaga muda wote atakwambia hana hela, yaani akikupa buku 2 mchaga atakukumbushia zaidi ya miezi sita.

3. Umoja - mchaga ataenda kununua kwa mchaga mwenzie, hata iweje. Mhindi hivyo hivyo.

4. Furaha yao ni kuwa na biashara kubwa na siyo kuvaa vizuri au kuwa na magari makali au nyumba kubwa. Wengi wao ukiwaona hata uwezi hamini ndo mmiliki wa biashara flani. Yaani yeye kuwa na zile biashara roho yake shwari.

5. Mashindano - Wachaga wanapenda mashindano ya maendeleo ya kibiashara. Hawashindani na kila mtu, wana shindana wenyewe kwa wenyewe mwezi wa 12 huko kilimanjaro. Kila mmoja atataka wenzie waone kafikia wapi. Kwahiyo miezi 11 watapambana hatari ili mwezi wa 12 wakaonyeshe.

Sisi wengine biashara ikianza kuingiza tu, mara gari, mara starehe, badilisha gari, iphones na kadharika. Yaani bata batani.

Wachaga wengi starehe ni moshi mwezi wa 12. Hii miezi 11 yote ni kupiga kazi.
 
Wanajituma sana, hawapendi maisha ya kujionesha, wanajitoa na wanafata kilichowaleta sehemu husika. Ni mara nyingi tu utakutana na wahindi au waarabu hata wanawake anaendesha scooter kiroho safi. Na wengine unakuta kampandisha mkewe au binti yake hawana tabu na mtu. Wengi wetu hili hatuliwezi. Angalia vaa yao hawa watu utagundua hawana makuu.
 
kuna KIJANA anakuja kasi kkoo anaitwa Bau aka Prosper sijui unamfahamu?
1234.PNG


Huyu ama?
 
Back
Top Bottom