Waandishi wa vitabu tanzania wako wapi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Waandishi wa vitabu tanzania wako wapi?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Bujibuji, Jan 19, 2010.

 1. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #1
  Jan 19, 2010
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,292
  Likes Received: 22,068
  Trophy Points: 280
  ZAMANI TULIKUWA TUNA WAANDISHI MAHIRI WA VITABU VYA KUSISIMUA.
  WALIKUWEPO KINA BEN R MTOBWA, MSIBA, NA WENGINE WENGI.
  KWA MARA YA MWISHO KUSOMA KITABU CHENYE KUSISIMUA ILIKUWA MIAKA MITATU NYUMA,
  NLIBAHATIKA KUSOMA KITABU CHA SEITH CHACHAGE KINACHOITWA MAKUWADI WA SOKO HURIA. KILA UKURASA ULIKUWA NA MSISIMKO WAKE WA KIPEKEE SANA.

  SIKU HIZI HAMNA TENA WALE WAANDISHI WETU MAHIRI.
  KAKA SHIGONGO ANAANDIKA HADITHI AMBAZO HAZI KABISA UHALISIA NDANI YAKE.
  HEBU CHEKI KITUKO KAMA HIKI.
  Baada ya kuzoea maisha ya Gamboshi akiwa ameshakatwa ulimi na kupumbazwa, Richard alianza kufanya kazi katika gazeti la kichawi lililoitwa Gamboshi Times. Gazeti hilo lilikuwa likiandika habari za kichawi na kusambazwa Gamboshi zima kwa ajili ya kusomwa na misukule iliyokuwa ikiishi huko.
  KWELI HUWEZI KUPATA MSISISMKO KWENYE AINA HII YA HADITHI,
  NIMECHOKA MIE.
   
 2. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #2
  Jan 19, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  ni kweli Bujibuji hadithi za kina Ben R. Mtobwa na bwana Msiba zilikuwa na msisimko na mvuto wa ajabu
  walitwandikia ,Salam Toka kuzimu ,Tumerudi na Roho zetu Malaika wa shetani ,na nyinginezo nyingi nzuri zisizo na mfano
  wako wapi wengine???ndo kusema TZ hatuna waandishi wa hadithi tena ??

  hizi za bwana shigongo sijui anazitoa wapi zina uongo mwingi na hazileti uhalisia na jamii hii tunayoishi
   
 3. D

  Darwin JF-Expert Member

  #3
  Jan 19, 2010
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 908
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Subirini kitabu cha Bluray disc kikiisha.
  Kwaninavyomjua kitakua cha msisimko
  .
   
 4. elimumali

  elimumali Senior Member

  #4
  Jan 19, 2010
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 149
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Wapo! ila wanakatishwa tamaa na faida ndogo inayopatikana. Pamoja na kwamba lengo la uandishi ni kuielimisha jamii, lakini pia kipato ni muhimu kwa mwandishi ili kumpa motisha. Kuna mwanandishi ninayemjua ameandika tamthilia nzuri, zimesomwa mashuleni na kutumiwa katika mitihani i.e. HIBA YA WIVU, KIU YA HAKI nk. lakini vikawa vinaibiwa na wajanja na kuchapishwa mitaani na kuuzwa kwa bei ya kutupa. Faida ikawa hapati. Watu hawa wanahitaji motisha ili waendelee kuandika! Tuwasaidieje?
   
 5. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #5
  Jan 19, 2010
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  Kuna huyu mtu anaitwa Emannuel Makaidi, alikuwa anakitabu chake kinaitwa Baada ya Kisa Mkasa, ukikisoma hiki utashikwa na hasira mbaya. kulikuwa na akina Hammie Rajab, Agoro Anduru na kile kitabu chake cha kiingereza, Eddy Ganzel, Kajubi D Mukajanga na yeye alikuwa mtunzi mzuri tuu. Wengine nimewasahau nilikuwa nasoma sana hivi vitabu.
   
 6. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #6
  Jan 19, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  Ngoja tusubiri maana wengine ugonjwa wetu ni hadithi (Novels)
   
 7. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #7
  Jan 19, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  mwandishi wa hiki kitabu hakika alikuwa na akili na alifikiria vyema sana hongera zake
  kitabu ni kizuri sana sana
   
 8. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #8
  Jan 19, 2010
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,292
  Likes Received: 22,068
  Trophy Points: 280
  Je serikali yetu inayalindaje maslahi ya waandishi hawa?
  Basata na lile li shirika lingine la copy right yamekufa.

