Waandishi wa habari wasikubali kutumika kushiriki siasa chafu arumeru mashariki

Kowakdengo

Member
Mar 20, 2012
21
12
Wadau,

Tukio la gari la waandishi wa habari walio kwenye msafara wa CCM kudaiwa kupopolewa mawe na watu wanaodaiwa kuwa wafuasi wa Chadema ni fedheha kwa fani ya habari nchini kutokana na mashaka ya ukweli wa tukio hilo.

Mashaka hayo yanatokana na sababu kuu tatu:

1. Inawezekanaje gari la waandishi pekee (lisilo na nembo ya CCM kwa mujibu wa maelezo yao wenyewe) lishambuliwe kwa mawe na kuvunjwa vyoo katikati ya magari zaidi ya 10 yaliyokuwa kwenye msafara wa mgombea wa CCM.

2. Aina ya waandishi waliojitokeza kueneza na kuzungumzia taarifa hizo (Eliya Mbonea-Mtanzania, gazeti la Rostam Aziz, Cloude Gwandu ambaye hata hajulikani anaadnikia gazeti gani na alifuata nini kwenye msafara huo (ni mfuasi mwaminifu wa Dk Batilda Burian na Edward Lowasa, mkwe wa mgombea CCM, Sioi Sumari, Charles Ole Ngereza ambaye kwa sifa yake yuko tayari kufanya lolote kushibisha tumbo lake (ana kitambi) na Moses Mashalla ambaye yuko tayari kuandika chochote kwenye gazeti lake analoganga njaa la Mwananchi ili mradi alipwe hata kama habari hiyo inamshushia hadhi yeye binafsi (kuna ushahidi kibao ikihitajika nitaweka hadharani ikiwemo kitendo cha kumgeuka na kumwandika vibaya kwa taarifa za uongo mtoto wa rafiki yake mkubwa, Danford Mpumilwa kwa kulipwa na James Ole Millya)

3. Ni jinsi CCM ilivyokimbilia kulihusisha Chadema na tukio hilo na kulifanya moja ya hoja kuu jukuani huku habari hiyo ikishadadiwa na vyombo vya habari vinavyoaminika kutumiwa kufanikisha malengo ya kundi la mafisadi nchini ambalo linaaminika kumuunga mkono Sioi katika harakati za kutetea kiti cha marehemu babake, Jeremih Sumari ili pamoja na kujifuta machozi ya kufiwa, lakini pia apate ajira itakayomhakikishia ujira wa kutunza familia kubwa aliyoachiwa.

Kwa tathmini yangu ya haraka, CCM ndiyo iliyoandaa, kuratibu na kutekeleza tukio hilo aidha kwa kushirikiana na waandishi hawa niliowataja kwa malipo maalum au baadhi yao ambao walitumika kuwaingiza kingi wenzao ili habari hiyo ichukuliwe kama habari kuu.

CCM ilifanya hivyo kwa sababu kubwa tatu:-

Mosi, kuchonganisha waandishi na Chadema.

Pili, kufanikisha propaganda kwamba Chadema ni chama cha fujo na kukichagua katika uchaguzi huo wa Aprili Mosi ni kuhamishia kile kinachodaiwa ni 'vurugu' za Arusha mjini Arumeru.

Na Tatu kunifanikiwa kupata hoja ya kupanda nayo jukuani baada ya kuona mbinu zote walizojaribu kuwavutia wapiga kura Meru kukwama.

Sababu ya kwanza ya kujaribu kukichonganisha Chadema na Press wamefanikiwa kiasi fulani baada ya baadhi ya waandishi wasiofikiria nje ya kuta za bongo zao kuaminishwa kwamba wenzao walishambuliwa na wafuasi wa Chadema. Lakini hizi mbili za mwisho, yaani propaganda kwamba Chadema ni chama cha fujo na hoja ya kupandia jukuani bado halijaingia vema kwenye vichwa vya wapiga kura na Watanzania wenye kuangalia mambo kwa tafakuri. Wengi wameshtukia mpango huo na badala ya kukichukia Chadema wala kusikiliza propaganda na CCM, sasa wamefanya uamuzi wa kukinyima kabisa kura chama hicho tawala kutokana mtindo wake wa kuwafanya wananchi mahayawani wasioweza kutegua hata mitego ya kitoto kama hiyo.

Tukio hili limenifanya nikumbuke lile la Igunga ambapo viongozi wa CCM waliwachukua waandishi wa habari na kuwapeleka kuwaonyesha nyumba iliyodaiwa kuchomwa moto na wana Chadema na vitu vyote kuteketea isipokuwa kikaratasi iliyokuwa na ujumbe kuwa wachomaji watarejea. Kwamba nyumba na vitu vyote viteketezwe kwa moto, lakini kipande cha karatasi chenye ujumbe kisalie. Hata akili za kiuendawazimu hauwezi kukubabalina na hilo.

Havyo ndivyo CCM inavyojaribu kulinganisha akili, fikra na uwezi wa kufikiri wa Watanzani ndiyo maana hata Mwenyekiti na Rais mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa aliyekaa madarakani kwa miaka 10 aliamua kuwahadaa wana Arumeru kuwa atamsahuri Rais Jakaya Kikwete kufuti hati miliki za mashamba ya walowezi waliokiuka masharti ya umiliki wa ardhi, kazi ambayo yeye alishindwa kuifanya kwa kipindi chote alichokaa madarakani.

Kuonyesha upeo wa dharau na fikra mgando walizonazo viongozi wengi ndani ya CCM na serikali yake, eti Lusinde, mbunge wa Mtera maarufu kwa jina la 'kibajaji' anaowamba wana Meru kumchagua Sioi ili wamfute machozi kwa kufiwa, kumpa ujara wa kulea familia kubwa aliyoachiwa na kumfurahisha Rais Kikwete.

