Waangalizi EU: Matokeo ya urais Bara, Z’bar hayakuwa wazi

abdulahsaf

JF-Expert Member
Aug 31, 2010
858
130
Written by amini // 12/02/2011 // Habari // 2 Comments

na Bakari Kimwanga
WAANGALIZI wa Uchaguzi Mkuu kutoka nchi za Jumuiya ya Ulaya (EU), wametoa masikitiko yao juu ya kutokuwa na uwazi katika ujumlishaji wa matokeo ya urais, ubunge na udiwani katika uchaguzi mkuu wa mwaka jana.
Mwangalizi mkuu wa uchaguzi kutoka nchi za jumuiya ya ulaya David Martin, alisema hayo jana alipokuwa akitoa taarifa ya mwisho ya jumuiya hiyo na ujumbe wa waangalizi wa Uchaguzi Mkuu na kusema kuwa ni muhimu kwa Tanzania kuwa na utaratibu wa mfumo mzuri utakaokuwa na mazingira ya kidemokrasia.
“Jumuiya ya Ulaya ilisikitishwa sana hasa na hatua ya kukosekana kwa uwazi wa pamoja katika ujumlishaji wa matokeo ya uchaguzi mkuu, sasa ni muhimu kuyaangalia haya kabla ya uchaguzi wa mwaka 2015,” alisema Martin.
Akifafanua ripoti hiyo yenye mapendekezo 30, kiongozi huyo wa timu ya waangalizi wa EU, alisema sasa umefika wakati kwa serikali ya Tanzania kuridhia mapendekezo kwa nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa juu ya hatua ya kupinga matokeo ya uchaguzi mara baada ya kutangazwa kuliko ilivyo sasa.
“ Ni muhimu Tanzania ikawa na utaratibu unaoeleweka kwani wao ni wanachama wa UN, kwani hali hiyo inaweza kuzidisha na kudumisha demokrasia ya kweli, wadau hasa vyama na wagombea urais wanashindwa kupinga matokeo hata kama kuna kuna kasoro zimejitokeza,” alisema Martin.
Ripoti hiyo ya waangalizi ilisema kuwa wakati wa hatua za mwisho ya kujumlisha matokeo Rais kwa pande zote mbili yaani bara za Zanzibar hazikuwa wazi kutokana na timu za waangalizi wa uchaguzi na waandishi wa habari kupingwa marufuku kufuatilia mchakato huo.
Hata hivyo waangalizi hao wameitaka serikali kutowatumia polisi katika hali iliyoleta taswira tofauti kwa wapiga kura kwa kuingiwa na hofu ya kukamatwa na hata kutopiga kura kabisa.
Hata hivyo timu hiyo ilisema kuwa kuna baadhi ya wapiga kura ambao walikuwa wakiunga mkono harakati za wagombea wa upinzani walifanyiwa hila na kuondolewa katika orodha ya wapiga kura bila kuwa na sababu za kuondolewa kwao katika orodha hiyo.
Kiongozi huyo wa timu ya waangalizi alisema umefika wakati kuwa ni kupunguza muda wa kufanya kampeni kwa kipindi kirefu ili kwenda sambamba na bajeti za vyama vya siasa kuliko ilivyo sasa ambapo chama tawala pekee ndicho chenye uwezo wa kuyafikia maeneo mengi kutokana na kuwa na rasilimali za kutosha.
European-Union report
 
Ripoti ishapelekwa masjala, na hutasikia good conclusions drawn from it. Zaidi ya kusikia ikipondwa kwamba kazi yao ni kuangalia na si kuamua kipi kizuri/kibaya
 
..Na ubaya hivyo vitu hata huwa havina impact kwa nchi kama bongo...labda kwingineko...after all this is a dead story..tufikirie tu namna ya kujinasua na yanayotusibu mpaka sasa...
 
Back
Top Bottom