   
 9. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #9
  Jan 19, 2010
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,316
  Likes Received: 1,785
  Trophy Points: 280
  Kama kila mtu akifanya kazi kwa approach hiyo hakuna litakaloweza kufanyika. Mambo mengi yanapita. Hili la industry yao kutolipa ni suala la muda tu maana hatujui kesho changes zitaleta nini kutoka kwenye hazina yake isiyokwisha. It would be wrong to throw away the whole future just because today the industry looks unprofitable.
  Mimi nilipojiunga na chuo niliambiwa course niliyokuwa nasomea haina market na nitahangaika sana kupata ajira.Tuliosoma ile kozi tulikuwa kama 25. Guess what? Baadae tulikuwa tunatafutwa mko wapi maana opportunities zilikuwa nyingi watu hakuna.
  Ni dhambi kukata tamaa na mambo haya yanayopita!
   
 10. N

  Natasha Ismail JF-Expert Member

  #10
  Jan 19, 2010
  Joined: Jul 14, 2008
  Messages: 511
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 60
  KABWE MAKANIKA NI JITU KUMBUKA KATIKA VITA DHIDI YA MAFIA MOB.By Zahir Zorro(baba banana)
   
 11. akashube

  akashube JF-Expert Member

  #11
  Jan 19, 2010
  Joined: Dec 24, 2009
  Messages: 411
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  Mi siku hizi nasoma hizi za live live hapa JF. Naona ni tamu zaidi
   
 12. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #12
  Jan 19, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  za live live ndo zipi tena ?

  Mzee mwanakijiji nae huwa anaachia ma hadithi ya mahaba huko kwenye web zake siku hizi sijui hadithi amemaliza au amekuwa busy na kuacha kutunga?
   
 13. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #13
  Jan 19, 2010
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,220
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  hujajishughulisha kuvitafuta hivyo vitabu unavyotaka wewe uvisome ambavyo vina msisimko. tatizo jingine ni kuwa hawa wachapishaji wetu ni WABABAISHAJI sana! mikataba yao mibovu mno! asilimia 10 kwa kila kopi itakayouzwa mwandishi utafaidika na nini? wakati huo huo hawakitangazi kitabu cha mwandishi inavyopasa. mbaya zaidi wanamwambia mwandishi atafute masoko wakati tayari mlishaingia mkataba na jukumu la kuuza na kutangaza ni lao. stupidity of the highest order. nasema hivi kwa vile mimi pia ni mwandishi. baada ya kutoa kitabu changu kimoja na cha kwanza kiitwacho Adha ya Heri nilihisi nimepoteza muda wangu asilimia 90. kinapatikana TUKI tu hapo UDSM. nimeona sasa nifikirie mpango wa kuanzisha kampuni niingie kwenye tasnia ya filamu. uwezo wa kujenga mawazo ninao. kwa mtakaopenda kutafuta hiyo kopi ya Adha ya Heri mtajionea mtiririko mzuri wa kupendeza na uhalisia wa maisha ujana na kakara zake. wala si kama nakitangaza ila nataka niwaambie tu kuwa mawazo na simulizi za kusisimua bado zipo na wala si zile za kufikirika. ni hayo tu
   
 14. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #14
  Jan 19, 2010
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 0
  jamani kuna mkahawa wa vitabu uko mtaa wa mlingotini pale morocco kuna vitabu vingi sana maktaba na sehemu ya wazi ya kufanya majadiliano na mambo mengine kama hayo kwahiyo kazi ni kwenu kama mnataka vitabu au nyingi ni waandishi wa vitabu munaweza kupeleka vitabu vyenu pale
   
 15. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #15
  Jan 19, 2010
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,292
  Likes Received: 22,068
  Trophy Points: 280
  thanx mpwa tutaenda huko kusoma vitabu vya zamani,
  lakini kuna haja ya kizazi hiki kuwa na wakali wa maandishi.
   
