Waandishi Walioripoti mkutano wa Lissu wahojiwa na Vyombo vya Dola!

Pozzers

JF-Expert Member
Sep 14, 2013
336
560
004520c70ff6281fb1b1722a50dd836c.jpg
Lissu jana amekamatwa mara ya nane (8) kuanzia June mwaka jana na hajawahi kupatikana na Hatia, Ubunifu ni Muhimu sana katika jambo lolote..

======

Dar es Salaam. Baadhi ya waandishi wa habari walioripoti mkutano wa Mwanasheria Mkuu wa Chadema, Tundu Lissu, uliofanyika Jumatatu ya wiki hii wamehojiwa na polisi.

Lissu ambaye pia ni Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika, (TLS) alifanya mkutano huo Jumatatu wiki hii ambapo pamoja na mambo mengine alilaani kukamatwa kwa wanachama wa Chadema.

Leo, Ijumaa, Julai 21, Mwandishi wa gazeti la Tanzania Daima, Ibrahim Yamola amehojiwa na watu waliojitambulisha kuwa ni polisi ambao walifika katika ofisi za gazeti hilo.

“Walitaka nifike Polisi Makao Makuu lakini tukakubaliana watakuja hapa ofisini kwetu asubuhi, wamekuja na wamenihoji kuhusu mkutano huo,” amesema.

Yamola amesema watu hao walimuhoji mazingira ya mkutano huo, maneno aliyoyatamka Lissu na namna walivyoichapisha habari hiyo siku ya pili.

Inaelezwa kuwa mwandishi mwingine wa gazeti la Mtanzania, Aziza Masoud naye anatarajia kuhojiwa baadaye leo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
=========================================

Akiwamaliza wapinzani watakao fwatia ni vyombo vya habari. Akivimaliza vyombo vya habari watafwata viongozi wa dini na mwisho atamalizana na wananchi wa kawaida.
Ole wangu Mimi alipokua anawamaliza wenzangu nilikaa kimya na wala sikupiga kelele sasa ni zamu yangu nani wa kunililia?
 
Sitaki kuamini kama tumefika hapa,ivi raisi wetu anayajua haya? Au watendaji wake ndio hujiamulia kufanya haya? Nakama raisi wetu anayajua haya nikweli hajui umuhimu wa democrasia na uhuru wakujieleza?? Sitaki kuamini kama magufuri anaogopa kukosolewa

Sent using Jamii Forums mobile app
Ukisikia wanasema tunatekeleza amri toka juu usijiulize maswali aina hiyo
 
Sitaki kuamini kama tumefika hapa,ivi raisi wetu anayajua haya? Au watendaji wake ndio hujiamulia kufanya haya? Nakama raisi wetu anayajua haya nikweli hajui umuhimu wa democrasia na uhuru wakujieleza?? Sitaki kuamini kama magufuri anaogopa kukosolewa

Sent using Jamii Forums mobile app

Kosa lao kubwa ni kuvammia chumba cha mahakama kukiteka nyara na kukigeuza chumba cha press conference bila ridhaa ya mahakama
 
Back
Top Bottom