Kweli !! Yaani kweeeli kabisa !!!,yaani elimu yenu yote,ya kipolisi,mashaada yote mliyo nayo,Lissu jana amekamatwa mara ya nane (8) kuanzia June mwaka jana na hajawahi kupatikana na Hatia, Ubunifu ni Muhimu sana katika jambo lolote..
======
Dar es Salaam. Baadhi ya waandishi wa habari walioripoti mkutano wa Mwanasheria Mkuu wa Chadema, Tundu Lissu, uliofanyika Jumatatu ya wiki hii wamehojiwa na polisi.
Lissu ambaye pia ni Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika, (TLS) alifanya mkutano huo Jumatatu wiki hii ambapo pamoja na mambo mengine alilaani kukamatwa kwa wanachama wa Chadema.
Leo, Ijumaa, Julai 21, Mwandishi wa gazeti la Tanzania Daima, Ibrahim Yamola amehojiwa na watu waliojitambulisha kuwa ni polisi ambao walifika katika ofisi za gazeti hilo.
“Walitaka nifike Polisi Makao Makuu lakini tukakubaliana watakuja hapa ofisini kwetu asubuhi, wamekuja na wamenihoji kuhusu mkutano huo,” amesema.
Yamola amesema watu hao walimuhoji mazingira ya mkutano huo, maneno aliyoyatamka Lissu na namna walivyoichapisha habari hiyo siku ya pili.
Inaelezwa kuwa mwandishi mwingine wa gazeti la Mtanzania, Aziza Masoud naye anatarajia kuhojiwa baadaye leo.
Sent using Jamii Forums mobile app
Sitaki kuamini kama tumefika hapa,ivi raisi wetu anayajua haya? Au watendaji wake ndio hujiamulia kufanya haya? Nakama raisi wetu anayajua haya nikweli hajui umuhimu wa democrasia na uhuru wakujieleza?? Sitaki kuamini kama magufuri anaogopa kukosolewa
Sent using Jamii Forums mobile app
Duh! Biblia inasema usiabudu miungu mingine kumbe ilikuwa inamaanisha! Sikujua kama kuna miungu mingi kiasi hiki hapa duniani.Kosa lao kubwa ni kuvammia chumba cha mahakama kukiteka nyara na kukigeuza chumba cha press conference bila ridhaa ya mahakama
=========================================
Dar es Salaam. Baadhi ya waandishi wa habari walioripoti mkutano wa Mwanasheria Mkuu wa Chadema, Tundu Lissu, uliofanyika Jumatatu ya wiki hii wamehojiwa na polisi.
Lissu ambaye pia ni Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika, (TLS) alifanya mkutano huo Jumatatu wiki hii ambapo pamoja na mambo mengine alilaani kukamatwa kwa wanachama wa Chadema.
Leo, Ijumaa, Julai 21, Mwandishi wa gazeti la Tanzania Daima, Ibrahim Yamola amehojiwa na watu waliojitambulisha kuwa ni polisi ambao walifika katika ofisi za gazeti hilo.
“Walitaka nifike Polisi Makao Makuu lakini tukakubaliana watakuja hapa ofisini kwetu asubuhi, wamekuja na wamenihoji kuhusu mkutano huo,” amesema.
Yamola amesema watu hao walimuhoji mazingira ya mkutano huo, maneno aliyoyatamka Lissu na namna walivyoichapisha habari hiyo siku ya pili.
Inaelezwa kuwa mwandishi mwingine wa gazeti la Mtanzania, Aziza Masoud naye anatarajia kuhojiwa baadaye leo.
Katika mahojiano yale matusi na kejeli yanasomekaje?! Na nani huyo katukanwa?!Uhuru wa kujieleza unaruhusiwa lkn sio Uhuru wa kutukana kukejeli na kutoa maneno ya kuudhi dhidi ya raia na serikali yake lkn kuchochea wananchi waichukie serikali yao.
Sent using Jamii Forums mobile app
Nakupa 100% kwa hili,kwa bahati maya ninafahamu maisha(hearsay za jirani) kabla hajawa mkulu wa kaya.Kwakuwa nilimuamini dada mleta story ambaye alikuwa 'shost' wa huyu mama namba moko wa sasa, hakuna ninachoshangaa.Ni kama tu mkulu anapigia mstari majibu yangu.Believe it or not,the worse is yet come.kuna sababu kwa wagombea uongozi wapimwe akili kwanza na kuchunguzwa juu ya mahusiano yao ndani ya familia zao..
kiongozi bora huanza kwenye familia yake..
Sent using Jamii Forums mobile app
Mwelezee huyu pimbi kazi yao kukurupuka tu kama lichama lao la makinikia likiongozwa m/kiti wao.(chama cha mambumbumbu).aka ma~fa~fa~fa.Umeambiwa Mkutano ule alioufanya mpaka mkakosa usingizi Lumumba wote.
Waandishi wa Uhuru,Habari Leo,Tazama na Watangazaji wa TBC,Uhuru FM.Awamu ngumu sana hii!!
Sijui nani atabaki salama
Jidanganye tu hizi hizi kelele ndo zinazidi kuwakosesha raha halafu mbaya zaidi wanazidi kuboronga hakuna watu wanaozaliwa na ujasiri tu wa kupinga utawala... dhuluma na uonevu wa wazi ukizidi hadi mbuzi wanaweza kuwa simba...Mmebaki kupiga kelele mtandaoni. Mnampa kichwa huyo Lisu halafu akiswekwa selo hata uji tu hamumpelekei.