 16. elimumali

  elimumali Senior Member

  #16
  Jan 19, 2010
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 149
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Nakubaliana nawe. Kitabu chake kingine - 'WIVU WA MUMEO' nilikisoma kikaniacha hoi. Tamthilia hizi zikiwekwa katika movie zitasisimua wengi na kuelimisha kwa kiwango kikubwa. Kuna mbinu za kuwapa moyo hawa wachangiaji wa burudani na elimu kwa njia ya uandishi. Wawe wanapelekwa japo nje kujifunza zaidi toka kwa wenzao, kukuza upeo wao wa uandishi. Hii pia ni Motisha!

  In life, we seldom find a TRUE person & if you ever find one, hold on and never let go, value that person co'z its lyfs gifts worth keepin n holdin on.. Take Care!!
   
 17. b

  bakarikazinja Senior Member

  #17
  Jan 19, 2010
  Joined: Nov 9, 2009
  Messages: 179
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Na dhani kuna kisa kimoja ambacho nikikitoa mnaweza mkajua ni kwa sababu gani hawa waandishi wanavyo pata tabu na kukata tamaa kabisa kujikita katika ulimwengu wa fasihii na kuwachia makasuku kama wa kina shigongo kuendelea kuipotosha jamii na ukasuku wao wa kuandika vitu visivyo kuwa na uhalisia ktk jamii usika .
  nilikuwa na rafiki ambaye tulisoma naye katika chuo kikuu cha udsm tulipo kuwa mwaka wa pili tuli opti nadhani kwa wale wenzangu nikisema ku opti mnafahahamu kozi ya uwaandishi wa vitabu tulisoma kozi ile mpaka tukamaliza tulipofika mtaani mwenzangu akajikita kwenye kazi za uhandishi akijua kwamba ninjia mojawapo ya kuelimisha jamii na kujipipatia kipato cha muda wake mwingi alio upoteza kutokana na kukaa chini kutunga kazi yake ambayo ni ngumu na wakati mwingine kushindwa kufanya mambo yake mengine binafsi.
  Basi alifanikisha kutunga kitabu kizuri ambacho kilikuwa na ujumbe muhimu sana ktk jamii yetu hususani hii inayo kabiliwa na janga kubwa la mauaji ya abino basi akatafuta wadhamini asipate, ktk maongezi na watu wa kamshauri aende ktk shirika fulani atapata mdhamini basi akaenda mpaka huko akakutana na mkurugenzi wa pale wa kazungumza na kufikia muafaka aiache kazi yake pale ili waipitie na siku inayofuatia kuifuata basi kwakuwa kijana anaitaji msaada akaaacha kazi yake bila kujua kwamba ametapeliwa siku iliyo fuata alipokwenda yule boss akamwambia nilikuwa busy ivyo njoo kesho nita kupatia kazi yako ikawa kesho mwishowe akamwambia imepotea awajaandikishiana popote pale je nini hatima ya huyu kijana ?je hatakuwa nahamu ya kuandika kazi nyingine tena?basi hilo ndio swali la kujiuliza katika maisha.
   
 18. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #18
  Jan 19, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  yap pia kweli hawa wasanii wajaribu kutafuta vitabu vya kibongo vinahadithi nzuri sana zenye maadili watoe movie kwa kupitia hadithi hizo kuliko kwenda ku-copy na kupaste movie za Nigeria
   
 19. D

  Darwin JF-Expert Member

  #19
  Jan 19, 2010
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 908
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35

  Duh!

  Kwa uandishi wako itachukua muda sana kama wataka kuandika kitabu.
   
 20. a

  adoado Member

  #20
  Nov 13, 2010
  Joined: Jul 3, 2010
  Messages: 22
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nashukuru kubaini kuwa bado kuna watanzania wanamapenzi na usomaji wa vitabu jambo ambalo limepotea kwa Watanzania wengi. Nasema hivi waandishi wapo tena wazuri. Mfano mzuri nilikutana na kijana mmoja anaitwa Ahmad Mussa Mniachi. Huyu alikuwa anaandika hadithi nzuri sana, lakini ajabu iliyopo ni kwamba amekuwa akiandika hadithi hizo na kuzisoma yeye mwenyewe kwenye daftari zake. Ndipo nikamlazimisha kutoa angalau moja, kweli sasa nimeanza kuona ameandika hadithi kwenye gazeti la KIU inaitwa mzigo. Bado naendelea kumlazimisha kwa sababu analalamikia maslahi.
   
Loading...