TAECOLTD
JF-Expert Member
- Mar 2, 2013
- 1,051
- 1,835
Habari za muda huu, napenda kutumia wasaa huu kuwakutanisha Waandishi wa vitabu, story za movie na tamthiliya. Binafsi ni mwandishi wa vitabu mchanganyiko vya biashara na stori fupi fupi na ndefu, changamoto kubwa ambayo nimekumbana nayo ni masoko. Tanzania bado watu hawana muamko wa kusoma vitabu hivyo inakuwa ngumu kidogo kuyapata masoko husika. Utapeli ni aina nyingine ya changamoto ambapo mwaka 2012 nilipoingia rasmi kwenye ulimwengu wa uandishi nilitapeliwa kazi zangu mbili moja na kampuni moja ya uchapaji hapa Dar na nyingine na msanii wa filamu aliniingiza choo cha kike na kwakuwa sikuwa nimezisajili ilikuwa ngumu kupata haki yangu. Wewe mwandishi mwenzangu share nasi mambo mbalimbali ambayo yataweza kupeleka kazi hii ya uandishi wa vitabu na story mbele na kuleta mafanikio kwa Waandishi wanaochipukia waweze kunufaika na kazi zao...Asanteni na kazi njema