Waangalizi wa Commonwealth hawajui hatuna Tume huru ya uchaguzi!!!!!!!!!!!!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Waangalizi wa Commonwealth hawajui hatuna Tume huru ya uchaguzi!!!!!!!!!!!!!

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Rutashubanyuma, Nov 2, 2010.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Nov 2, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,345
  Likes Received: 418,852
  Trophy Points: 280
  Waangalizi wa Commonwealth wamefyatua taarifa yao ya awali ya kutathmini chaguzi yetu bila ya kujua ya kuwa haina tambuzi kuwa hatuna Tume huru ya uchaguzi ila tuna Tume ya Uchaguzi ya chama cha tawala iitwayo CCM-NEC...............

  wamekosoa mambo mbalimbali lakini tathmini yao ni bure bila ya kutambua ya kuwa Tume ya Uchaguzi yaani NEC inaongozwa na kuratibiwa na wakurugenzi wa halmashauri ambao ajira zao zinathibitiwa na wagombea wa chama tawala ambao ni magwiji wa kufuta majina ya wagombea wa upinzani na kujipitisha bila ya kupingwa kinyume na matakwa ya kikatiba................

  Maoni kama haya hapo chini ya waangalizi hao ni changa la usoni kwani bila ya kutambua sheria ya uchaguzi haina mashiko ya kuwazuia CCM kufanya watakavyo ni sawasawa na haipo...........Mfano wapi NEC imefuatilia matumizi ya wagombea au msajili wa vyama na fedha hizo CCM hayo mabilioni wameyatoa wapi?

  Yaani hawa waangalizi ni watalii tu.........
   
Loading...