Waangalizi 92 kutoka nje kushuhudia uchaguzi mkuu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Waangalizi 92 kutoka nje kushuhudia uchaguzi mkuu

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by MziziMkavu, Oct 9, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Oct 9, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,617
  Trophy Points: 280
  Fredy Azzah na Jackline Laizer
  IKIWA zimebaki siku 23 kabla ya kufanyika kwa uchaguzi mkuu, waangalizi 92 kutoka nje, wakiwemo 68 kutoka Umoja wa Ulaya (EU), wameanza kuwasili nchini.

  Kwa mujibu wa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe waangalizi waangalizi wengine 24 wanatoka Umoja wa Afrika (AU).

  Membe alisema waangalizi kutoka Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) na Jumuiya ya Masoko ya pamoja ya Mashariki na Kusini mwa Afrika (Comesa), wamealikwa kushuhudia uchaguzi huu ingawa bado hawajathibisha siku ya kuwasili nchini.

  Akizungumza na waandishi wa habari jana, Membe alisema kuwa waaangalizi wa EU ambao baadhi yao wameshawasili nchini, wanaweza kuanza shughuli zao leo, baada ya kusaini mkataba wa makubaliano jana.
  “Ni imani yetu kuwa mtafuata sheria za kimataifa na kitaifa zinazohusu uangalizi wa uchaguzi,” Membe aliwaeleza wawakilishi wa EU waliofika ofisini kwake kutia saini mkataba huo.

  Aliwataka kutoingilia kwa namna yoyote shughuli za kampeni, na kuwa wanachotakiwa kufanya ni kuorodhesha mambo wanayoyaona na kisha kuja kuyaeleza katika ripoti yao baada ya kufanyika kwa uchaguzi.

  “(Tume ya Taifa ya Uchaguzi) NEC na (Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar) ZEC ndiyo wasimamizi wa shughuli za kampeni na uchaguzi na hivyo ndio wanaohusika kushughulikia malalamiko yote endapo yatatokea,” alisema Membe.

  “Kama waangalizi wataona jambo fulani linafanyika, hawataruhusiwa kulizungumza mpaka baada ya uchaguzi mkuu kumalizika ndipo watakapochagua kiongozi wao atakayewasilisha ripoti pamoja na maoni yao juu ya kile walichokiona wakati wa kampeni na uchaguzi.”

  Balozi wa EU nchini, Tim Clarke alisema timu yake pamoja na watu wengine pia inajumuisha wanasiasa mbalimbali walioteuliwa na Bunge la EU.

  Alisema baadhi ya watu wanaounda timu ya EU waliowasili nchini mpaka sasa ni pamoja na wataalam wa siasa, vyombo vya habari pamoja na watu wa Itifaki, ambao wataangalia mwenendo wa kampeni.


  Chanzo: Gazeti la Mwananchi
   
 2. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #2
  Oct 9, 2010
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Hawa hawatasaidia kitu. Kuangalia mchakoto wa kupiga kura si pamoja na kuangalia mchakato wa kuhesabu kura. Stalin aliwahi kusema kuwa wanaopiga kura si waamuzi. Wanaoamua ni wale wanaohesabu kura.
   
Loading...