Waandishi Walioripoti mkutano wa Lissu wahojiwa na Vyombo vya Dola!

Wapuuzo tuu ujue kukaa kimya hakumaanishi kwamba sisi ni wajinga

Mtu anapoambiwa ukweli sharti ajirekebishe
Kuna mtu katukana juzi wapunbavu na marofa uuko kitaa amuoni kuna mis treatment iv mnafikir ao walinzi wanaweza kuwazuia msidhulike
Tenden haki kwa afya ya maisha yenu
 
Afu huwa mnajifanyaga hamnazo. TL ana jeshi? Mbina akitokaga rumande wote humu mnakimbia? Ile namba ingine kwa hoja.

Ccmscrow mnaongoza kwa vioja na mabavu. Na kununua mikweche ya ndege
Mmebaki kupiga kelele mtandaoni. Mnampa kichwa huyo Lisu halafu akiswekwa selo hata uji tu hamumpelekei.
 
Safi sana viherehere vitawaisha waangalie gazeti uhuru na mzalendo ni magazeti bora kabisa africa
 
Huyu jamaa sio wa nchi hii watanzania hawapo hivi...atakua na nasaba za kutoka nchi jirani tu...
 
Sitaki kuamini kama tumefika hapa,ivi raisi wetu anayajua haya? Au watendaji wake ndio hujiamulia kufanya haya? Nakama raisi wetu anayajua haya nikweli hajui umuhimu wa democrasia na uhuru wakujieleza?? Sitaki kuamini kama magufuri anaogopa kukosolewa

Sent using Jamii Forums mobile app
Wewe unasema Rais analijua hilo, wakati hayo mambo ni yeye ndiye anayeyaagiza?
 
Eti polisi wakawahoji Lissu alisema nini.

Wangewaonyesha video iko Youtube!
 
004520c70ff6281fb1b1722a50dd836c.jpg
Lissu jana amekamatwa mara ya nane (8) kuanzia June mwaka jana na hajawahi kupatikana na Hatia, Ubunifu ni Muhimu sana katika jambo lolote..

======

Dar es Salaam. Baadhi ya waandishi wa habari walioripoti mkutano wa Mwanasheria Mkuu wa Chadema, Tundu Lissu, uliofanyika Jumatatu ya wiki hii wamehojiwa na polisi.

Lissu ambaye pia ni Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika, (TLS) alifanya mkutano huo Jumatatu wiki hii ambapo pamoja na mambo mengine alilaani kukamatwa kwa wanachama wa Chadema.

Leo, Ijumaa, Julai 21, Mwandishi wa gazeti la Tanzania Daima, Ibrahim Yamola amehojiwa na watu waliojitambulisha kuwa ni polisi ambao walifika katika ofisi za gazeti hilo.

“Walitaka nifike Polisi Makao Makuu lakini tukakubaliana watakuja hapa ofisini kwetu asubuhi, wamekuja na wamenihoji kuhusu mkutano huo,” amesema.

Yamola amesema watu hao walimuhoji mazingira ya mkutano huo, maneno aliyoyatamka Lissu na namna walivyoichapisha habari hiyo siku ya pili.

Inaelezwa kuwa mwandishi mwingine wa gazeti la Mtanzania, Aziza Masoud naye anatarajia kuhojiwa baadaye leo.

Sent using Jamii Forums mobile app


Serikali ya awamu ya tano itapelekea nchi kwenye vurugu.
 
Back
Top Bottom