Waandishi wa vitabu tanzania wako wapi?

wasanii wa utunzi wa vitabu wapo ila jamii ya sasa imesahau kwa makusudi kabisa ama kutojua umuhimu wa kusoma vitabu..binafsi nimekua msomaji mwandamizi msaidizi wa vitabu hususani vya riwaya na vingine fikirishi vilivyonisaidia kwa namna moja ama nyingine kujenga uelewa wa mambo mengi madogo kwa makubwa..
Kuna Mwandishi kasahaulika angali hai ambaye ni masalia ya kina Eddie Ganzel,huyu ni Beka Mfaume ambaye nilimjua kwa mara ya kwanza kwenye kitabu chake alichokipa jina la Mwiba. Ni kitabu chenye mafundisho ambacho japo kimeandikwa kwa mfumo wa kisa cha mapenzi ila hata amaye hakupata kuingia kwenye mapenzi atapata funzo..ni kitabu kizuri kukisoma..baada ya kusoma kitabu hiki nilimtafuta mzee Beka,akanipatia nakala ya kitabu chake kipya kilichopo sokoni tittled Mhanga wa Ikulu....hivyo nadhani ni kupoteza morari wa usomaji kwa sababu ya sanaa za maigizo zilizochukua kasi miaka ya karibuni..
Ni vyema serikali kupitia Taasisi na asasi za utamaduni kuweka mfumo ambao utawavutia vijana/watoto kukua wakijua Watunzi na kazi zao ili kuwakuza kifikra,na kuotesha miyoni mwao ari ya kufikia mafanikio km waliyopata kufikia watunzi wetu adhimu!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom