Waangalizi EU: Matokeo ya urais Bara, Z’bar hayakuwa wazi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Waangalizi EU: Matokeo ya urais Bara, Z’bar hayakuwa wazi

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Rutashubanyuma, Feb 12, 2011.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Feb 12, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,789
  Likes Received: 416,595
  Trophy Points: 280
  Waangalizi EU: Matokeo ya urais Bara, Z’bar hayakuwa wazi


  na Bakari Kimwanga


  [​IMG] WAANGALIZI wa Uchaguzi Mkuu kutoka nchi za Jumuiya ya Ulaya (EU), wametoa masikitiko yao juu ya kutokuwa na uwazi katika ujumlishaji wa matokeo ya urais, ubunge na udiwani katika uchaguzi mkuu wa mwaka jana.
  Mwangalizi mkuu wa uchaguzi kutoka nchi za jumuiya ya ulaya David Martin, alisema hayo jana alipokuwa akitoa taarifa ya mwisho ya jumuiya hiyo na ujumbe wa waangalizi wa Uchaguzi Mkuu na kusema kuwa ni muhimu kwa Tanzania kuwa na utaratibu wa mfumo mzuri utakaokuwa na mazingira ya kidemokrasia.
  “Jumuiya ya Ulaya ilisikitishwa sana hasa na hatua ya kukosekana kwa uwazi wa pamoja katika ujumlishaji wa matokeo ya uchaguzi mkuu, sasa ni muhimu kuyaangalia haya kabla ya uchaguzi wa mwaka 2015,” alisema Martin.
  Akifafanua ripoti hiyo yenye mapendekezo 30, kiongozi huyo wa timu ya waangalizi wa EU, alisema sasa umefika wakati kwa serikali ya Tanzania kuridhia mapendekezo kwa nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa juu ya hatua ya kupinga matokeo ya uchaguzi mara baada ya kutangazwa kuliko ilivyo sasa.
  “ Ni muhimu Tanzania ikawa na utaratibu unaoeleweka kwani wao ni wanachama wa UN, kwani hali hiyo inaweza kuzidisha na kudumisha demokrasia ya kweli, wadau hasa vyama na wagombea urais wanashindwa kupinga matokeo hata kama kuna kuna kasoro zimejitokeza,” alisema Martin.
  Ripoti hiyo ya waangalizi ilisema kuwa wakati wa hatua za mwisho ya kujumlisha matokeo Rais kwa pande zote mbili yaani bara za Zanzibar hazikuwa wazi kutokana na timu za waangalizi wa uchaguzi na waandishi wa habari kupingwa marufuku kufuatilia mchakato huo.
  Hata hivyo waangalizi hao wameitaka serikali kutowatumia polisi katika hali iliyoleta taswira tofauti kwa wapiga kura kwa kuingiwa na hofu ya kukamatwa na hata kutopiga kura kabisa.
  Hata hivyo timu hiyo ilisema kuwa kuna baadhi ya wapiga kura ambao walikuwa wakiunga mkono harakati za wagombea wa upinzani walifanyiwa hila na kuondolewa katika orodha ya wapiga kura bila kuwa na sababu za kuondolewa kwao katika orodha hiyo.
  Kiongozi huyo wa timu ya waangalizi alisema umefika wakati kuwa ni kupunguza muda wa kufanya kampeni kwa kipindi kirefu ili kwenda sambamba na bajeti za vyama vya siasa kuliko ilivyo sasa ambapo chama tawala pekee ndicho chenye uwezo wa kuyafikia maeneo mengi kutokana na kuwa na rasilimali za kutosha.
   
 2. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #2
  Feb 12, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,789
  Likes Received: 416,595
  Trophy Points: 280
  Serikali sikivu ingelikuwa tayari imekwisha kuandaa miswada ya kufuta NEC, na kubadilisha sheria zote za uchaguzi kandamizi bila ya uhaja hata wa kusubiri Katiba mpya mchakato utakaochukua muda mrefu...............................

  uundaji wa NEC mpya ni lazima utoe fursa sawa kwa watanzania wote kuziomba nafasi zote ndani ya Tume hiyo kwa kuzitangaza magazetini na asiwepo mtu ambaye anafanya uteuzi wake kimya kimya tu........................................

  Vile vile watendaji wa serikali za mitaa waondolewe moja kwa moja katika kusimamia chaguzi zote.........................na NEC iwe na watendaji wake wa kudumu ambao wanawajibika moja kwa moja kwake na huku NEC ikiwajibika moja kwa moja Bungeni.................haya marekebisho hayahitaji kusubiri Katiba Mpya kama wanasiasa ndani ya CCM wanavyotaka kuendelea kuongoza nchi hii bila ya ridhaa ya nguvu ya umma....................................................
   
