Uchaguzi 2020 Waangalizi wa Uchaguzi kutoka Jumuiya ya Afrika Mashariki kuwepo mikoa 13

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
Timu ya watazamaji kutoka Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) yenye waangalizi 59 imewasili nchini kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu utakaofanyika kesho.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, kiongozi wa watamazaji hao wa uchaguzi wa EAC, Rais Mstaafu wa Burundi, Sylvestre Ntibantunganya alisema wapo 59 na watasambaa mikoa 13 nchini ya Dar es Salaam, Tanga, Unguja, Pemba, Lindi, Mtwara, Dodoma, Mbeya, Kigoma, Singida, Kilimanjaro, Morogoro na Mwanza.

Alisema wakati kuingiwa mkataba wa kuanzishwa Jumuiya ya Afrika Mashariki, nchi Wanachama zilikubaliana kuwa na kigezo cha kuwa na uchaguzi huru na wa haki.

"Hivyo kila nchi mwanachama inapokuwa na zoezi la uchaguzi mkuu wa Rais na wabunge wa Jumuiya ya Afrika Mashariki hutuma watazamaji wa uchaguzi katika nchi mwanachama inayofanya uchaguzi ili kuhakiki kama imezingatia vigezo vilivyokubaliwa, sheria na Katiba ya nchi husika."

“Huo ndio msingi wa uwapo wa timu ya watazamaji wa Jumuiya ya Afrika Mashariki katika uchaguzi nchini Tanzania,” alisema.

Ntibantunganya alisema zoezi hilo halilengi tu kuangalia uchaguzi unavyofanyika, bali pia ni sehemu ya kujifunza ili mazuri yatakayobainika Jumuiya izishauri nchi nyingine kuiga na pale itakapobainika mapungufu nchi mwanachama husika ashauriwe kuchukua hatua za kurekebisha ili zisijirudie tena.

"Dhumuni la waangalizi hawa ni kufanya uangalizi wa mchakato mzima wa uchaguzi, kutoa tathmini iliyo sawa na kamili, kubaini changamoto, udhaifu na fursa ambazo zinaweza kujumuishwa kama mafunzo bora katika mchakato wa uchaguzi na Bodi za Usimamizi wa Uchaguzi katika Jumuiya ya Afrika Mashariki," alisema.

Alisema waangalizi hao wanatoka kwenye Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki (EALA), mabalozi wa vijana wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, viongozi wa vijana na wawakilishi kutoka wizara zinazohusika na masuala ya Jumuiya ya Afrika Mashariki kutoka nchi wanachama.

Wengine ni kutoka tume za kitaifa za uchaguzi, Mahakama ya Haki ya Afrika Mashariki na Sekretarieti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Alisema dhumuni la jumuiya hiyo ni kujenga imani ya wananchi katika michakato ya uchaguzi kwa kuhamasisha wapiga kura na wadau wengine kushiriki kwa uhuru na katika mazingira ambayo yanakuza ushindani na uvumilivu bila vitisho au uvinjifu wa amani.

Alisema jumuiya hiyo pia inatoa mapendekezo ya kuimarisha mchakato mzima wa uchaguzi sio tu kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lakini pia kwa nchi zote wanachama wa jumuiya hiyo.

Kuanzia Oktoba 24 hadi 25 waangalizi wa uchaguzi huo walipata mafunzo kabla ya kuanza rasmi zoezi la uangalizi Oktoba 26.

Ntibantunganya alisema Ibara ya tatu (3) aya ya 3 (b) ya Mkataba wa Uanzishwaji wa Jumuiya ya Afrika Mashariki inazitaka nchi wanachama kuheshimu kanuni za utawala bora, demokrasia, haki za binadamu na za kijamii.
 
Kwa hiyo ni mikoa 13 tu ndio itakayokuwa na uangaliz wa kimataifa?

Mkuu hao wa EAC unategemea wamekuja kutenda haki? mimi hata wangekuwepo mikoa 2 nisingeshangaa, EAC yote imekaliwa na madikteta ambao wote ni marafiki wa Jiwe
 
Ni vizuri, wamepata fursa ya kujifunza kwa baba la demokrasia Afrika, Tanzania.
 
mkuu hao wa EAC unategemea wamekuja kutenda haki ? mimi hata wangekuwepo mikoa 2 nisingeshangaa,EAC yote imekaliwa na madikteta ambao wote ni marafiki wa Jiwe
Ukipewa kazi ya kuchunguza akili za vijana wa Chadema sidhani kama utapata jibu litakalopinga kuwa hao ni vichaa na wendawazimu,

Juzi si ndo nyie mlikuwa mkiimba, Magufuli kaharibu mahusiano ya Kimataifa nchi zote kasoro Burundi?

Leo tena mnasema nchi zote za EAC Ni marafiki wa JpM na nchi yetu?

Very ignorant you people wa Chadema
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom