Waangalizi EU: Matokeo ya urais Bara, Z’bar hayakuwa wazi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Waangalizi EU: Matokeo ya urais Bara, Z’bar hayakuwa wazi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by mabadilikosasa, Feb 12, 2011.

 1. m

  mabadilikosasa JF-Expert Member

  #1
  Feb 12, 2011
  Joined: Dec 23, 2010
  Messages: 379
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  na Bakari Kimwanga


  [​IMG]
  WAANGALIZI wa Uchaguzi Mkuu kutoka nchi za Jumuiya ya Ulaya (EU), wametoa masikitiko yao juu ya kutokuwa na uwazi katika ujumlishaji wa matokeo ya urais, ubunge na udiwani katika uchaguzi mkuu wa mwaka jana.
  Mwangalizi mkuu wa uchaguzi kutoka nchi za jumuiya ya ulaya David Martin, alisema hayo jana alipokuwa akitoa taarifa ya mwisho ya jumuiya hiyo na ujumbe wa waangalizi wa Uchaguzi Mkuu na kusema kuwa ni muhimu kwa Tanzania kuwa na utaratibu wa mfumo mzuri utakaokuwa na mazingira ya kidemokrasia.
  “Jumuiya ya Ulaya ilisikitishwa sana hasa na hatua ya kukosekana kwa uwazi wa pamoja katika ujumlishaji wa matokeo ya uchaguzi mkuu, sasa ni muhimu kuyaangalia haya kabla ya uchaguzi wa mwaka 2015,” alisema Martin.
  Akifafanua ripoti hiyo yenye mapendekezo 30, kiongozi huyo wa timu ya waangalizi wa EU, alisema sasa umefika wakati kwa serikali ya Tanzania kuridhia mapendekezo kwa nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa juu ya hatua ya kupinga matokeo ya uchaguzi mara baada ya kutangazwa kuliko ilivyo sasa.
  “ Ni muhimu Tanzania ikawa na utaratibu unaoeleweka kwani wao ni wanachama wa UN, kwani hali hiyo inaweza kuzidisha na kudumisha demokrasia ya kweli, wadau hasa vyama na wagombea urais wanashindwa kupinga matokeo hata kama kuna kuna kasoro zimejitokeza,” alisema Martin.
  Ripoti hiyo ya waangalizi ilisema kuwa wakati wa hatua za mwisho ya kujumlisha matokeo Rais kwa pande zote mbili yaani bara za Zanzibar hazikuwa wazi kutokana na timu za waangalizi wa uchaguzi na waandishi wa habari kupingwa marufuku kufuatilia mchakato huo.
  Hata hivyo waangalizi hao wameitaka serikali kutowatumia polisi katika hali iliyoleta taswira tofauti kwa wapiga kura kwa kuingiwa na hofu ya kukamatwa na hata kutopiga kura kabisa.
  Hata hivyo timu hiyo ilisema kuwa kuna baadhi ya wapiga kura ambao walikuwa wakiunga mkono harakati za wagombea wa upinzani walifanyiwa hila na kuondolewa katika orodha ya wapiga kura bila kuwa na sababu za kuondolewa kwao katika orodha hiyo. Kiongozi huyo wa timu ya waangalizi alisema umefika wakati kuwa ni kupunguza muda wa kufanya kampeni kwa kipindi kirefu ili kwenda sambamba na bajeti za vyama vya siasa kuliko ilivyo sasa ambapo chama tawala pekee ndicho chenye uwezo wa kuyafikia maeneo mengi kutokana na kuwa na rasilimali za kutosha.
   
 2. Mohammed Shossi

  Mohammed Shossi Verified User

  #2
  Feb 12, 2011
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 3,986
  Likes Received: 123
  Trophy Points: 160
  Mods unganisha hii na ile ya kingereza...............
   
 3. Omuregi Wasu

  Omuregi Wasu JF-Expert Member

  #3
  Feb 12, 2011
  Joined: May 21, 2009
  Messages: 753
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Mkuu Mud Kwani zimepishana kwenye kuwasilisha mahudhui ya wasimamizi hao wa EU au unataka kutupa raha zaidi wasomaji ili tupate mwanga mkubwa wa mtizamo wa EU ulivyo?
   
Loading...