 3. Mvaa Tai

  Mvaa Tai JF-Expert Member

  #3
  Feb 12, 2011
  Joined: Aug 11, 2009
  Messages: 6,174
  Likes Received: 2,175
  Trophy Points: 280
  Ufumbuzi wa hili ni Kuunda katiba mpya itakayopelekea tume huru ya uchaguzi, ambapo itakuwa vigumu sana tume kututeulia Rais mwenye madaraka makubwa kiasi hiki. Inauma sana Rais hukumchagua na kuna mazingira kwamba hakushinda anaingia madarakani bila matakwa yako na anakuletea mrembo fulani awe boss wako kama mkuu wa wilaya. Mungu aepushie mbali katiba mpya ipatikane kwa njia ya amani tuu maana kuna kila dalili ya nguvu ya umma kutumika.:A S 20:
   
 4. makoye2009

  makoye2009 JF-Expert Member

  #4
  Feb 12, 2011
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,646
  Likes Received: 500
  Trophy Points: 280
  Juzi wakti Waziri katika Ofisi ya Waziri Mkuu Wiiliam Lukuvi akijibu swali kuhusiana na Uchaguzi wa 2010 alijigamba na KUSEMA KUWA HATA WAANGALIZI WA KIMATAIFA WALISEMA UCHAGUZI ULIKUWA HURU NA HAKI!Akaendelea kupiga vijembe kuwa Uchaguzi umekwisha na WAPINZANI waweke ILANI ZAO KABATINI ZISUBIRI 2015!!! Kumbe MARTIN hapa KAGUNDUA KULIKUWA NA KASORO ZAIDI YA 30!!!!!!!!!!!!

  Lukuvi Pambaf kabisa. Sasa tunakwambia hivi KWA SASA HATUNGOJI TENA UCHAGUZI WA 2015 TUNATAKA PEOPLES POWER. Shhhhhhhheeenzzzzzzzzzi kabsa.
   
 5. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #5
  Feb 12, 2011
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  Kama Kweli Lukuvi kasema hivyo basi kwa sasa ninajua kwa nini wanahofia wapinzani kuendesha shughuli zao kwa mikutano na maandamano, maana ni kuwazindua watanzania na hilo ndilo CCM wanaliogopa. Wanataka kuvifanya vyama vya upinzani kuwa vya uchaguzi tu baada ya uchaguzi vitulie kimya kuwaacha wao waendelee na propaganda za kuwarubuni watanzania ili 2015 wawachague tena.

  CDM na upinzani hii miaka mitano ni moto chini kueneza elimu ya uraia na kuwapa wananchi taarifa sahihi jinsi CCM inavyowa-screw na kuwadunisha. Matatizo yote ya watanzania yanatokana na utawala mbovu na wa kibinafsi wa viongozi wa CCM na serikali yake. Tunataka 2015 iwe mwisho wa CCM na kama watang'ang'ania kwa nguvu bora watawale miti na wanyama ila tutahitaji haki itendeke katika kupata viongozi na si mapinduzi ya kipolisi na jeshi kama wanavyotumia kila uchaguzi mkuu. Hawa wote kina Lukuvi wanajua wazi kuwa hawana qualifications zozote za kuwapatia kazi kwenye sector binafsi baada ya kuondolewa katika utawala na hawa ndiyo adui namba moja wa amani na utulivu wetu. Kwao wao ni bora Tanzania iangamie kuliko wao kutokuwa watawala hata kama wananchi hatuwataki.

  Ningekuwa ni strategist wa CCM kwa sasa ningesema tuache porojo miaka hii mitano tu-focus kwa wananchi na ikibidi hata sisi tusilipwe ila tuhakikishe wananchi wanakuwa na mazingira mazuri ya ajira na kushuka kwa ugumu wa maisha, anything more than that ni kupoteza muda kwani watanzania si mabwege tena.
   
 6. Ngalikivembu

  Ngalikivembu JF-Expert Member

  #6
  Feb 14, 2011
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 1,908
  Likes Received: 355
  Trophy Points: 180
  Hakuna comment ni katiba tu.
   
 7. tzjamani

  tzjamani JF-Expert Member

  #7
  Feb 14, 2011
  Joined: Oct 9, 2010
  Messages: 997
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Sikio la kufa halisikii dawa....ccm imeshakufa. Kama mwanzilishi wake Mwl. Nyerere (RIP) aiipigia kelele haikusikia... na anaweza kuiamsha ccm ikafufuka tena?

  Lazima ionje kuwa chama cha upinzani ili isambaritike kwanza....

  Katiba mpya ndio jibu kama hawataki nguvu ya umma iko around the corner.
   
 8. MAMMAMIA

  MAMMAMIA JF-Expert Member

  #8
  Feb 14, 2011
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 3,822
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0
  Kwa sasa ufumbuzi kwa njia ya amani ni katiba mpya, lakini CCM waelewe kuwa ziko njia nyengine za kudai haki za Watanzania. .
   
Loading...