Waandishi wa UHURU na HABARI LEO WALIKUWEPO?

kaburunye

JF-Expert Member
May 12, 2010
672
74
Nimesikia namna gazeti la Uhuru na Habari leo zilivyoripoti Tamko la CHADEMA kutomtambua JK nikashangaa sana maana ni kama vile jamaa waliongea na Dr Slaa mwingine. Kwa mfano uhuru wameandika Chadema yakubali kushirikiana na JK. Hawa jamaa yaani hata habari simple kabisa lazima waichakachue. Habari leo nao utafikiri ni gazeti la CCM, lazima wapindishe habari kuwafurahisha akina MAkamba!!!
 
Ukistaajabu maajabu ya Jakaya utaona ya Makamba! Na ukistaajabu ya Uhuru utaona ya Habari leo au Mtanzania
 
Ilibidi nicheki kalenda upya nilidhani April 1....
Manake kila gazeti liliongelea kukataa kumtambua JK kasoro wao tu...
 
Don't be alarmed, hao nao vibaraka, wanajali maslahi yao; that is how it works for cowards
 
Hayo magazeti yana nia ya kuwaprovoke wana CHADEMA ili wamchukie Slaa. Tunaifahamu hiyo
 
ama kweli nchii basi Magazeti tetu haya Loh!, kuna mtu jana kasema watoza ushuru, waandishi na Watetezi ni wapindisha wa mambo ya wazi, ilimradi wapate kula kwao, wote, na ndio wanasababisha vita, kuachana kwa ndoa siku zote, walilaaniwa tangu Yesu awepo, ukiangalia kwa undani wote tabia ni zile zile hebu chuku;ia waandishi wanaacha mambo muhimu kama kupanda bei holela za mafuta, vyakula lakini wanaona wakiandika Slaa, wakiandika Sitta ndipo watakula
 
Nisha sahau kama hayo magazeti yapo!!!!! Tokea kipindi cha uchaguzi niliacha kununua ikiwa nipamoja nakuyasoma kutokana na habari wazo chapa sijui kama wa hariri wapo:doh:
 
Ndo mana ukienda kwenye vibanda vya magazeti utayakuta yamejaa tele hata ya juzi! nani anunue? mi aku!:nono:
 
Issue hapa si tu kuwa haya magezeti hakuna wa kuyanunua "Habari leo na Daily news" ila yanatumia pesa za walipa kodi! kwa maana hiyo tunahitaji kuyahoji na kujua kwa nini yanachezea pesa za walipa KODI??? kwanini tuyaache yaendelee kupata hasala kwa kuendelea kutumia pesa zetu na kuandika habari ambazo hazina MVUTO kwa jamii ili yauzike???. Mtanzania wa leo haitaji kudanganywa anahitaji kuambiwa UKWELI na ndo hapo utauza gazeti.
 
Back
Top Bottom