Elections 2010 waangalizi wabaini kasoro katika kuhesabu kura

Saint Ivuga

JF-Expert Member
Aug 21, 2008
54,635
58,922
Friday, 05 November 2010 08:45

Geofrey Nyang'oro

WAANGALIZI wa ndani wa wameeleza kuwa uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 31 ulikuwa huru na wa haki lakini kulikuwa na kasoro kwenye kuhesabu kura, kwa mujibu wa ripoti yao ya awali.

Waangalizi hao pia wamependekezwa kufumuliwa kwa Tume ya Uchaguzi na kuundwa upya ili isishirikishe wakurugenzi wa halmashauri ambao imewaelezea kuwa ni watumishi wa serikali ambao daima wanakitii chama kilicho madarakani.

TACCEA, muungano unaoundwa na mashirika 17 na unaofanya kazi chini yab uratibu wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), imesema ingawa kasoro zilianza kujitokeza wakati wa kuhesabu kura.

Akisoma ripoti hiyo mbele ya waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana Msemaji mkuu wa TACCEA, Martina Kabisa alisema hali hiyo inatokana na mchakto huo kukumbwa na vitendo vinavyokiuka haki za binadamu.

"Uchaguzi huu ulifanyika katika mazingira huru. Watu walishiriki kampeni na hata kupiga kura. Lakini kumekuwa na matukio mengi yaliyofanya uchaguzi mzima kutokuwa wa haki," alisema Kabisa katika mkutano huo uliofanyika makao makuu ya LHRC.

Kabisa alitaja baadhi ya mambo yanayofanya uchaguzi huo kutokuwa wa haki kuwa ni pamoja na kuchelewesha matokeo katika maeneo ambayo upinzani una nguvu na ambako upinzani ulikuwa na uwezekano wa kushinda.

Kabisa alisema malalamiko ya Dk Slaa dhidi ya uchakachuaji wa kura pia yamethibitishwa na waangalizi hao waliosambaa kila jimbo. Aliitaka Tume ya Uchaguzi (Nec) kutopuuza malalamiko hayo na badala yake iyafanyie kazi ili haki itendeke.

"Madai ya kuwapo kwa tofauti za kura yamethibitishwa na waangalizi wetu walioko kwenye vituo mbalimbali kote nchini. Wametueleza kuwa kura zinazotangazwa ni tofauti na kura za vituoni. Sasa tunaomba Nec iyafanyie kazi madai hayo kama mhusika atakuwa amefuata taratibu za kisheria katika kuyawasilisha," alisema Kabisa.

Katika hatua nyingine umoja huo umependekeza Nec ifumuliwe na kufanyiwa marekebisho ili iwe huru na haki.

Walisema tume hiyo inayosimamia uchaguzi mkuu siyo huru na haitendi haki. Hali hiyo ndiyo inatia shaka kuwa ndio chanzo cha kasoro mbalimbali zilizofanywa kwa lengo la kukibabeba chama tawala, walisema.

"Maafisa wa tume wako chini ya serikali na wengi wao wameteuliwa na rais. Watendaji hawa si rahisi kuona aliyewateua anaanguka na hiyo inaweza kuwa ndiyo moja ya sababu za kufanya kazi kwa upendeleo," alisema Kabisa.

Aliendelea kueleza kuwa kumekuwa na tofauti ya idadi ya kura zilizojumulishwa vituoni na zilizokuwa zikitangazwa na Nec, jambo ambalo linachangia kuwanyima watu haki yao ya kupata viongozi waliowachagua.

Mjumbe wa TaCCEA, Hebron Mwakagendi alisema muungano huo umependekeza wakurugenzi watendaji kuondolewa kazi ya usimamizi wa uchaguzi kwa kuwa ni watumishi wa serikali na hivyo hawawezi kuwa huru na kutenda haki.

Alisema maofisa hao wa serikali kutumika kwenye uchaguzi imekuwa chanzo cha kushamili kwa vitendo vinavyokwamisha haki ya mpigakura.

"Pendekezo jingine ni kuwekwa hadharani kwa daftari la wapigakura ili kila mtu aweze kulipitia. Hii itapunguza usumbufu wa kutafuta majina wakati wa uchaguzi," alisema.

Kuhusu matumizi ya vifaa vya kisasa ambavyo maafisa wengi walionekana kushindwa kuvitumia, mjumbe huyo alisema TACCEA ilipendekeza wahusika kupatiwa mafunzo mapema ili kuwajengea uwezo wa kutumia teknolojia hiyo.

"Sambamba na hilo tume imetakiwa kuajiri wafanyakazi wake watakaoshiriki mafunzo mbalimbali, zikiwamo taratibu za uchaguzi ili kuondoa usumbufu uliojitokeza katika uchaguzi wa awamu hii," alisema.

Alisema katika uchaguzi wa mwaka huu wasimamizi walikuwa na uelewa mdogo na baadhi yao walilazimika kufundishwa wakiwa kazini.

