Uchaguzi 2020 Waangalizi wa Afrika Mashariki wamesema uchaguzi umefanyika kwa kufuata utaratibu

Mocumentary

JF-Expert Member
Jul 31, 2017
766
1,954
Rais wa zamani Silvestre Ntibantunganya ambaye ndiye Mwenyekiti wa ujumbe wa waangalizi kutoka Afrika Mashariki, amesema kuwa uchaguzi mkuu Tanzania ulifanyika kwa kufuata taratibu.

Ujumbe wa waangalizi wa EAC ulikuwa na wajumbe 89 waliosambazwa maeneo mbalimbali , kufuatilia mchakato wa upigaji kura lakini pia utangazaji wa matokeao ya kura hizo.

Bwana Ntabitunganya amesema walikutana na wadau wa uchaguzi ikiwemo tume na vyama vya kisiasa na waangalizi wengine.

Ujumbe huo umesema umeshuhudia hali ya usalama kaika maeneo mbalimbali, watu wakifanya kampeni kwa uhuru kabla ya kuanza shughuli ya upigaji kura.

Katika siku ya kupiga kura vituo vilifunguliwa kwa muda muafaka, masuala ya ya kiufundi yalifanywa kwa weledi.

Waangalizi walishuhudia wapiga kura wakitekeleza wajibu wao bila kutishwa wala hofu.

''Baadhi ya vyama vya siasa au wagombea wamelalamikia kuhusu namna uchaguzi ulivyoandaliwa na namna matokeo yalivyotangazwa na tume ya taifa ya uchaguzi.Ujumbe wa waangalizi unatoa wito kwa vyama vya kisiasa, kufuata taratibu za kisheria kuonesha kutoridhishwa kwao na matokeo.Tunatoa wito kwa vyama vya siasa kuweka mbele maslahi ya Watanzania, ikiwemo usalama na amani na kuepuka vitendo vyovyote vya uvunjifu wa amani'', alisema.

Ujumbe umewapongeza Watanzania kwa busara walioionesha katika shughuli za wakati wa kampeni na uchaguzi kwa kuzingatia kwanza masuala ya amani na usalama.

''Ujumbe unawasisitiza wagombea, vyama vya siasa na wengine wote kuendelea kuimarisha usalama na amani ''. Alisema mwenyekiti wa ujumbe huo Bw. Ntibantunganya.

Chanzo: BBC swahili
 
IMG_20201030_190720.jpg

Nina unga mkono hoja mweshimiwa tuongeze kutoka miaka 10 adi 30
 
Uchaguzi wetu kwa upande wa haki za wapiga kura ulienda vizuri kwa maana watu wakipiga kura zao kwa uwazi na utulivu.kwenye uchaguzi huu haki za wagombea kupitia mawakala wao haikutendeka.kwa mfano baadhi ya vituo mawakala wa vyama vya siasa waliingia kwenye vituo vya kupigia kura baada ya masaa manne kupita, pia baadhi ya vituo mawakala wa upinzani walitolewa na polis na kupelekwa rumande za polis.taarifa zisizo rasmi inasema kwamba baadhi ya wasimamizi wa uchaguzi walitumika kuingiza kura kwenye mabox kura walizokuwa nazo ambao zilitiwa tiki kabisa za ccm.pia polis wanatuhumiwa kutumika kupenyeza hizo kura.Uchaguzi wa mwaka huu wizi umefanywa na wasimamizi wa uchaguzi wenyewe ngazi za vituo kwa kushirikiana na ccm, pamoja na wakurugenzi wa halmashauri.
 
Chukulia mfano wewe udokoe pesa bila muhusika kujua labda shekeli kadhaa! Halafu kakuona nduguyo nae kaingiwa tamaa anasema anataka kudokoa ! Jibu litakua dokoa tu wala sitokusema pia maana ulinifichia siri!
 
Tunashukuru kwa report waangalizi toka afrika mashariki. Mungu ibariki Tanzania Mungu ibariki Afrika
Tuondoe presha, chuki, matusi tujenge familia zetu na nchi
 
Back
Top Bottom