Waandishi wa Magazeti na Blogs za michezo acheni udalali wa wachezaji

mmteule

JF-Expert Member
Oct 3, 2011
3,987
2,000
Wapenda soka heshima kwenu,

Kiukweli hao niliowataja wanatia uchungu sana, wamekuwa kama madalali wa nyumba na Viwanja huku Mitaani wanavyotangulia kwa wenye nyumba kuwapanga ili mteja akifika apandishiwe dau. Wanaviingiza vilabu vyetu hasara, mbaya zaidi wanashusha hata viwango vya wachezaji kwa kufanya wasajiliwe kwa bei kuuuuuubwa tofauti na uwezo wao na kusababisha mchezaji kuwekwa kiti moto/underpressure na mashabiki. Wanawaletea wachezaji Migogoro na vilabu vyao. Unajua ikoje........

Mchezaji anapomaliza mkataba wake anamfuata mwanablog/gazeti X la michezo.... kumpa dili, Hatimaye unaanza kusikia Simba yamwekea Mezani Ngoma Mil. 200, Juuuko mikononi mwa Manji kupewa nyumba na Ghorofa Masaki, Ajibu aitwa Ofisini kwa Moo, Kakolanya bila 75 Mil hatii wino nk nk lakini ukweli ni kwamba mambo haya ni ujanja ujanja wa mjini ili watu waendelee kupiga pesa kirahisi. Hebu tuambieni wandishi wetu suala hili linaendelea kukua siku hadi siku mnachofanya mnaona ni sahihi?

Tafakarini
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom