Waandishi wapotoshaji

Yona F. Maro

R I P
Nov 2, 2006
4,202
218
Mimi sio mpenzi wa kusoma magazeti, ni mtu ninayependa kuangalia vichwa vya habari tu kisha huyo naacha sisomi tena, kama kusoma basi kuna waandishi ambao nimejijengea mazoea ya kusoma maoni na habari zao. Tazama www.jikomboe.com. Huyu ni Ndesanjo Macha na kama uko Tanzania, makala zake unazipata katika gazeti la Mwananchi Jumapili kila wiki. Mfano, wiki hii sikuona makala yake, sijui nini kinaendelea.

Unaweza kujiuliza kwanini napenda Macha na yeye ndio nimechukulia mfano wake? Ni kwa sababu habari na maoni yake yanachambulika na kutambulika. Yaani, siku ya Jumapili ikifika ukifungua Mwananchi, unakuwa unahisi leo Macha anaandika kuhusu siasa za Tanzania, teknologia za mawasiliano, au mambo mengine ya maisha. Anaeleweka, huwezi kukuta ameingilia fani ambayo sio yake. Mfano, kuandika mambo kuhusu mapenzi na mahusiano na udaku mwingine.

Kuna muandishi mwingine kama Dismas Lyasa, huyu anajulikana zamani alikuwa anaandikia Magazeti ya Udaku, sasa hivi amejiunga na Mwananchi. Pamoja na mimi kupenda magazeti ya Mwananchi, kuna mambo mengine lazima tuyakemee na kuyasema wazi kwamba hayapendezi na kuvutia. Wakati mwingine yanaweza kuchochea watu kwenda katika vyombo vya sheria kutafuta ukweli.

Sasa hivi ni zaidi ya miezi 2 toka nimesoma makala hiyo "UCHUMI WA TANZANIA UMELALA" makala hii iliandikwa na Dismas Lyasa, niliangalia kichwa cha habari nikaja kuangalia mwandishi nikawa na wasiwasi naye. Mbona huyu alikuwa anaandikia magazeti ya udaku, na muda mwingi anachangia katika mambo ya mapenzi na mahusiano, leo vipi amekuwa katika uchumi?

Nikasoma takwimu zilizoandikwa na bwana Dismas na kuchapishwa katika gazeti la Mwananchi wakati huo, kisha nikafungua tovuti ya Shirika la Fedha Duniani na Benki ya Dunia kwenda kuangalia takwimu hizo. Mambo yakawa ni tofauti sana. Takwimu zilizoandikwa na Dismas zilikuwa ni za uwongo hazina ukweli wowote.

Alichokosea zaidi hakuweka chanzo cha habari na hizo takwimu zenyewe lakini tukaziona katika gazeti. Nimefuatilia kuona nani atajibu makala ile, hakuna mpaka leo mtu aliyejibu makala ile. Kwahiyo inaonyesha makala imekubalika hata kama ilikuwa ya uzushi.

Tunatoa wito kwa wamiliki wa vyombo vya habari, haswa wahariri, waangalie sana na wawe makini na waandishi wao. Wengine haswa hawa wanaovamia fani ambazo sio zao. Wanapotoa habari au uchambuzi, basi wawaombe kutoa vyanzo vyake na kuandika hapo chini ya habari husika.

Wasipofanya hivi, basi ni kuangusha fani nzima ya uandishi na waandishi wenyewe. Sasa tunakuwa hatuwaamini waandishi na vyombo vyao haswa katika kuandika habari za uchumi na biashara. Au basi wawe na vitengo maalumu vya waandishi hawa.

Mfano, muandishi wa uchumi, tusimwone kesho anaandika udaku, au mapenzi na mahaba. Kweli hivi vitu haviendani. Tanzania ni kubwa ina watu zaidi ya milioni 30, mikoa zaidi ya 20, na mambo mengi sana. Naamini kuna mambo mengi sana ya kuandika mtu akiamua kutulia katika uchumi peke yake, au biashara peke yake, au udaku peke yake.
 
baada ya wewe kuangalia takwimu hizo na kukuta ni za uongo na za ukweli unazijua una wajibu kamna mwandishi (shy a freelance writer) kusahihisha hilo na kuhoji chanzo cha takwimu hizo. Kutumia hoja za mwandishi mmoja na kuamua kuhitimisha kuwa "waandishi wapotoshaji" hujitendei haki hata wewe mwenyewe kwani nawe ni mwandishi, unless unataka kusema waandishi "wengine" tu ndiyo "wapotoshaji" isipokuwa wewe.

Kama wote ni wapotoshaji, basi na mimi nakupotosha hapa na wewe ulichoandika ni upotoshaji na majibu yako ya upotoshaji wangu utakuwa ni upotoshaji mwingine.
 
waandishi wa habari waliowengi huwa wanapewa kidogo ili kupindisha mambo

angalia sakata la Lowasa kozomewa mbeya, ilivyoandikwa na magazeti yenyewe kuwa walipewa sh.10 000 za kitanzania ili wasiandike yaliyotokea. sisi tuliokuwepo, hata yaliyoandikwa hayafikii robo ya kitu kizima

ona kuzomewa kwa lowasa hukuhuku mbeya hawajaandika chochote. sijui tukiunga mkono ule mswada wa Bunge kuwa wakasome ingesaidia kujikomboa kimawazo, au ndiyo hivyo kuwa samaki mkunje angali mbichi.....
 
Back
Top Bottom