Wakati Lusinde akisema hivyo, alikuwa jukuani na Sioi ambaye kama mfiwa mwenye kuitaji faraja, basi wafariji wangemkuta nyumbani kwao. Vile vile Sioi siyo pekee aliyefiwa Meru, wako waliopoteza wazazi wote na hawana hata uhakika wa mlo mmoja kwa siku. Wengine ni jirani au ndugu wa Sioi ambaye licha ya ukwasi wa marehemu babake, pia anamiliki au kuwa na hisa kwenye kampuni kadhaa na ni mwajiriwa wa moja ya mabenki kubwa nchini kwa nafasi ya ukurugenzi.

Hoja ya kumfurahisha Rais ni tusi kwa wana Arumeru ambalo sipendi kulizungumzia nisijeonekana mie ndio nawatukana. Lakini itoshe tu kuhoji hivi wanaume wa Arumeru watamfurahishaji mheshimiwa Rais ambaye ni mwanamume mwenzao?

Ushauri wangu:

Kwanza Waandishi wa habari wasikubali kutumika kufanikisha siasa chafu zilizojaa hila zinazofanywa na vyama vyote vinavyoshiriki uchaguzi huo mdogo. Watumie kalamu, kamera na vinasa sauti vyao kuelimisha jamii na wapiga kura ili kuwawezesha kufanya chaguo sahihi siku ya kupiga kura kwa kuzingatia mahitaji yao. Wasiangalie rangi za bendera, sare, takrima, ufiwa wala umaarufu wa chama. Wachague mtu anayewafaa bila kujali chama chake. Pamoja na ukweli kwamba chama kama taasisi ni muhimu kiuongozi, lakini uongozi pia ni karama. Siyp kila mtu aweza kuongoza.

Pili, CCM sasa watambue kwamba fikra na uwezo wa tafakuri wa Watanzania umekuwa kulinganisha na enzi za kidumu fikra za mwenyekiti.

Lakini mwisho ni kwa wakuu wa vyumba vya habari nchini kujiahadhari na kutafakari taarifa wanazopelekewa na waandishi wao. Siyo kwa masuala ya uchaguzi huu mdogo pekee, bali kila siku kwa sababu wengi wa wawakilishi wao wako tayari kufanya na kuandika lolote ili mradi wanashibisha tumbo zao.

Naendelea kufuatilia suala hilo nitawajuza kwa kirefu matokeo yake.......

Wadau nawasilisha tutafakari.
 
Umeandika vema sana mkuu!

Haiingii akilini hata kidogo, eti, gari la waandishi kushambuliwa, hapa ccm amejiccm na kwa kulitumia jeshi la polisi wanakuja na dhahania mfu 'wafuasi wa cdm kushambulia gari la wanahabari'.

Waandishi wengi bongo, kutokana na kulipwa malipo na chama (chombo anachofanyia kazi) usitegemee akaandika habari yenye uchambuzi yakinifu. hapa tegemea ukasuku:violin:
 
Jambo jipya lililojitokeza wakati nikiendelea na uchunguzi wangu kuhusu tukio la gari la waandishi kudaiwa kupigwa mawe ni kwamba waandishi watatu waliojitokeza kushadadia tukio hilo kwenye vyombo vya habari, yaani Mbonea, Gwandu na Ngereza wote ni viongozi wa juu wa klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Arusha inayojulikana kama Arusha Press Club (APC).

1. Gwandu - Mwenyekiti
2. Mbonea- katibu mkuu
3. Ngereza- Makamu Mwenyekiti

Mashala yeye nimeelezwa kwamba ni mjumbe wa kamati ya utendaji.
Kwa mukhtadha huu, je, tuamini kwamba CCM imekilipa fedha APC kukifanyia propaganda kwa gharama ya shida, taabu na mihangaiko ya wana Arumeru au ni tabia ya ufisi maji wa hawa viongozi ambao wameamua kutumia matumbo yao kuwazia. (afadhali wanaotumia Masaburi walikuwa wakitetea maslahi ya umma wa Dar-UDA)

Tungependa kupata kauli ya waandishi wa Arusha kwa pamoja au mtu mmoja mmoja kuhusu ushiriki wao katika mpango huu haramu ambao ungeweza hata kusabisha maafa iwapo kungetokea majibizano kati ya watekelezaji wa mpango huo haramu na wana CCM safi ambao hawakushirikishwa kwenye jambo hilo ambao wangejitokeza 'kuwatetea' waandishi wasishambuliwe.

kila nikipata data nitaendelea kuwajuza.....


 
Ahsante sana kwa kutufumbua macho ikifika mahali waandishi wa habari wakaanza kupigishwa kwata na wenye pesa wanaweza hata kufuramishwa bila yao kupenda haitoshi mwandishi ukafanya dhuluma na dhambi kubwa ya aina hiyo wakati umma unakutegemea,kuna siku yatakuja kuwatokea puani waandishi hawashindi nguvu ya umma ,ndio waliandika mbona habari yenyewe,haikupewa uzito wowote na wananchi propaganda za kijinga sana hizo
 
Hata kama ni kweli walipigwa mawe, je kwa kutumia common sense waandishi hao watakua walipigwa kwa sababu wao ni waandishi?????
 
Hoja mpya kuhusu gari la waandishi wa habari kupigwa mawe:

Waandishi wa habari mkoa wa Arusha sasa wanafanya uchunguzi kubaini iwapo viongozi wao (Mwenyekiti Gwandu, makamu wake, Ngereza na Katibu Mkuu, Mbonea walitumika kutekeleza propaganda ya CCM kuhusu tukio hilo.

nitawajuzi wadau..
 
Back
Top Bottom