Waandishi wengi wa habari Tanzania hawajui Kingereza hata cha kuokoteza? Why?

Tabutupu

JF-Expert Member
Nov 26, 2010
13,107
18,323
Mwandishi yeyote wa habari jambo kubwa analo takiwa kulijua ni lugha na sio moja.

Sasa Tanzania kuna tatizo gani kwa waandishi wengi wa habari kuto jua kingereza?

Alikuja Rais Obama, wakashindwa kuuliza maswali kwa sababu ya ung'eng'e.

Tumeona pia baadhi ya wageni wakija waandishi wa habari wananikanyaga balaa utadhani wote waliishia darasa la pili?

Tatizo wapi? Mfumo wa elimu au nini?

Wizara ya habari na vyuo hili linawahusu.

1608850133341.jpeg
 
Mwandishi yeyote wa habari jambo kubwa analo takiwa kulijua ni lugha na sio moja...
Mi nadhani mfumo wetu was elimu ndio unatutengeneza hivyo,kingereza chetu Ni Cha kusoma sio Cha kuongea.Mkazo mkubwa kwa wanafunzi ni kufaulu mtihani. Hata hizi za English medium ukienda shule ukasikia kingereza Cha walimu was kitanzania unabaki unajiuliza maswali mengi.

Lazima tukiri tuna tatizo.
 
Tofauti kabisa na mada iliyowasilishwa.

Kiingereza (lugha) sio taaluma ya habari.

Kama mwandishi anajua vyema taaluma yake ya habari, haijalishi ni lugha gani anayoitumia kuwasilisha kwa ufasaha anayoyawasilisha.

Kwa hiyo, mwandishi wa habari aliyeiva vizuri katika tasnia hiyo ya uandishi wa habari, tuseme kwa kutumia lugha ya kiswahili; kazi zake katika lugha hiyo zitakuwa nzuri kabisa.

Mwandishi huyo huyo, aliye mjuzi na kazi yake, lakini anajua kiingereza cha kujiumauma, bado anaweza kuwasilisha kazi yake hiyo vizuri na watu wakaielewa vyema, hata kama lugha ya kiingereza haikunyooka sana.

Tatizo la waandishi wa habari wa Tanzania (na kwa kweli sio waandishi wa habari pekee, bali hata nyanja nyingi nyingine), tatizo kubwa ni taaluma (elimu) zao zaidi kuliko lugha.

Elimu yetu inahitaji jitihada zaidi kuwaandaa watu wanaojua wanachojifunza katika lugha yoyote wanayotumia kujifunza.
 
usiwalaumu hao waandishi wa habari kutokujua ung'eng'e, umewahi kumsikia rais wao wa nchi akiongea hicho kingreza?!.
Raisi wa China, Urusi, waziri mkuu wa Japan hawaongei lugha ya malikia lakini raia wao wengi wanaongea lugha ya malikia,wakati mwingine muwe mnafikiria kabla ya kutoa maoni, si lazima utoe utumbo wako kwenye jambo usilolijua.
 
Upo sahihi na tutaishia kuajiri wageni kwenye issue zote za lygha ya kingereza .. hata Capital TV wanapata shida sana kuwa pata waandishi wazuri.
Mi nadhani mfumo wetu was elimu ndio unatutengeneza hivyo,kingereza chetu Ni Cha kusoma sio Cha kuongea.Mkazo mkubwa kwa wanafunzi Ni kufaulu mtihani.Hata hizi za English medium ukienda shule ukasikia kingereza Cha walimu was kitanzania unabaki unajiuliza maswali mengi.
Lazima tukiri tuna tatizo.
 
Back
Top Bottom