Mjumbe huyo alieleza pia kuwa kitendo cha ujumlishaji kura kufanywa na watu wachache ni kasoro nyingine walioibaini katika uchunguzi wao.

"Tume inatakiwa kufanya majumuisho ya kura kwa uwazi kwa kushirikishi wadau mbalimbali zikiwamo asasi za kiraia badala ya kujifungia kama ilivyo sasa ili kuondoa matatizo ya kutoa kura zinazotofautiana na zile za vituoni," alisema.

Baadhi ya taasisi zinazounda muungano huo ni Leadership Forum, ForDIA, TANLAP, WiLDAF, SAHRiNGON, TAHURIFO, MPI, ACCORD, ZLSC, HAKIMADINI, LEAT na Hivos na Sida.

CHANZO: Mwananchi
 
kuna mwenye usemi? kila kitu kipo uchi hapa na mengi tutayasikia
 
mwendelezo.......

KASORO mbalimbali zilizojitokeza katika uchaguzi mkuu, ikiwemo muundo mbaya wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na matumizi ya teknolojia mpya, zimedaiwa kusababisha kutokuwa wa haki.

Mbali na kasoro hizo, zingine ni uwezo mdogo wa wasimamizi wa uchaguzi juu ya baadhi ya taratibu za uchaguzi, daftari la wapiga kura kutopatikana kiurahisi ili watu wahakiki majina yao, majina ya wapiga kura kutokuonekana vituoni na kukosewa kwa namba za kitambulisho cha mpiga kura, ambazo ziliwafanya wananchi kushindwa kutumia haki yao ya kuchagua kiongozi wanayemtaka.

Hayo yamo katika taarifa ya awali ya Mtandao wa Mashirika 17 ya Asasi za Kiraia (TACCEO) yakiongozwa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), ambayo yalikuwa na waangalizi wa uchaguzi katika majimbo kadhaa ya nchini.

Akizungumza na waandishi wa habari jana Dar es Salaam, kwa niaba ya TACCEO, mmoja wa wajumbe wa mtandao wa mashirika hayo, Bi. Martina Kabisama alisema kuwa kasoro hizo zimeufanya uchaguzi huo uwe huru lakini si wa haki.

"Ingawa tunakiri kuna baadhi ya maeneo NEC imefanya vizuri na inaweza kusifiwa, lakini leo tunajielekeza katika mapungufu zaidi.

Daftari la wapiga kura halikupatikana kwa urahisi pamoja na kuwa liliwekwa mtandaoni, lakini si wananachi wengi wanaweza ku-access (kupata) taarifa za mtandaoni…lakini pia hata huko lilikuwa halipatikani kwa urahisi.

"Watu wengi hawakuona majina yao kwenye daftari, lakini hata vituoni yalipobandikwa wengi walipata taabu kuyaona au hawakuyaona kabisa…bado hata namba yenyewe ya watu waliosajiliwa inatia shaka maana inaonesha kuwa karibu nusu ya Watanzania wote nchini wana sifa za kupiga kura, kitu ambacho kinatia wasiwasi," alisema Bi. Kabisama.

Source: Majira
 
Ikiwa kama mambo yako hadharani namna hii, sijui tume wanajisikiaje. Lakini nadhani kuna taratibu za kuwakilisha tatizo hili, kama waangalizi hawa walivyosema, "ikiwa kama walalamikaji watataka" kuna taratibu za kufanya hivyo ili haki itendeke.
 
Hapa Dawa kubwa ni kuvunja hilo litume lao, NEC ili iundwe tume huru ambayo itakuwa hailalii upande wowote. Naimani tutafika salama kuunda hiyo tume, ila kwa ndugu zetu CCM najua watalikataa hilo.
 
waangalizi wabaini kasoro katika kuhesabu kura Send to a friend Friday, 05 November 2010 08:45 0diggsdigg

Geofrey Nyang’oro
WAANGALIZI wa ndani wa wameeleza kuwa uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 31 ulikuwa huru na wa haki lakini kulikuwa na kasoro kwenye kuhesabu kura, kwa mujibu wa ripoti yao ya awali.

Waangalizi hao pia wamependekezwa kufumuliwa kwa Tume ya Uchaguzi na kuundwa upya ili isishirikishe wakurugenzi wa halmashauri ambao imewaelezea kuwa ni watumishi wa serikali ambao daima wanakitii chama kilicho madarakani.
TACCEA, muungano unaoundwa na mashirika 17 na unaofanya kazi chini yab uratibu wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), imesema ingawa kasoro zilianza kujitokeza wakati wa kuhesabu kura.
Akisoma ripoti hiyo mbele ya waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana Msemaji mkuu wa TACCEA, Martina Kabisa alisema hali hiyo inatokana na mchakto huo kukumbwa na vitendo vinavyokiuka haki za binadamu.

