Waandishi wameandamana sawa,je tuishie hapo? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Waandishi wameandamana sawa,je tuishie hapo?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by security guard, Sep 12, 2012.

 1. s

  security guard JF-Expert Member

  #1
  Sep 12, 2012
  Joined: Sep 27, 2011
  Messages: 706
  Likes Received: 258
  Trophy Points: 80
  Jana waandishi wa habari kutoka katika vyombo mbalimbali nchini waliandamana kulaani kuuwawa kwa mwandishi wa habari wa Kituo cha Chanel 10 huko Iringa,kifo cha mwandishi huyu kwa bahati mbaya na kwa mara nyingine tena kimewagawa wananchi katika makundi yanayotofautiana kifikra kuhusu chanzo na hatimaye kufariki kwake,wapo wanao ona na kuamini polisi wametumia nguvu kubwa katika kukabiliana na tatizo lililokuwepo,wapo wanaoamini kwamba jeshi la polisi lilikuwa linatimiza wajibu wake na madhara haya makubwa yaliyotokea yanatokana na chama cha Chadema kuendeleza ghasia katika nchi na kujaribu kuifanya isitawalike kama walivyo ahidi baada ya kushindwa vibaya katika uchaguzi mkuu uliopita (walishinda viti 23 kati ya majimbo 239),lakini kabla ya kuingia katika tafakuri pana zaidi zinazotokana na msiba huu sina budi kutoa pole kwa familia ya Mwangosi,waandishi waliokuwa karibu naye katika kufanikisha majukumu yake ya uandishi wa habari,kituo cha channel 10 na watanzania wote kwa ujumla,kwa kuondokewa na mwananchi mwenzetu katika mazingira ambayo wote hatukuyategemea ,tumeshuhudia wakati taifa likiwa katika simanzi nzito kutokana na msiba huu, wapo wenzetu walioamua kuutumia kama turufu ya kuleta chuki baina ya jeshi la polisi na waandishi na zaidi uma wa watanzania ambao usalama waona mali zao unategemea sana uwepo wa jeshi hilo,kuna mambo mengi ambayo nimekuwa najiuliza na ningependa watanzania wote tujiulize ,hivi ghasia zilizopelekea msiba huu zilisababishwa na nini/nani?,je kulikuwa na ulazima kwa CHADEMA kukaidi amri ya polisi ya kusubiri sensa ipite?,je ukaidi wa chadema siyo chanzo cha maafa yaliyotokea na yanayotokea mara kwa mara nchini?,je ingekuwa sawa kwa jeshi la polisi kuwaachia chadema kufanya shughuli ambayo walikwisha wazuia wasiifanye?, je polisi ingewaachia kufanya jambo ambalo walikwisha wazuia kulifanya wangekuwa wanatimiza sheria na wajibu wao,na je uhalali wa uwepo wa jeshi hilo ungeendelea kuwepo?,wananchi wote tunapaswa kuheshimu sheria na polisi wana jukumu la kutulazimisha kufuata sheria tunapo zikiuka vikiwemo vyama vya siasa,najua sheria ya vyama vya siasa inavipa fursa vyama kufanya maandamano na mikutano baada ya kutoa taarifa polisi,lakini sheria hiyo hiyo inasema vitafanya hivyo endapo tu kama havitapata amri pingamizi kutoka polisi (sheria ya vyama vya siasa 1992 kifungu cha 11),tujiulize kulikuwa na ulazima gani kwa chadema ambao mwaka mzima wamekuwa waruhusiwa kufanya mikutano na maandamano kulazimisha kufanya mkutano uliopelekea kifo baada ya kupata amri pingamizi?kama waliona polisi hawakuwafanyia haki je ilikuwa vyema kuandaa mapambano dhidi ya polisi?je walichukua hatua yoyote ya kisheria dhidi ya polisi au hawana imani na vyombo vya kisheria kama ambavyo Tundu lisu anavyo ziponda mahakama zetu bila kuheshimu kwamba zilimpa ushindi yeye binafsi katika kesi yake ya uchaguzi aliyofunguliwa na mgombea wa CCM, na zile zilizokipa ushindi chama chake zilizowavua ubunge wana CCM huko Sumbawanga na Igunga,mimi naamini ili jeshi la polisi liweze kuendelea kulinda amani ndani ya nchi ni lazima tuliamini na lazima tujue kwamba lipo,likizuia jambo kwa mujibu wa sheria wote tuheshimu vinginevyo litakuwa halina sababu ya kuwepo,si mara moja au mbili mamlaka za uma na vyombo vya sheria viliamua mambo muhimu katika maendeleo ya taifa lakini yalipata upinzani hadi pale polisi ilipotumia nguvu kuhakikisha sheria inafuatwa na utekelezaji wake unatimia?je kumfukuza Waziri katika hafla ya kulaani mauaji na kumkaribisha mwanachadema Dr Lweitama kuhutubia na kuilaani serikali ni sawa?,je ni sawa kulilaumu jeshi zima la polisi kwa tatizo lililojitokeza sehemu moja ya nchi tena katika kutimiza wajibu wao?,kitendo cha kuto walaani walioanzisha uvunjaji wa sheria uliopelekea ndugu yetu Mwangosi kupoteza maisha katika umri mdogo kinaashiria nini kutoka katika taasisi zetu za habari? ,hapa ndiyo maswali mengine yasiyo na majibu yanapoanza,kwa nini tamko lililotolewa na CHADEMA na lile la wanahabari yanashabihiana,kwa nini wanahabari hawakuilaumu CHADEMA hata mara moja kwa kutokutii sheria na kuanzisha ghasia zilizopelekea maafa ya ndugu yetu ,nadhani tunahitaji tafakuri pana zaidi,je wametumwa?,wana hasira? au nao wameanza kushirikishwa katika ajenda za siri dhidi ya serikali na vyombo vyake?,wote tumesikitishwa na msiba huu sidhani kama ni vyema kuendelea kushambulia jeshi la polisi bali kuangalia nani ameanzisha sokomoko hili awajibishwe kisheria, kama ikibainika aliyeua ni raia wa kawaida sheria ichukue mkondo wake,lakini pia ikibainika muuaji ni askari akiwa katika kutimiza majukumu yake ni vyema taratibu za kijeshi pamoja na mahakama zake zitumike badala ya kuendeleza chuki zisizo na msingi,tusijisahau wote tunawahitaji polisi kama ambavyo tulikuwa tunamhitaji ndugu yetu Mwangosi nikiwemo mimi nilieshirikiana nae katika shughuli mbalimbali,tusiwe na Hasira maana wahenga walisema hasira hasara,tutafute suluhisho wa yanayotokea yasijirudie
   
 2. t

  thatha JF-Expert Member

  #2
  Sep 12, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  Yaa tuishie hapo, hadi atakapokufa Mwandishi mwingine tena.
   
Loading...