“Uchaguzi huu ulifanyika katika mazingira huru. Watu walishiriki kampeni na hata kupiga kura. Lakini kumekuwa na matukio mengi yaliyofanya uchaguzi mzima kutokuwa wa haki,” alisema Kabisa katika mkutano huo uliofanyika makao makuu ya LHRC.

Kabisa alitaja baadhi ya mambo yanayofanya uchaguzi huo kutokuwa wa haki kuwa ni pamoja na kuchelewesha matokeo katika maeneo ambayo upinzani una nguvu na ambako upinzani ulikuwa na uwezekano wa kushinda.
Kabisa alisema malalamiko ya Dk Slaa dhidi ya uchakachuaji wa kura pia yamethibitishwa na waangalizi hao waliosambaa kila jimbo. Aliitaka Tume ya Uchaguzi (Nec) kutopuuza malalamiko hayo na badala yake iyafanyie kazi ili haki itendeke.

“Madai ya kuwapo kwa tofauti za kura yamethibitishwa na waangalizi wetu walioko kwenye vituo mbalimbali kote nchini. Wametueleza kuwa kura zinazotangazwa ni tofauti na kura za vituoni. Sasa tunaomba Nec iyafanyie kazi madai hayo kama mhusika atakuwa amefuata taratibu za kisheria katika kuyawasilisha,” alisema Kabisa.

Katika hatua nyingine umoja huo umependekeza Nec ifumuliwe na kufanyiwa marekebisho ili iwe huru na haki.
Walisema tume hiyo inayosimamia uchaguzi mkuu siyo huru na haitendi haki. Hali hiyo ndiyo inatia shaka kuwa ndio chanzo cha kasoro mbalimbali zilizofanywa kwa lengo la kukibabeba chama tawala, walisema.

“Maafisa wa tume wako chini ya serikali na wengi wao wameteuliwa na rais. Watendaji hawa si rahisi kuona aliyewateua anaanguka na hiyo inaweza kuwa ndiyo moja ya sababu za kufanya kazi kwa upendeleo,” alisema Kabisa.
Aliendelea kueleza kuwa kumekuwa na tofauti ya idadi ya kura zilizojumulishwa vituoni na zilizokuwa zikitangazwa na Nec, jambo ambalo linachangia kuwanyima watu haki yao ya kupata viongozi waliowachagua.

Mjumbe wa TaCCEA, Hebron Mwakagendi alisema muungano huo umependekeza wakurugenzi watendaji kuondolewa kazi ya usimamizi wa uchaguzi kwa kuwa ni watumishi wa serikali na hivyo hawawezi kuwa huru na kutenda haki.
Alisema maofisa hao wa serikali kutumika kwenye uchaguzi imekuwa chanzo cha kushamili kwa vitendo vinavyokwamisha haki ya mpigakura.

"Pendekezo jingine ni kuwekwa hadharani kwa daftari la wapigakura ili kila mtu aweze kulipitia. Hii itapunguza usumbufu wa kutafuta majina wakati wa uchaguzi," alisema.

Kuhusu matumizi ya vifaa vya kisasa ambavyo maafisa wengi walionekana kushindwa kuvitumia, mjumbe huyo alisema TACCEA ilipendekeza wahusika kupatiwa mafunzo mapema ili kuwajengea uwezo wa kutumia teknolojia hiyo.
"Sambamba na hilo tume imetakiwa kuajiri wafanyakazi wake watakaoshiriki mafunzo mbalimbali, zikiwamo taratibu za uchaguzi ili kuondoa usumbufu uliojitokeza katika uchaguzi wa awamu hii," alisema.
Alisema katika uchaguzi wa mwaka huu wasimamizi walikuwa na uelewa mdogo na baadhi yao walilazimika kufundishwa wakiwa kazini.

Mjumbe huyo alieleza pia kuwa kitendo cha ujumlishaji kura kufanywa na watu wachache ni kasoro nyingine walioibaini katika uchunguzi wao.
"Tume inatakiwa kufanya majumuisho ya kura kwa uwazi kwa kushirikishi wadau mbalimbali zikiwamo asasi za kiraia badala ya kujifungia kama ilivyo sasa ili kuondoa matatizo ya kutoa kura zinazotofautiana na zile za vituoni," alisema.
Baadhi ya taasisi zinazounda muungano huo ni Leadership Forum, ForDIA, TANLAP, WiLDAF, SAHRiNGON, TAHURIFO, MPI, ACCORD, ZLSC, HAKIMADINI, LEAT na Hivos na Sida.

mwananchi

Tupo pamoja kuwa kupiga kura kuliwa huru lakini haki haikutendeka kwenye kuhesabu kura. Hivyo marekebisho niya muhimu. Nadhani kwa kuwa tumepata kikosi chapo ni kidogo lakini kihakikishe marekebisho haya yanafanyiwa kazi.
 
Back
Top Bottom